8 Nov 2017 in National Assembly:
kuhusisha wale watu ambao wako kule mashinani kama vile wale walioongea mbele yangu wamesema. Ni vizuri wale matajiri wanapotajirika, nalo eneo lile limefanya watajirike, litajirike. Lakini ukitafuta usawa wa pahali madini yametoka na pahali yanaenda kuendeleza, hakuna uhusiano kamwe. Ombi la watu wote wale wako maeneo ya madini haya ni kuwa ni vizuri wahusishwe kabla hata madini hayajaanza kuchimbwa. Tukifanya hivyo, Kenya yetu itakuwa ya kuheshimika. Itakuwa katika mrengo wa mbele wa dunia pahali madini yamekuwa ya kuleta utajiri lakini si umasikini na vita. Ninaunga mkono Hoja hii.
view
11 Oct 2017 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Mwenyekiti. Kusema kweli, tuko hapa kuhusisha wakenya wote. Kama kuna jambo lolote la kutenga wengine, basi hatutendei Wakenya haki. Kwa hivyo, ni vyema kufanya mambo haya yote kwa uwazi na tuandike maandiko yatakayosomwa na wote kwa sababu hakuna Mkenya nusu; Wakenya wote tuko sawa na tunastahili kuheshimika sawa.
view
11 Oct 2017 in National Assembly:
Naunga mkono.
view
14 Sep 2017 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika. Mimi ninatoka Eneo Bunge la Ruiru katika Kaunti ya Kiambu. Eneo hili ni moja kati ya maeneo Bunge makubwa humu nchini na lina idadi ya watu 160,000. Ningependa kuwashukuru watu wa Ruiru ambao walinichagua na kunipigia kura zaidi ya 108,000. Nawapa shukrani kubwa watu wa Ruiru kwa kunipatia fursa hii ya kuwawakilisha hapa Bungeni. Sitasahau kurudisha shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutupatia ujasiri wa kuchagua Spika Mhe. Muturi na Naibu Spika. Mlihudumia Bunge muhula uliopita na tukaona ujasiri wenu na vilevile tukawachagua. Kwa sisi Wabunge, ni shukrani kwa wananchi wa Kenya kutupatia mwanya wa kuwawakilisha. ...
view
14 Sep 2017 in National Assembly:
kusoma wakati tunaendeleza maendeleo yetu. La muhimu, alisema hata kama kuna vurugu na joto kali la kisiasa, atasimama kidete kuona sisi viongozu tumetimiza majukumu yetu bila wasiwasi wowote ule. Na kama kiongozi wetu amesema hakuna wasiwasi, sisi ni akina nani kuwa na wasiwasi? Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kama kiongozi wetu hana wasiwasi. Sisi tuko wengi.Yeye ako peke yake na amesimama na uzito wa kuonyesha Kenya itakuwa na amani hata kama vipande vingine vimekaa vile wamekaa. La muhimu ni kuhimiza wote ambao wamechaguliwa kuja Bungeni ili tutimize yale ambayo tulichaguliwa kutimiza. Ni aibu kidogo wakati mtu ambaye amechaguliwa anakuja ...
view