16 Dec 2008 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I rise on a point of order. Is it in order for us to continue with this debate, having read the mood of hon. Members? Standing Order No.21(1) provides as follows:- "A Member who wishes to postpone to some future occasion the further discussion of a question which has been proposed from the Chair may claim to move "That, the debate be now adjourned," or, in the Committee of the Whole House "That, the Chairman do report the progress." Mr. Speaker, Sir, this is at your discretion, but we can still use our Standing Orders to enable ...
view
16 Dec 2008 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I beg to move a Motion for adjournment of debate under Standing Order No.21(1). Standing Order No.21(1) says:- "A Member who wishes to postpone to some future occasion the further discussion of a question which has been proposed from the Chair may claim to move "That, the debate be now adjourned," or, in the Committee of the Whole House "That, the Chairman do report the progress." Mr. Speaker, Sir, having said that, I beg to move:- THAT, debate on the Motion be adjourned.
view
16 Dec 2008 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, you have said it. Already I know in the Supplementary Order Paper there is a Motion of Adjournment of the House where we will go for recess. Mr. Speaker, Sir, however, the adjournment I am seeking now does not recognise that Motion that is already before this House. So, any adjournment to be done is to the next sitting which you have ably clarified is tomorrow morning.
view
10 Dec 2008 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu. (a) Wizara yangu, kupitia shirika la National Water Conservation and Pipeline Corporation (NWCPC), imekuwa ikichukua hatua za kurekebisha mabwawa yaliyozibwa na mchanga Wilayani Samburu. Kutoka mwaka 2005, mabwawa 12 yamerekebishwa, na katika mwaka huu wa Kiserikali mabwawa tisa yatarekebishwa. Pia kuna mpango wa kujenga mabwawa 12 kupitia shirika la Ewaso Nyiro North Development Authority. (b) Wizara yangu itachimba visima vitatu katika eneo la Samburu Mashariki na Samburu Magharibi mwaka huu wa Kiserikali. Visima vingine vinne vinaendelea kuchimbwa Wilayani Samburu Kazikazini. Kazi hii inafanywa kwa kutumia fedha kutoka shirika la Water Services Trust Fund.
view
10 Dec 2008 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, ukweli wa mambo ni kuwa visima vimechimbwa. Lakini ni kweli pia kuwa havitoshi na si eneo la Samburu peke yake linalohitaji visima, bali ni Kenya nzima. Tunajitahidi lakini hatuna pesa za kutosha. Tutakavyoendelea kupata pesa kutoka kwa Serikali ndivyo tutakavyoendelea kuchimba visima. Ikiwa Mbunge ana tashwishi kwamba tunasema tumechimba visima lakini havionekani kule mashinani, basi tungependa kujua, ili tuchunguze na tutatue hilo jambo.
view
10 Dec 2008 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, sijui kama nitapata nafasi ya kusoma majina ya visima vyote, lakini nina majina 14 na niwaweza kumpa ajionee. Kwa mfano, kuna Metumi Dam, Naireri Dam na Laitasin Dam. Pia kuna visima tisa ambavyo tunahitaji kuchimba, na tunaendelea kuchimba vitatu wakati huu. Nitaomba ruhusa yako nimwonyeshe hayo majina, maanake yuko ndani ya Bunge. Tukimaliza hili Swali, nitakwenda kumwonyesha majina yote, na kama ana wasiwasi yoyote, tunaendelea kumtatulia shida zake.
view
10 Dec 2008 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, inategemea Kiswahili cha Mbunge. Hata katika Kiingereza, tunaadhiriwa na lugha zetu na tuna shida za matamshi. Hilo jambo halijawahi kinishtua wakati wowote, na hata katika siasa yangu, halijawahi kunizuia kwenda popote. Kwa hivyo, hiyo ni shida yake kwa sababu niko sawa.
view
10 Dec 2008 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, ni rekodi kuchimba mabwawa saba katika wilaya tatu, kwa sababu sehemu nyingi nchini hazijapata hata bwawa moja. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hayajatosha. Tunakubaliana hivyo, lakini kulingana na tulivyogawa nchi, mabwawa tuliyoweka kule ni mengi. Ikiwa kuna bwawa lolote ambalo limeharibika, na kwa miezi mitatu watu hawajapata maji, hilo jambo halikubaliki, na nitamuuliza Mbunge aniletee hilo jina, tujue ni sehemu gani ili lirekebishwe mara moja.
view
10 Dec 2008 in National Assembly:
Bi. Naibu Spika wa Muda, tutaendelea kurekebisha na ukarabati utaendelea. Jambo la muhimu ni kujiuliza ni wapi tutapata fedha zaidi. Tuna hiyo shida na tunaielewa. Pole kwa hayo lakini tutajaribu iwezekanavyo, hata kama ni mwaka ujao, kuwaomba Wabunge kutupitishia pesa za kutosha kujenga na kuendesha miradi ya maji ambayo itawasaidia wananchi.
view
10 Dec 2008 in National Assembly:
Madam Temporary Deputy Speaker, I beg to reply. A total of Kshs15,893,470 has been allocated in the current Financial Year, 2008/2009, for development, operation and maintenance of irrigation and drainage infrastructure within Perkerra Irrigation Scheme. However, the developed infrastructure for this Scheme is not fully exploited due to inadequate water for irrigation, caused by low river discharges, particularly during the dry seasons.
view