Rehema Hassan

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 71.

  • 30 Aug 2018 in National Assembly: Ahsante Bwana Spika. Nimesimama kuiunga mkono Ripoti hii. Bado napinga wazo la kumtoa huyu dada yetu, Ashubwe. Sababu moja ambayo napinga ni kuwa wanadamu kadri tunavyoishi huko nje tuna maadui wengi sana. Hakuna yule ambaye hakutakii mazuri atakaye kuunga mkono. Kwa hivyo, katika wale watu wa Central Organisation of Trade Unions (COTU) ambao walipinga uchaguzi wa huyu mama, pengine wengine ni watu walikosana naye kwa njia moja ama nyingine. Kwa hivyo, mimi sioni kama hiyo ni sababu ambayo inapaswa ichukuliwe kwa uzito kumnyima mama huyu nafasi. Naomba marekebisho yafanyike na mama huyu achukuliwe kuwa mmoja wa Tume hii. Naunga mkono ... view
  • 30 Aug 2018 in National Assembly: Bwana Spika, tafadhali naomba unitetee. view
  • 30 Aug 2018 in National Assembly: Mambo mengine ni yangu mwenyewe. Mambo mengine hata nikisema ni ya undani, ni yangu mwenyewe na ni siri yangu. Lakini ni mtu namjua ako na uzoefu wa kazi, hana shaka kwa kazi ya Serikali na hata kazi zinginezo. view
  • 30 Aug 2018 in National Assembly: Kwa sasa, ni Mkurugenzi Mkuu katika Bandari ya Mombasa. Anatuwakilisha vilivyo bila tashwishi. Kwa hivyo, naona ametosha kuwa katika Tume hii. Naiunga mkono Riporti hii. view
  • 31 Jul 2018 in National Assembly: Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I also stand here to condemn the satanic act taken by that teacher because when somebody takes such an act, that person is not normal. Kenya is a country where there is freedom of worship. What he did was wrong and I condemn it. At the same time, I thank the people of Ijara for not beating him up because I know how rough Muslims can be because of the Quran. We would be talking about a different story today. I pray for them. May God bless the people of Ijara. view
  • 3 May 2018 in National Assembly: Asante Bwana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii. Nasimama kumpa kongole Mheshimwa Rais kwa Hotuba aliyotoa jana. Lakini pia nasikitika kuwa watu wa Tana River, wakati Mheshimiwa Rais alizungumza kuhusu masuala ya barabara katika maendeleo, walitarajia awatajie kuwa barabara ya Tana River, ambayo ilianza kujengwa nikiwa darasa la tatu itajengwa. Miaka 50 tangu tupate Uhuru, hatuna barabara nzuri. Juzi nikitoka Bura nikienda Garissa upande wa Madogo, ilibidi niogelee katika mashimo saba kwa hiyo barabara iliyokatika. Inasikitisha sana. Mheshimiwa Rais ako na mipango mizuri kwa Wakenya lakini baadhi yetu, ufisadi umetufanya hatuhurumiani. Nashukuru waliotoa Hoja ya Fedha za Kusawazisha ... view
  • 3 May 2018 in National Assembly: Namshukuru Mhe. Rais kwa mipango yake yote ambayo ako nayo. Nilikuwa natarajia atatupa pole. Natoa pole kwa watu wa Tana River kwa majanga yaliyowapata. Tumepoteza watu, wanyama, mashamba na hata ardhi zimeeda kwa sababu haya maji yaliyokuja safari hii ni mengi kushida maji ya El Nino . Hata sehemu zile ambazo maji ya El Nino hayakufika, safari hii maji yamefika. Kwa hivyo, watu wetu hawana mahali pakuishi saa hii. Nilitarajia pia tupangiwe angalau fedha za wale ambao wamekumbwa na janga hili la maji ya mvua inayonyesha. Kule kwetu, maji yamefurika lakini hatuna mvua. Sisi, watu wa Tana River, mvua ikinyesha ... view
  • 3 May 2018 in National Assembly: Naomba wale wahusika wa idara ya maji watusaidie. Maji ambayo yametufanya tuumie saa hii Tana River yananyesha kutoka huko juu. Tafadhali tujengewe mabwawa huku katikati ndio maji yasitufikie. Sisi tumeumia. Naomba kama mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Mazingira; tafadhalini, mkipanga, msituache nyuma. Tana River iko Kenya. Sisi tumepata Uhuru kama watu wengine. Isiwe miaka 50 tangu tupate Uhuru, sisi tunalia shida kila siku. view
  • 3 May 2018 in National Assembly: Namshukuru Mhe. Rais kwa sababu hachukii watu wa Tana River. Namuomba Mhe. Rais ahusishe watu wa Tana River katika suala la handshake maana inaonekana huu ni wakati wa kusameheana. Kuna watu waliopigana kabla ya kura za 2013 na baadhi yao wako jela. Wanateseka na ni watu ambao wako na watoto na wake. Tunaiomba tume ya uhusiano ili izungumze na watu ili wasameheane na hata hao vijana wasamehewe. Mhe. Rais, sauti yako ni kubwa na najua ukisema umewasemehe, watatoka jela na washughulikie watu wao. view
  • 3 May 2018 in National Assembly: Asante. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus