Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 272.

  • 5 Apr 2022 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Wakenya wamekumbwa na majanga mengi, likiwemo janga la korona na ukame. Leo hii kuna uhaba wa mafuta nchini. Nilisafiri juzi. Nilikuwa miongoni mwa watu waliopanga foleni ndefu kusubiri mafuta. Kule nitokako, wale wanaoathirika zaidi ni watu wanaondesha boda boda. Bi. Spika wa Muda, kwa kweli, Hoja hii imefika wakati mwafaka. Sen. Kang’ata ameleta Hoja hii wakati unaofaa kwa sababu hili ni janga ambalo limetukumba. Endapo ulipata muda wa kutembea katika sehemu za Nairobi, katika vituo vya kuuza mafuta, mtu alikuwa anawekewa mafuta ya Ksh1,000 pekee ili watu wengine waweze kupata ... view
  • 5 Apr 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 5 Apr 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, namuunga mkono Sen. Kang’ata. Vile vile, nampa kongole kwa kuleta Hoja hii kwa wakati unaofaa. Asante kwa kunipa nafasi. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Madam Deputy Speaker, I am on request. I would have liked to comment on the cultural things, but you we went ahead and gave another statement. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Thank you, Madam Deputy Speaker. That is okay. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi. Naunga mkono Taarifa ya Sen. Khaniri. Hakika, sisi kukuza mali yetu kama Wakenya na pia talanta zetu ndani ya Kenya ni jambo muhimu kuliko kuleta vitu kutoka nje. Biashara nyingi zimekuwa za watu wa kutoka nje, hasa Wachina nchini. Kama vile Senata mwenzangu alivyosema, sisi pia Wakenya tumeingia katika ubumbuwazi wa akili ya kwamba vitu vya Kenya ni vitu ambavyo havifai. Ndio kwa sababu wengine wanasema hawawezi kuvaa nguo ambazo zinatoka Kenya, mpaka wavae nguo za nje. Ni jambo la busara kukuza talanta na biashara zetu ndani ya Kenya. Hii ... view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi. Naunga mkono Taarifa ya Sen. Kasanga. Kwa kweli, uraibu wa vitu vya kisasa, hasa na vijana, umekuwa changamoto katika jamii. Kuna uraibu wa aina mbali mbali. Mara nyingi watu huwa na uraibu wa pombe na mambo mengine kadha wa kadha. Jamii ya kesho, ambayo ni vijana wa leo, ina kasumba ya ulevi na uraibu wa vitu tofauti tofauti. Kwa hakika, vijana hao ni wazembe kwa sababu ya ulevi na uraibu wa vitu vingine. Iwapo jambo hili halitaangaliwa kwa kina ili kukomesha vijana kutokana na uraibu wa vitu tofauti tofauti, basi siku zijazo ... view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Wakenya wengi wako gizani na wanataka kujua mwelekeo wa ujenzi wa hii Expressway. Hii Expressway ambayo imejengwa kutoka huko uwanja wa ndege wa JKIA na kupita hapa nyuma ya Bunge ndio barabara ninayotumia nikitoka nyumbani kwangu. Wakenya wengi wanauliza kuhusu ujenzi wa hii Expressway. Kwa lugha ya Kiswahili express inamaanisha kupita moja kwa moja bila kusimama. Najua Bw. Spika wa Muda ni Mswahili na anaweza kufafanua vizuri haya mambo ya Expressway. Hii Expressway ilikuwa ikamilike Desemba mwaka jana na itumike lakini mpaka leo tunaona bado watu wanaendelea kuijenga. Nadhani huu mradi ... view
  • 2 Mar 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: tulielezwa kuwa Desemba kazi hii itakuwa imeisha na bado haijaisha. Inaonekana hata hii Desemba ijayo hii kazi haitakuwa imekamilika. Tulitaka matunda ya Rais Uhuru, kuja kutuonyesha magari ikipita juu. Ile kazi inayoendelea sio mbaya; ni nzuri. Ni kama hiyo barabara imepata gorofa. Watu wanatembea chini ya gorofa lakini huko juu utendekazi na usafiri hujaanza. Wanakenya wengi wako katika giza, hawajui wakati barabara itaanza kutumiwa. Wengine wanasema kuna majumba yamejengwa ya kulipia pesa pale mbele. Sasa wanaulizana kama watatembea juu kwa Expressway ama chini. Haijulikani ni Wakenya wagani wataenda juu kwa malipo na wagani watatumia chini. Tunataka ufafanuzi kwa kina, vile ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus