1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nimejaribu kutembea katika Kaunti yangu ya Nyamira na nimeona kwamba kweli kuna shule nyingi sana katika Kaunti yangu ambazo bado hazijakuwa na nafasi ya kupewa madawati. Kwa hivyo, naomba wale ambao wanasimamia Wizara ya Elimu wafanye jitihada kuhakikisha kwamba madawati haya yapelekwe kwatika kaunti zote 47 zenye ziko katika nchi ya Kenya. Hatutaki kusikia kwamba madawati haya yamegawa katika kaunti fulani na kwamba kuna kaunti zingine ambazo hazijakuwa na nafasi ya kupata madawati haya.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, hoja nyingine ambayo ningetaka kuguzia katika ile Hotuba ya Rais ni kuhusiana na jitihada ambayo Serikali yake imeweza kufanya kupigana na hili janga la COVID-19. Nakubali kwamba Rais alipoanza kushughulikia ugonjwa wa COVID-19 alianza kusaidia wakenya ambao walikuwa wanaathiriwa na hili janga. Aliweka mikakati rasmi ya kuwalinda Wakenya, haswa mambo ya kupunguza kodi na kuhakikisha kwamba watu walikuwa wanawekewa amri ya kutokutana ama kutembea kutoka kaunti moja hadi nyingine.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Asante sana Bw. Spika wa Muda. Mimi nawazungumzia watoto kule Kaunti ya Nyamira na Nairobi ambao wamezoea ile Kiswahili ya Sheng . Nataka kuwatia moyo kwamba Serikali imeweka mikakati maalum ya kuhakikisha kwamba wakirudi shuleni mwaka ujao, hawatakuwa kwenye hatari ya kupata ule ugonjwa wa COVID-19. Nikimalizia kuhusu COVID-19, ningemuomba Rais wetu aangalie upya ile mikakati ambayo imewekwa kuthibiti huu ugonjwa wa COVID-19, haswa wakati huu ambapo tunaelekea katika ule msimu wa Krismasi. Kutakuwa na watu wengi ambao watakuwa wanakusanyika wakiwa katika sherehe za kuburudika na familia na marafiki. Bw. Spika wa Muda, lakini hatari yenye iko ni kwamba, wataki ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
Nikizungumza kama Seneta wa Kaunti ya Nyamira, nataka niwashukuru sana. Hii ni kwa sababu tulipopata hii ripoti mara ya kwanza sisi hatukuwa tumeongezewa eneo Bunge katika kaunti yetu ya Nyamira. Lakini baada ya wengine wetu kuteta sana na kusema kwamba hatungekubali hii BBI kama hatungekuwa na eneo Bunge limeongezwa kule Kaunti ya Nyamira, nafurahi sana kusema kwamba sasa Kaunti yetu ya Nyamira imeongezewa eneo moja la Bunge. Ikiwa BBI itapita, sisi watu wa Kaunti wa Nyamira tutarudi hapa tukiwa na eneo Bunge na wawakilishi watano na sio wane. Pia nafurahi sana kwamba Kipengele 11 sasa kinaongea kuhusu maneno ya kilimo. ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
Hii ni kwa sababu hii kampuni ya Kenya Power Company hata kama tumeipatia jukumu la kuunganisha umeme kwa Wakenya, imeonyesha wazi kwamba haina uwezo. Wakati umewadia ambapo inatakikana tukubali kwamba kampuni ingine ije ili iweze kusaidia katika hii shughuli ya kuunganisha umeme katika maeneo mbali mbali katika taifa letu la Kenya. Bwana Spika wa Muda, katika maneno ya kupigana na umasikini na upweke kwa vijana, namshukuru Rais vile amesema sasa hivi hapa Kenya tuko na wale vijana ambao wanafanya kazi ya boda boda . Wanazidi sasa million moja nukta nne. Hao vijana wenyewe wanaleta katika uchumi wa taifa letu karibu ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
. Bw. Spika wa Muda, nataka nikuambie kwamba hata Ijumaa iliopita nilikuwa katika Kaunti yangu ya Nyamira nikitembea kutoka soko moja inaitwa Ikonge, nikatokea katika barabara nyingine inatokea katika kampuni ya Kipkebe. Hapo kati kati, kuna maaskari wameweka kizuizi. Hao vijana wanasema kuwa kila mara wanapopita pale wanatoa kodi ya Kshs50. Wengine wanatoa Kshs100. Huo sio ungwana kabisa. Baadhi ya vijana hao wamesoma sana lakini wanafanya kazi ya boda boda kwa sababu Serikali yetu haijaweka mikakati ya kutosha ya kupata ajira ya kutosha kwa vijana wetu. Bw. Spika wa Muda, naomba Mkuu wa idara ya polisi ahakikishe kwamba mambo ya ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ningependa. Nampa nafasi rafiki yangu, Seneta wa Kaunti ya Nairobi.
view
1 Dec 2020 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nimefurahi sana na hiyo taarifa ya kujulishwa na Seneta wa Nairobi. Kwa hakika ni aibu sana kuona kwamba maaskari wetu ambao wanatakikana kutulinda na kuhakikisha kwamba wale wanafanya biashara hawatishwi, ndio wanawatesa vijana wetu. Nafikiri kama Mwenyekiti wa Kamati wa Haki wiki ijayo sisi tutafunga safari hadi ofisi ya Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC). Hii ni ili tujue ni jitihada gani zitawekwa na ile ofisi kuhakikisha kwamba maaskari wetu ambao wako katika barabara zetu na vizuizi hawawatesi vijana wetu wa boda boda . Bw. Spika wa Muda, hii ni kwa sababu hakuna haja ya kukubalia kitengo ...
view
1 Dec 2020 in Senate:
chifu wajaribu kuwadhulumu Wakenya wenzao. Hii sheria tutaenda kule na kuongea na watu wetu kule tunatoka na tutaipitisha kwa amani. Hatutaki Wakenya washurutishwe. Huu ni mjadala ambao uko na wafuasi wengi. Tungetaka Wakenya wapewe nafasi yao waweze kuchukua hatua ya kidemokrasia. Kuna wengi ambao wataipigia kura. Kuna wale wanaoipinga, ambao nafikiri ni wachache. Wakiikataa basi hiyo pia ni demokrasia. Tumepata eneo Bunge mpya katika jimbo la Nyamira. Tumeambiwa kuwa mambo ya wakulima wa majani chai watashughulikiwa. Kwa hivyo, tutaungana na Wakenya wengine kuhakikisha kwamba tunawapatia wetu nafasi ya kusoma vitabu vya the Building Bridges Initiative (BBI). Wakiona kwamba wanafurahishwa na ...
view
24 Nov 2020 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise pursuant to Standing Order No.48(1) to seek a Statement from the Standing Committee on Health regarding the death of Ms. Martha Kemunto Ochoki at the Nyamira County Referral Hospital. In the Statement, the Committee should- (1) Investigate the circumstances leading to the death of Ms. Martha Kemunto Ochoki who passed away while giving birth at the Nyamira County Referral Hospital on 24th October, 2020. (2) Explain why the deceased was neglected by medics during her stay at the hospital and further not given immediate medical attention when her situation deteriorated leading to her death. (3) ...
view