All parliamentary appearances
Entries 1591 to 1600 of 1714.
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. Is it in order for the hon. Member to introduce irrelevant things about who was been in KANU, including the President, yet he and his father were life members of KANU?
view
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuzungumza juu ya jambo hili ambalo ni muhimu sana. Mtu yeyote ambaye ana fikira timamu atakubaliana nami ya kwamba walimu wana haki ya kuuliza nyongeza ya mshahara kwa sababu kila mfanyakazi pamoja nasi, ingawa mara nyingi tunapigwa, hatuwezi kukataa kuongezwa pesa.
view
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
Serikali haikukataa kuwapatia walimu nyongeza. Walijadiliana na wakakubaliana. Shida iliyoko ni kwamba Serikali inasema: "Kwa wakati huu, hatuna pesa za kutosha. Tumekubaliana na nyinyi. Tuko tayari kuwapatia nyongeza hiyo lakini tutafanya mipango ya kuwalipa kwa muda."
view
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, sisi ni viongozi katika nchi hii na tumepewa mamlaka ya kuangalia nchi nzima kwa jumla. Ni vizuri tufikirie sana jambo hili kwa sababu walimu ndio wafanyakazi pekee ambao wako zaidi ya 250,000. Kama watalipwa nyongeza hiyo mara moja, wakati tunajua ya kwamba hata Bajeti yetu ambayo tunasema tutapata kwa sababu ya shida zilizotoka kwa sababu ya uchaguzi, huenda tusipate pesa hizo.
view
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
Tunasoma kwa gazeti na kuona kwa televisheni vile watu wengi wanateseka kwa sababu ya njaa. Wakati mwingine unaona kuwa ni dhambi kubwa sana kula chakula. Ni lazima walimu watafakari sana kwa sababu haina faida yoyote kwao na kwa nchi pia kudhalilisha watoto ambao hawana dhambi na wanataka kusoma. Wanaweza kuendelea kufunza na pia watafute haki yao vile inavyopaswa. Adhuhuri ya leo, Kaimu Waziri wa Fedha aliomba Bunge hili lipatie Serikali hii ruhusa ya kukopa Kshs7 bilioni. Makosa mawili hayafanyi moja kuwa sawa. Makosa ni makosa. Kama kweli kuna tuhuma ya kwamba mahindi yanatumiwa kwa njia mbaya, yameibwa na hii ni ...
view
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
Pia, ni makosa ikiwa tutainyima Serikali kibali cha kuomba pesa za kununua chakula na kulisha watu wetu ambao wana njaa wakati huu. Tukikataa hiyo, tunafanya makosa kwa binadamu. Mtu mmoja akifa leo kwa sababu Bunge hili limetukataza kuomba pesa, nafikiri ni vizuri mtu akiiba pesa ashtakiwe na tumfuate tukiwa pamoja.
view
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
Ni vizuri tuangalie hadhi na heshima ya Bunge hili. Bunge hili ni Jumba la wazee ambalo linatakiwa kutatua matatizo ya nchi hii. Kama kuna watoto wako wawili wanapigana kama vile Wizara ya Elimu na walimu, ni vibaya Wabunge kuenda kufanya mkutano wa wanahabari na walimu wakipeleka mambo yao dhahiri mbele ya umma. Itakuwa vibaya na ni kuvunja heshima ya Bunge hili. Kama mtu yeyote anataka kupinga ama kukubali kitu chochote, nidhamu ni kwamba tuje katika Bunge hili na tuzungumze yale ambayo tunataka kuzungumza.
view
-
21 Jan 2009 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninapinga Hoja hii. Asante sana.
view
-
20 Jan 2009 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I beg to reply
view
-
20 Jan 2009 in National Assembly:
(a) Archers Post Military Training area, which is in Ewaso Nyiro Division of Samburu East District, was gazetted on 31st October, 1977, as a military training area by the Commissioner of Lands. That is vide Gazette Notice No.3210 dated 31st October, 1977. The area involved is about 83,327 acres.
view