Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.
2 Aug 2023 in National Assembly:
(Likoni, ODM)
view
6 Jul 2023 in National Assembly:
(Likoni, ODM)
view
9 Jun 2022 in National Assembly:
There is nothing out of order. I am looking at the time and standing under Standing Order No. 95. Looking at the mood of the House, I see everybody is supporting this Report. I request the Mover to reply so that the House can adopt this Report. I am looking at the time.
view
7 Jun 2022 in National Assembly:
(Likoni, ODM); Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kuafiki Ripoti hii ya Kamati ya kuangalia uwekezaji wa Umma katika utumizi wa fedha za umma. Kamati hii ni muhimu sana, kwa sababu inaangalia takriban mashirika thelathini ya Serikali. Naunga mkono ripoti hii, kwa sababu imeangazia mambo ya kimsingi sana katika utumizi wa fedha za umma, na katika uwekezaji wa mambo ya umma au ile miradi ya umma ambayo inafanyika katika takriban mashirika thelathini. Mwenyekiti amezungumzia sana changamoto ambazo tumezikumba baada ya kupata Ripoti ya Auditor-General, ambayo huwa anaangazia mashirika haya thelathini katika utumizi wao wa pesa wakati wanaweka uwekezaji ...
view
7 Jun 2022 in National Assembly:
Vile vile, Mhe. Naibu Spika wa Muda, katika haya mambo ya kupeana zabuni katika kutengeneza miradi, tumeona ya kwamba kuna maofisa ama wale wahusika ambao hawafanyi ile mipango mahsusi, ambayo tunaita feasibility studies kwa Kiingereza. Inafika wakati mradi huo unakuwa ni mgumu sana kutekelezwa na Serikali.
view
7 Jun 2022 in National Assembly:
Vile vile, tumeona kunakuwa na tofauti katika kulipa fedha ambayo tunaita variation kwa Kiingereza, kwa wale ambao hawataelewa. Hii tumeona sana katika shirika la Kenya Rural Roads Authority (KeRRA), Kenya National Highways Authority (KeNHA), Kenya Urban Roads Authority (KURA), na mashirika mengine mengi katika mambo ya barabara. Hiyo ni mifano tu ambayo natoa. Tumeona ya kwamba Serikali ya Kenya inapoteza fedha nyingi sana. Hivyo basi, tumeweka mapendekezo na kusema ni hatua ngani za kisheria ambazo zitachukuliwa, haswa kwa wale wahusika wa mambo kama haya.
view
7 Jun 2022 in National Assembly:
Vile vile, tumeona ya kwamba mashirika thelathini yetu ya Serikali hayakupata umiliki wa majengo na ardhi yao. Kwa mfano, kuna Shirika la Reli, ama Kenya Railways . Nyumba na ardhi zao nyingi zimechukuliwa na watu binafsi kiholela. Hiyo ni rasilimali ya Wakenya, lakini imechukuliwa kiholela.
view
7 Jun 2022 in National Assembly:
Mhe. Abdullswamad amezungumzia kinaga ubaga kuhusu Shirika la KenGen. Wako na visima vya nguvu ya mvuke ambavyo wangetumia kwa miradi, lakini mashirika ya kibinafsi yalipatiwa zabuni ile. Hivyo basi, Kenya inapoteza fedha nyingi sana ambazo zingetumia kufanya mradi mwingine.
view
7 Jun 2022 in National Assembly:
Pia tumeona ya kwamba kuna wakati mwingine tunapata kuwa hakuna maafisa wa hesabu, ama wale tunaita accounting officers kwa Kiingereza, katika mashirika mengi ya Serikali. Hivyo basi, hata wakati wanafanya ile miradi, watu ambao wanatoa maamuzi ni maofisa ambao sio wahasibu. Hata ukiangalia hesabu zao, unakuta kuwa kuna changamoto na tofauti nyingi sana. Lazima mashirika yaangaliwe na yapigwe msasa tuone utumizi wao. Shirika la KAA lina mradi wa Greenfield, ambao ulileta changamoto nyingi sana. Kuna fedha nyingi zilipotea hapo. Pia, kuna yale mambo tunaita variation, ama tofauti nyingi ambazo The electronic version of the Official Hansard Report is for information ...
view
7 Jun 2022 in National Assembly:
zimetokea. Kama kungefuatwa sheria vile inavyotakikana, basi suala kama hili lisingetokea kabisa.
view