Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 424.

  • 8 May 2025 in Senate: Bw. Spika, nami ningependa kuongezea maoni yangu kuhusu Taarifa iliyoletwa na Sen. Omtatah. Vile vile katika gazeti hilo, Kiwanda cha Mchele cha Mwea kimeorodheshwa kama mojawapo ya viwanda ambavyo vinafaa kubinafsishwa. view
  • 8 May 2025 in Senate: Babu yangu ni mmoja wa wale waliopeana mashamba na vile vile kuchangia katika kujengwa kwa kiwanda hicho. Kwa hivyo, Serikali inapoamua kukiuza, ni vyema tujue ni kwa jinsi gani wale waliopeana mashamba kwa hiari watafaidika. Nikikupa shamba ufanyie kitu fulani, ikiwa huna haja nalo tena, unafaa kunirudishia mimi niliyekupa kwa sababu sikuuza. view
  • 8 May 2025 in Senate: Jambo la pili ni kuwa kuna mchango uliofanyika ili kuhakikisha kuwa kiwanda hicho kinaendelea. Wengi wa watu hao huzikwa makaburini. Sisi kama Wakikuyu kutoka Kirinyaga tunashika mashamba yetu. Tulipeana mashamba na sasa watu wanakaa vijijini ambako hawana hata mahali pa kuzikwa. view
  • 8 May 2025 in Senate: Ni vyema kwa watu hao waliokuwa na roho nzuri kuhusishwa kwa jambo kama hili. Waliobaki kama sisi tunafaa kuitwa kwa sababu kuna wengine waliotutangulia kwenda ahera. Tunafaa kupeana maoni yetu kwa sababu wale waliobaki hawataki uwanja huo uuzwe. view
  • 8 May 2025 in Senate: Jambo la tatu ni kuwa kuna viwanda ambavyo vimejengwa kule Sagana. Tunaambiwa kuwa tunafaa kwenda huko kutafuta huduma kwa sababu shamba lililoko Mji wa Ngurubani linapakana na maghala ya Halmashauri ya Nafaka, mahali ambapo wakulima wanaenda kuchukua mbolea ya ruzuku. Pahali hapo panaposemekana kuwa katikati ni Zaidi ya kilomita 30. Ni kama kutoa jikoni karibu na sebule na kuipeleka karibu na bafu. Inafaa kuwa mahali ambapo unaweza kutembea. view
  • 8 May 2025 in Senate: Sisi tungetaka huduma zinazopelekwa katika kiwanda hicho zibaki pale pale. Kama wakulima wataamua kwamba kiwanda hicho kipeanwe, basi wanafaa kuhusiswa kikamilifu ili waamue kama kitatolewa au la. view
  • 8 May 2025 in Senate: Asante sana Bw. Spika. view
  • 2 Apr 2025 in Senate: Asante, Bw. Spika. Swali langu linahusu muda. Bw. Waziri, waswahili husema, mnyonge mnyongeni na haki yake mpe. Umesema ya kwamba kuna mazungumzo ambayo yanaendelea ili kuhakikisha kwamba wale ambao hawakulipwa pesa zao waweze kuzipata. Ukipiga hesabu, utapata ya kwamba takriban miaka 27 zimeisha. Wengi wao walikufa wakingojea pesa zao. Bw. Waziri, ingekuwa wewe, ungeweza kungoja pesa kwa miaka karibu 30 ilhali uko na matumizi ya hizo pesa? Je, inawezekana utupe muda ambao unaona kama unakadiria? Hili jambo linaweza kumaliziwa ili hawa watu waweze kufaidika na pia waweze kupata nafuu kwa sababu pesa zao zimekaa kwa muda mrefu sana. Nchi hii ... view
  • 2 Apr 2025 in Senate: Asante sana, Mstahiki Spika, kwa kunipa nafasi kuchangia na kutoa tafsida yangu kwa Taarifa iliyoletwa na Sen. Orwoba. Wakati huu nchi inapambana kuhakikisha kwamba vijana na wananchi kwa jumla wanapata kazi hapa na nchi za nje. Ni jambo la aibu kuona watu wakiritimba wamejipanga kuhadaa Wakenya. Hakuna jambo mbaya kama mawakala tisa wameungana na benki tatu kuhakikisha kwamba wamewalaghai wanaotafuta kazi. Waziri wa Leba na Maslahi ya Jamii anafaa kujua mambo haya yote kabla hayajafika hapa. Kama amemakinika anafaa kujua kuna jambo linaendelea kule nje na Wakenya wanapoteza fedha zao. Bwana Spika, mambo ni wawili- iwe anafahamu kinachoendelea au la. ... view
  • 2 Apr 2025 in Senate: Tunao ushahidi ni akina nani wanafanya mambo hayo. Tunajua inaendelezwa katika ofisi zipi. Wanaotenda hayo wanafanya sinema ya Kichina kutuonyesha wanavyopeleka watu nchi za nje. Watoto wetu bado wako kule mashinani na pesa zao zimepotea. Benki inaitisha Shilingi 5,000 kutoa mkopo ili ilipe moja kwa moja kwa wale mawakala bila kupitia kwa wale wanaotafuta kazi. Imefika wakati ambao sisi kama Seneti tunafaa kusimama tusichukuliwe kama wanasesere kwa sababu tunajua tunayofanya. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus