2 Feb 2022 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nichangie maneno yangu mawili matatu katika Mswada huu. Vile vile, ningependa kutoa shukrani ama kumpa kongole Mhe. aliyeleta Mswada huu, kwa sababu umefika kwa wakati wake. Kabla sijaanza kuzungumza, ningependa kutoa salamu za rambirambi kwa kisa kilichotokea Mvita. Tunaomba Mwenyezi Mungu awaweke mahala pema wale waliotangulia .
view
2 Feb 2022 in National Assembly:
Watu wanaohudumu katika nchi hii kwa njia ngumu na ya matatizo ni wahudumu wa afya wa jamii. Mswada huu ukipata nafasi ya kufika kwenye Bunge hili ni kwa sababu sisi ni wawakilishi, na kule chini nyanjani sisi ndio tunaona vile hawa wafanyikazi ambao wamejitolea wanavyofanya kazi. Mazingira yao ni magumu na hawana vifaa vya kufanya kazi. Kama juzi wakati wa Corona, hawa ni kati ya wale wafanyikazi waliojitokeza kuwa tayari kuhudumia wananchi kwa njia yoyote. Kwanza, walikuwa wametia maisha yao kwenye hatari. Pili, walikuwa wamejitolea kwa sababu kila tunapo ondoka katika mitaa yetu ama katika sehemu tunazoishi kwa sababu pengine ...
view
2 Feb 2022 in National Assembly:
Sisi, kama Bunge la Kitaifa, tuko na nguvu ya kupanga bajeti na ya kutatua maswala yanayotoka nyanjani. Lakini, kwa maswala kama haya ambayo wale wanaotokwa na jasho jingi katika nchi hii ni wale walio nyanjani, kwa mfano, c ommunity health workers, w azee wa mitaa na mabalozi wa vijiji…Mfano mzuri ni kama kobe. Unajua kobe akicheza, ndani yuko kama mkakasi. Akiwa anapiga ngoma, atapiga ngoma kule ndani lakini huwezi kujua kama anacheza mpaka uone jasho linamtoka. Hao wafanyikazi, c ommunity health workers, wanafanya kazi kubwa sana kwa sababu sehemu tunazotoka ni sehemu ambazo, kwa mfano, hazina barabara na d ispensaries ...
view
2 Feb 2022 in National Assembly:
na tulifanye kuwa swala litakalosimamiwa na Serikali kuu ili tukiweka bajeti, Serikali kuu iweke mikakati sawa kuhakikisha kuwa pesa hizo zinatiririka mpaka nyanjani. Nikimalizia, huenda hili likawa nje ya mada, kule kwangu, kwa sababu wakati wa siasa umefika, kuna sehemu inayoitwa Miongoni sehemu ya Kidomaya. Hii ni sehemu ambayo iko na shamba ambalo limekuwa na utata. Ni shamba la Parbat. Hili shamba lease yake iliisha. Hakuna
view
2 Feb 2022 in National Assembly:
ambayo yaweza kupitishwa, kuregeshwa au kuongezwa bila ya kupitia c ounty government . Lakini, yasemekana kuwa kuna familia zaidi ya elfu moja na mia mbili amabazo ziko hatarini. Ningependa Bunge hili la Kitaifa liliangalie swala hili kiundani. Niko katika Kamati ya Mashamba, na hili ni swala ambalo tuko nalo mezani. Kupitia kwako, naomba Waziri wa Mashamba atuletee ripoti ya swala hili ili tujue kama hii lease ya Parbat ilikuwa extended au
view
2 Feb 2022 in National Assembly:
na ilifanyika kwa mikakati gani nam katika Serikali gani. Serikali ya c ounty mpaka sasa hivi imekataa. Gavana Mvurya, ambaye ni Gavana wa Kwale, amesema hajatia kidole kwa lease hiyo kupeanwa. Sasa hivi tunavyozungumza, wananchi wengi wamewekwa katika senyeng’e, yaani katika fence, na wakati wowote wanaweza kufurushwa. Ikiwa Serikali haitaweza kuchukua mkondo wake na kutumia nguvu zake, sisi kama viongozi na wananchi tunaokaa sehemu hiyo tutatumia njia ambayo sidhani itakuwa njia sawa. Kwa hayo machache, nashukuru. Naunga mkono Mswada huu.
view
7 Oct 2021 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. I rise to present a Public Petition regarding appeal for land adjudication in Wasini Island. I, the undersigned, on behalf of residents of Wasini Island, draw the attention of the House to the following:- The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
7 Oct 2021 in National Assembly:
That Wasini Island, which is also known as Wasini Mkwiru Island, is located near Shimoni town in the Coastal Region and covers approximately 289 acres of land registered as Provincial Plot No. PW 33/Wasini Island, that sustains a community of over 300 families. That, on 31st October 1979, the then Kwale District Lands Adjudication Office declared Wasini Island an adjudication area pursuant to Section 5 of the Land Adjudication Act, which implied that all rights and interests within the adjudication section were to be strictly observed as required by law. That the Island was thereafter surveyed and adjudicated by the ...
view
10 Aug 2021 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. I would like to table the Report of the Departmental Committee on Lands on its consideration of: (a) Public Petition of Residents of Tetu Sub-County regarding resettlement of squatters of Tucha Kiandangoro Forest on Solio Ranch Village. (b) Public Petition by residents of Ndindiri, Makata and Kaole Village in Chasimba Ward, Kilifi South Constituency, regarding disposition of land belonging to residents of Ndindiri and Kaole villages. (c) Public Petition by residents of Chidondo, Junju, Mrima and Bodio villages of Kilifi South Constituency regarding resettlement of the residents. Thank you, Hon. Speaker.
view
6 May 2021 in National Assembly:
Napiga kura ya ndio.
view