5 Jun 2018 in National Assembly:
Members of this Parliament can also lead by example in fighting against corruption and the culture of impunity. When a person is arrested for corrupt practices or removed from office for corrupt reasons, we should not stand with that person because he is one of us or he is a member of our tribe or ethnic group. We should let the law take its course in the fight against corruption and impunity. We can also teach the public the need to fight impunity. Finally, we need to have social justice, equity, affordable housing and clean water. We should make sure ...
view
5 Jun 2018 in National Assembly:
Thank you so much, I support the President’s Address.
view
5 Jun 2018 in National Assembly:
Thank you so much, I support the President’s Address.
view
13 Sep 2017 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika. Kwanza, nachukua fursa hii kuwapongeza Wabunge wote ambao wamechaguliwa na wananchi. Nataka kusema kwamba Bunge ni nguzo muhimu katika uongozi wa nchi yetu. Lazima tushikilie hiyo kwa nguvu na tuhakikishe kwamba tunawakilisha umma.
view
13 Sep 2017 in National Assembly:
Hon. Speaker: Order, Members. Those who are withdrawing for whatever purposes, you still must observe decorum. I just reminded you that we are not in the outfit called Bunge laMwananchi . This is the National Assembly of the Republic of Kenya.
view
13 Sep 2017 in National Assembly:
Proceed, Hon. Hassan.
view
13 Sep 2017 in National Assembly:
Mhe. Spika, nataka kuwapongeza Waheshimiwa waliochaguliwa na umma na kutupatia fursa ya kuwakilisha Kenya katika Bunge hili la 12. Nikiongezea sauti yangu kwa wale wengine, tuendelee na kazi zetu. Tumechaguliwa kama Wabunge. Tuwaachie hawa wakereketo wakubwa wakongwe waendelee na mambo yao huko Kibera na Kamukunji Grounds. Kazi yetu iwe kutimiza wajibu wa kutunga sheria, kuwakilisha wananchi wetu katika Bunge hili na tutimize kazi yetu kama tulivyoletwa hapa na wananchi.
view
13 Sep 2017 in National Assembly:
Ninajua ya kwamba watu wengi watauliza suala la demokrasia. Maana ya demokrasia ni kwamba unawakilisha wananchi wa Kenya, na umechaguliwa kihalali katika Bunge hili. Sisi wote tumechaguliwa. Sasa kazi ambayo wananchi wa Kenya wanataka ni kutimiza wajibu wetu. Kesho utakaporudi katika eneo la Bunge ulilochaguliwa, hawatakuuliza kama ulisimama Kibera ama Kamukunji Grounds ukazungumza. Watakuuliza umefanya nini, umetunga sheria gani na umefanya kazi gani katika Bunge kuajibika kuchaguliwa tena.
view
13 Sep 2017 in National Assembly:
Mkumbuke kwamba, demokrasia tuliyonayo tumeipigania kwa miaka mingi. Wengi wetu tumekuwa uhamishoni, wengine wamekwenda jela na wengine wamefariki ili tupate haki ya kupata kuwakilisha sawa sawa wananchi wa Kenya. Kwa hivyo, lazima tushikilie na tupiganie hiyo haki, tuindeleze mbele na tuhakikishe kwamba tunatumia Bunge kubadilisha mambo tunayotaka kuyabadilisha, tutengeneze mambo yanayohitajika kutengenezwa, tutunge sheria za haki na tuendeleze nchi yetu pamoja.
view
13 Sep 2017 in National Assembly:
Nawasihi ndugu zetu wa Upinzani wasione kwamba Kenya ni ya vyama na mikoa. Kenya ni nchi moja na tunahitaji kuwa pamoja tushikane pamoja tuipeleke mbele. Mnapoenda kutafuta mzozano, mnaumiza uchumi wa nchi yetu. Mkienda kuzozana, mnaumiza umoja wa nchi yetu. Tupeleke Kenya yetu mbele na tujenge nchi yetu pamoja. Ikiwa mnataka kugeuza mambo, tuje hapa pamoja tuyageuze kidemokrasia na sio huko nje ambayo ni extra-parliamentary activities . Wawachie hao makereketo wakongwe wafanye hiyo kazi. Hawako Bungeni kwa sababu hawakuchaguliwa. Wao wakae huko na sisi tufanye kazi yetu tuendelee na hoja yetu na tuchague viongozi watakaoendesha kazi za Bunge, ili iendelee ...
view