1 Dec 2020 in Senate:
Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. I second the Motion that has been put forth by the Senator for Murang’a, who is the Senate Majority Whip. It is true that we still have some business that is pending and it is only fair that we give Senators in the House ample opportunity to make contributions to the Adjournment Motion. I second.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Asante sana Bw. Spika wa Muda. Nitajitahidi sana kuendelea na kumaliza katika lugha ile ya kitaifa ya Kiswahili. Nataka kumshukuru Rais kwa ile Hotuba ambayo alitoa. Hii ni kwa sababu alitueleza kwamba katika huu mwaka ambao alikuwa anatupa ripoti hii ambayo ilisomwa tarehe 12 Mwezi wa 11 mwaka wa 2020, Serikali ilikuwa imeweka mikakati ya kununua madawati ya shule 250,000. Hii ni ili kuhakikisha kwamba watoto wetu watakapokuwa wanarudi shule mwaka ujao, watakuwa na nafasi ya kuwa na ule umbali wa mita moja na nusu. Hiyo ni ili kusiwe na madhara katika shule kupitia ugonjwa huu wa Coronavirus (COVID-19).
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nimejaribu kutembea katika Kaunti yangu ya Nyamira na nimeona kwamba kweli kuna shule nyingi sana katika Kaunti yangu ambazo bado hazijakuwa na nafasi ya kupewa madawati. Kwa hivyo, naomba wale ambao wanasimamia Wizara ya Elimu wafanye jitihada kuhakikisha kwamba madawati haya yapelekwe kwatika kaunti zote 47 zenye ziko katika nchi ya Kenya. Hatutaki kusikia kwamba madawati haya yamegawa katika kaunti fulani na kwamba kuna kaunti zingine ambazo hazijakuwa na nafasi ya kupata madawati haya.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, hoja nyingine ambayo ningetaka kuguzia katika ile Hotuba ya Rais ni kuhusiana na jitihada ambayo Serikali yake imeweza kufanya kupigana na hili janga la COVID-19. Nakubali kwamba Rais alipoanza kushughulikia ugonjwa wa COVID-19 alianza kusaidia wakenya ambao walikuwa wanaathiriwa na hili janga. Aliweka mikakati rasmi ya kuwalinda Wakenya, haswa mambo ya kupunguza kodi na kuhakikisha kwamba watu walikuwa wanawekewa amri ya kutokutana ama kutembea kutoka kaunti moja hadi nyingine.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Asante sana Bw. Spika wa Muda. Mimi nawazungumzia watoto kule Kaunti ya Nyamira na Nairobi ambao wamezoea ile Kiswahili ya Sheng . Nataka kuwatia moyo kwamba Serikali imeweka mikakati maalum ya kuhakikisha kwamba wakirudi shuleni mwaka ujao, hawatakuwa kwenye hatari ya kupata ule ugonjwa wa COVID-19. Nikimalizia kuhusu COVID-19, ningemuomba Rais wetu aangalie upya ile mikakati ambayo imewekwa kuthibiti huu ugonjwa wa COVID-19, haswa wakati huu ambapo tunaelekea katika ule msimu wa Krismasi. Kutakuwa na watu wengi ambao watakuwa wanakusanyika wakiwa katika sherehe za kuburudika na familia na marafiki. Bw. Spika wa Muda, lakini hatari yenye iko ni kwamba, wataki ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
Nikizungumza kama Seneta wa Kaunti ya Nyamira, nataka niwashukuru sana. Hii ni kwa sababu tulipopata hii ripoti mara ya kwanza sisi hatukuwa tumeongezewa eneo Bunge katika kaunti yetu ya Nyamira. Lakini baada ya wengine wetu kuteta sana na kusema kwamba hatungekubali hii BBI kama hatungekuwa na eneo Bunge limeongezwa kule Kaunti ya Nyamira, nafurahi sana kusema kwamba sasa Kaunti yetu ya Nyamira imeongezewa eneo moja la Bunge. Ikiwa BBI itapita, sisi watu wa Kaunti wa Nyamira tutarudi hapa tukiwa na eneo Bunge na wawakilishi watano na sio wane. Pia nafurahi sana kwamba Kipengele 11 sasa kinaongea kuhusu maneno ya kilimo. ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
Hii ni kwa sababu hii kampuni ya Kenya Power Company hata kama tumeipatia jukumu la kuunganisha umeme kwa Wakenya, imeonyesha wazi kwamba haina uwezo. Wakati umewadia ambapo inatakikana tukubali kwamba kampuni ingine ije ili iweze kusaidia katika hii shughuli ya kuunganisha umeme katika maeneo mbali mbali katika taifa letu la Kenya. Bwana Spika wa Muda, katika maneno ya kupigana na umasikini na upweke kwa vijana, namshukuru Rais vile amesema sasa hivi hapa Kenya tuko na wale vijana ambao wanafanya kazi ya boda boda . Wanazidi sasa million moja nukta nne. Hao vijana wenyewe wanaleta katika uchumi wa taifa letu karibu ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
. Bw. Spika wa Muda, nataka nikuambie kwamba hata Ijumaa iliopita nilikuwa katika Kaunti yangu ya Nyamira nikitembea kutoka soko moja inaitwa Ikonge, nikatokea katika barabara nyingine inatokea katika kampuni ya Kipkebe. Hapo kati kati, kuna maaskari wameweka kizuizi. Hao vijana wanasema kuwa kila mara wanapopita pale wanatoa kodi ya Kshs50. Wengine wanatoa Kshs100. Huo sio ungwana kabisa. Baadhi ya vijana hao wamesoma sana lakini wanafanya kazi ya boda boda kwa sababu Serikali yetu haijaweka mikakati ya kutosha ya kupata ajira ya kutosha kwa vijana wetu. Bw. Spika wa Muda, naomba Mkuu wa idara ya polisi ahakikishe kwamba mambo ya ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ningependa. Nampa nafasi rafiki yangu, Seneta wa Kaunti ya Nairobi.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nimefurahi sana na hiyo taarifa ya kujulishwa na Seneta wa Nairobi. Kwa hakika ni aibu sana kuona kwamba maaskari wetu ambao wanatakikana kutulinda na kuhakikisha kwamba wale wanafanya biashara hawatishwi, ndio wanawatesa vijana wetu. Nafikiri kama Mwenyekiti wa Kamati wa Haki wiki ijayo sisi tutafunga safari hadi ofisi ya Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC). Hii ni ili tujue ni jitihada gani zitawekwa na ile ofisi kuhakikisha kwamba maaskari wetu ambao wako katika barabara zetu na vizuizi hawawatesi vijana wetu wa boda boda . Bw. Spika wa Muda, hii ni kwa sababu hakuna haja ya kukubalia kitengo ...
view