9 Apr 2025 in Senate:
Asante, Bw, Spika wa Muda. Kiwanja hiki cha ndege cha Isiolo kina wale mahandisi na maafisa husika ambao waliweza kutayarisha ripoti juu yake. Tukiangalia, kwanza, hawa wataalam waliweza kutayarisha ripoti yao na kusema kwamba hiki kiwanja kitakuwa tayari ikiwa kitatumia shilingi 1.5 bilioni. Bw. Waziri, ningependa kujua majina ya hawa mahandisi ambao waliweza kutengeneza kiwanja hiki cha ndege na wakaangalia na kusema watatumia shilingi 1.5 bilioni. Mahandisi waliyofanya kazi hii wawekwe wazi hapa pamoja na wahusika wowote waliokuwa na uwezo wa kutengeza kiwanja hicho. Swala langu la pili ni ikiwa hivi sasa imeonekana ya kwamba chini ya hii ardhi haiwezi ...
view
9 Apr 2025 in Senate:
wameadhibiwa? Swala la tatu ni Bw. Waziri atueleze wao mahandisi walisomea wapi uhandisi wao?
view
9 Apr 2025 in Senate:
La mwisho, Bw. Spika wa Muda---
view
9 Apr 2025 in Senate:
Swali langu la mwisho ambalo ningetaka kumuuliza Bw. Waziri- --
view
9 Apr 2025 in Senate:
Ndio Swali ni moja lakini, pole, ningetaka kuongezea. Ni hatua gani ambayo inaweza kuchukuliwa kuona ya kwamba athiri kama hii haitatokea na hawa mainjinia wanatakikana kumsaida Mhe. Rais ili aonekane akisema kitu kitafanyika, kifanyike. Hawa ndio wafisadi kwa sababu wanataka kurudi tena watengeneze pesa, ilhali, pesa ambayo ilikuwa allocated kwa airport hiyo ni zile ambazo walizitumia na sasa wamezweka mara mbili, kutoka shilingi 1.5 bilioni. Sasa wanasema ya kwamba wanaweza kumaliza kiwanja hicho ikiwa watatumia shilingi bilioni nne. Kwa hivyo, ni hatua gani ambayo Waziri amechukua kuona ya kwamba hawa wahandisi waliofanya hii kazi wamechukuliwa hatua?
view
8 Apr 2025 in Senate:
Thank you, Madam Temporary Speaker. It is not dirty. I just wanted to say that it might not appear to be clean, but that word ‘dirty’ does not exist legally. He can use another language.
view
3 Apr 2025 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Hukuwa umeniita lakini nimechukuwa nafasi hii kwa sababu ulikuwa unaongea na dadangu, nikasema ni sawa, nitatendelea.
view
3 Apr 2025 in Senate:
Bw. Spika, kawaida lazima umtaje mtu jina kama ilivyo kawaida.
view
3 Apr 2025 in Senate:
Bw. Spika, kwanza nataka kuunga mkono hii Hoja ya kuongeza muda kwa ile jopo linalofanya interview kuchagua wale wenzetu ama watu ambao watakuwa makamishina. Jopo hili lina kazi nyingi sana kwa sababu lilikuwa limepewa muda kulingana na Katiba. Hata hivyo, ule muda unaonekana umeyoyoma sana na bado wale watu wanafanyiwa interview wanaendelea kuja. Muda ukifiki hawatakuwa wamekamilisha na ndiyo sababu wameomba muda, waongezewa siku 14. Sababu walizosema ni kuwa hawakutarajia kitendo kama hiki kitaweza kutendeka. Walitumaini watamaliza ili Wakenya wapate tume itakayosimamia mambo ya uchaguzi katika nchi yetu ya Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for ...
view