All parliamentary appearances
Entries 1 to 10 of 533.
-
5 Dec 2024 in National Assembly:
, (Kinango, PAA): Thank you, Hon. Temporary Speaker. I will summarise. The report is good on paper but on the ground, things are bad. Over 160 families were affected by this dam in 2021. To date, they have not been settled. When will the Hon. Chairman visit the affected persons? He can call for a meeting with the Coast Water Works Development Agency, ministry and affected persons so that they can be given a timeline on when they will be compensated. They want to find a better place to stay. Currently, it is raining and they have not been provided ...
view
-
5 Dec 2024 in National Assembly:
, (Kinango, PAA): This grievance redress committee has been there since 2021. I am requesting the Committee to give an undertaking because nothing has been done. People are suffering. So, the Committee should handle this matter. I will truly appreciate. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
-
27 Apr 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Mswada huu na kuiombea kuwa sheria. Sisi ambao tumetoka eneo kame na mahali ambapo maji ni shida, hatukuwahi kuiona kiliniki. Tuliishi kutumia madawa ya kienyeji. Hivi sasa, wanatekinolojia wanaona kwamba ni vyema kuwa na kituo kama hicho ambacho kinaweza kuleta utafiti na kuboresha mambo kama haya ili yaweze kunawiri. Ningependa kulipongeza suala hilo kwa sababu enzi zile za nyuma, tulikuwa tukitegemea mavi ya ndovu kutibu homa. Yalikuwa yakiwekwa kwenye makaa na tungewekwa karibu na ule moshi. Tulinawiri na tumefika pahali ambapo tumefika. Tumeharibiwa masuala mengi na mzungu aliyetutawala pia kiakili. Imefika mahali ...
view
-
27 Apr 2016 in National Assembly:
binadamu kusema kwamba amejitoa katika minyororo ya wakoloni, lakini ukoloni unaendelea kumsumbua akilini. Katika Vitabu vya Mwenyezi Mungu, Biblia na Quran, tuliwahi kuambiwa kuwa miti mingi ni dawa. Zama zile, tulipokumbana na nyoka, hatukupelekwa hospitalini kwa sababu nyoka angesemewa na kusikia na sumu ingesimama mahali ilipokuwa. Uwezo huo ulikuweko na labda utafiti wa kuboresha hali hiyo unakosekana. Naunga mkono kwamba kituo hicho kitakapoanzishwa, kipewe pesa kwa sababu kuna vitu viwili. Tupitishe na kiwe kituo cha kufanya utafiti lakini tukikosa kukipa pesa, itakuwa tumejenga nyumba ambayo haina wanadamu ndani. Naunga mkono na kutia sauti kwa wale wengi ambao walikuwa tayari wameunga ...
view
-
27 Apr 2016 in National Assembly:
Tunaweza kufanya utafiti wa miti, mbegu na miche yetu, na kujua ni ipi yenye faida na yenye haina faida. Tunaweza kutilia maanani yaliyo na nguvu. Hapo awali, hatukuwa tunaenda hospitali tukipata maradhi kama msukumo wa damu. Tulikuwa tunatumia mbegu na madawa ya kienyeji, na tulikuwa tukipona. Lakini, kutokana na haya makubwa tuliyoletewa na mkoloni, hata mtoto mchanga anaugua saratani kwa sababu ya mafuta tunayotumia. Tunaambiwa kwamba kuna madawa ambayo yanaweza kuregesha saratani chini. Lakini kinachohitajika ni kuboresha mimea ama dawa ili kuhakikisha kwamba tunapata lishe bora.
view
-
27 Apr 2016 in National Assembly:
Mswada huu unahitaji kuboreshwa katika Kamati ya Bunge nzima ili kuhakikisha kwamba umeweza kuyalenga yale yote ambayo yanaweza kumnufaisha mwanadamu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba kuunga mkono.
view
-
23 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaomba kuchukua nafasi hii kukushukuru na kumshukuru aliyeleta Hoja hii. Ni wakati mwafaka kwa sababu baada ya miaka 50 tangu tupate Uhuru, itakuwa ni jambo bora kama tungeanza kuangazia masuala ya afya kuwa muhimu sana katika maisha ya jamii. Kadri tunavyoendelea kumuunga mkono Mhe. Wanga kwa sababu ya Hoja hii, lingekuwa pia wazo bora kama pengine baada ya haya yote ya kuwatuma wataalam kwenda kusomea na kuja kuleta mwelekeo bora, ingekuwa bora kujua baadhi ya wataalam fulani kielimu ili kuhakikisha kwamba masuala ya elimu katika jamii yameaangaziwa. Hii ni kwa sababu punde saratani inapomkumba mwanadamu, ...
view
-
23 Mar 2016 in National Assembly:
ya kupitisha Hoja hii, kuifuatilia kwa karibu sana ili kuona kwamba matokeo yake yamesaidia jamii ya Wakenya na kuleta afueni katika maisha ya mwanadamu. Kimekuwa kitu cha kawaida, pengine tumwuulize Mhe. Wanga ilimchukua muda gani kufikiria suala hili na hasa baada ya suala kumalizika pengine aangazie pia kufanya utafiti. Hii “saratani” ya ufisadi ataweza kuitumia tiba gani ama kuiletea Hoja gani kwa sababu pasipo sisi kupata suluhisho la kudumu--- Mara nyingi suala linaloulizwa ni kwamba wakati tunapohitaji msaada wa aina yoyote, huambiwa kwamba Serikali haina pesa. Lakini haijapata jibu la wale watu wanaopoteza pesa za Umma kwa sababu anayekula pesa ...
view
-
10 Jan 2013 in National Assembly:
Nashukuru, Bw. Naibu wa Spika, kwa kupata nafasi hii ili niweze kuwashukuru watu wa Kinango kwa kuniweka katika Bunge hili sasa nikitimiza miaka 15. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu, nikisema asante kwa yale ambayo niliweza kuyafanya kwa kipindi hicho. Ni imani yangu kwamba niliyafanya kwa uwezo wake Mola. Tunapokwenda kufanya sasa, maombi yangu ni kwamba Wakenya waiombee nchi hii kwa sababu uchaguzi unafuata si wa kawaida; na kwamba yale yatakayoipata umma tarehe 4.3.2023 tumeze kuyapokea kwa mikono miwili tukiwa na imani kwamba yote yatakuwa kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. Sisi kazi yetu ni kuomba. Analoitikia Mwenyezi Mungu ndilo litakalo kuwa. Kwa hivyo ...
view
-
9 Jan 2013 in National Assembly:
Mr. Deputy Speaker, Sir, I beg to reply. (a) It is true that PDP No. N9/84/18 of 14th August 1984 was approved in favour of Kisumu Union Primary School, Kisumu Municipality. (b) Title for Kisumu Municipality/Block 9/169 in favour of St. Alloys Obby Annam, doing business in the names of Annat Technical Services was issued based on the PDP No. N9/95/6 of 8th February 1995.
view