Hon Members, we do not have the requisite numbers. I order that the Quorum Bell be rung for five minutes.
Order, Hon. Members! When the Quorum Bell is being rung, you should not walk out of the Chamber. I want to ask those Members who are walking out to please adhere to the Standing Orders.
Hon. Members, I can confirm that we now have the numbers to start the session.
Mheshimiwa wa Kamukunji, Mhe. Yussuf Hassan.
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nafurahi sana kwamba hii leo tumekianza kikao hiki cha Bunge kwa lugha yetu tamu ya mama ya Kiswahili. Arifa ya Hoja yangu ya leo inahusiana na kushughulikia utaratibu wa Kiswahili na ukuzaji wa Kiswahili.
Hoja yako ya nidhamu ni gani, Mhe. Opiyo Wandayi?
Mhe. Spika wa Muda, mambo anayozungumzia Mhe. Yusuf ni ya muhimu sana. Hii ni Hoja inayotuhitaji sisi sote tufuatilie kwa makini. Ninakuomba umruhusu Mhe. Yusuf Hassan aje karibu ili sisi sote tumfuate kwa makini na tumuone kinaga ubaga.
Naam, vile Mhe. Pkosing anavyosema, hii ni kwa sababu mambo ya Kiswahili ni magumu kidogo kwa wengi wetu; na tungependa nasi tupate nafasi ili tujifunze lugha ya Kiswahili.
Asante Mhe. Opiyo Wandayi. Nakubaliana nawe. Kanuni za Kudumu za Bunge zipo katika lugha ya Kiswahili. Natumahi Mhe. Yusuf huna shida kusonga mbele ili Wabunge na watu wote wakuone vizuri ili wajifunze kutoka
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
kwako. Wanaweza fanya hivyo kwa kuchukua makaratasi ili waweze kuandika maandishi madogo madogo ili wasomeshwe. Karibia, Mhe. Yusuf. Mhe. Wangwe, kwenye Hoja ya kufahamisha, unayetaka kumfahamisha ni lazima awe anaongea. Kwa sasa, Mhe. Yusuf ndiye ako na usukani. Mhe. Hassan, endelea tafadhali.
Asante Mhe. Spika wa Muda. Nakushukuru kwa kupata fursa hii ya kuweza kuleta Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya kwenya Kamati ya Idara ya Michezo, Utamaduni na Utalii. Tukitambua kifungo cha 7…
Subiri kidogo, Mhe. Yusuf. Hoja yako ya nidhamu, Mhe. Makali Mulu ni ipi?
Asante sana Mhe. Spika wa Muda. Niko na heshima kuu kwa Mhe. anayezungumza kwa sasa. Hili jambo la kusema asonge mbele kule linanitatiza. Naamini kuwa Ukumbi huu unatukubalisha tuongee tukiwa upande wowote. Sielewi lengo la Kiongozi wa Chama cha walio Wachache ni nini. Inamaanisha pia nasi tutakuwa tunakaa pale mbele? Mimi ni backbencher, na ninaona ugumu kuongea pale mbele. Ningependa uturuhusu tuongee mahali popote katika Ukumbi huu.
Mhe. Makali Mulu, hilo lilikua ombi la Kiongozi wa Chama cha walio Wachache kwenye Bunge. Kwa fikira yangu, nadhani anataka kufuata matamshi na kuangalia jinsi mdomo wa Mhe. Yusuf unavyotamka maneno katika lugha ya Kiswahili. Nakubaliana nawewe kwamba unaeza zungumza mahali ulipo. Endelea Mhe. Yusuf.
Mhe. Spika wa Muda, mbele ya kikao hiki cha Bunge, napendekeza Hoja ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya ambayo itapelekwa kwa Kamati ya Idara ya Michezo, Utamaduni na Utalii: KWAMBA, tukitambua Kifungu cha 7 cha Katiba ya Kenya kinabainisha Kiswahili kuwa lugha pekee ya kitaifa, na pia lugha rasmi pamoja na Kiingereza, na aidha kwamba Serikali ina wajibu wa kulinda, kuendeleza na kukuza matumizi ya lugha za kiasili za watu wa Kenya; KUWA Vifungu vya 119 na 137 vya Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vinawajibisha dola za Afrika Mashariki kustawisha na kuendeleza Kiswahili kama lugha ya mshikamano wa nchi wanachama; KWAMBA Mkutano wa 21 wa Marais wa nchi za Afrika Mashariki uliridhia Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwajibisha Tume ya Kiswahili Afrika Mashariki (EastAfrican Kiswahili Commission) kuwezesha kukoleza matumizi ya Kiswahili katika kanda hii; na KWAMBA Kiswahili ni moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika, na kwamba Umoja wa Mataifa kupitia UNESCO umetenga kila Julai 7 kuwa Siku ya Kiswahili duniani; TUKIFAHAMU nchi ya Tanzania iliunda Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) mwaka wa 1967 na Zanzibar ikaanzisha Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) mwaka wa 2004 kwa madhumuni ya kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili eneo la Tanzania bara pamoja visiwa vya Zanzibar; IKIFAHAMIKA Kiswahili ni lugha asili kwa jamii za Mkoa wa Pwani nchini Kenya na pia Wakenya wengi ni wazungumzaji wa Kiswahili; TUKIJUA lugha ya Kiingereza ina nguvu sana katika mawasiliano rasmi na hivyo kuchangia kudhoofika kwa lugha yetu ya Kiswahili; TUKITAMBUA uamuzi wa mkutano wa tatu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya uliofanyika tarehe 14 Agosti 2018 ulioidhinisha kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya kulingana na
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Kifungu cha 137 cha Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki haujatekelezwa; BUNGE hili linahimiza Serikali Kuu kupitia Wizara ya Michezo, Utamaduni na Mirathi, kwa ushirikiano na vyombo vya kitaifa na vya kibinafsi vinavyohusika na uboreshaji wa lugha ya Kiswahili kuanzisha rasmi Baraza la Kiswahili la Kenya na kuzindua mikakati, mbinu na sera mahususi zinazohitajika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili.
Subiri, Mhe. Yusuf. Mhe. Mpuru Aburi wa Tigania Mashariki, Hoja yako ya nidhamu ni gani?
Asante, Mhe. Spika wa Muda. Naona ndugu yangu pale akiendelea kusoma Hoja yake, ilhali ningependa atueleze katika lugha ya Kiswahili bila kusoma. Asante.
Mhe. Yusuf, uko sawa. Unakubaliwa kusoma maandishi ambayo umenakili unapo anzisha mjadala wa Hoja yako.
Ningependa kuelezea umuhimu wa lugha hii. Lugha ya Kiswahili ni muhimu nchini, katika Afrika Mashariki, Afrika na Ulimwengu wote. Ni lugha yetu ya mama na ya kiasili tunayojivunia; sio lugha ya kigeni, ya mkoloni au ya mbeberu, bali ni lugha yetu ya kitaifa, ya kitamaduni ya Kenya na Mwafrika. Lugha hii inazungumzwa na Wakenya wengi zaidi kuliko lugha yoyote ile. Asilimia themanini na tano ya Wakenya, ambao ni watu karibu milioni arubaini na mbili, wanazungumza lugha hii. Mbunge anapokuwa katika pilka pilka za uchaguzi, na hata alipokuwa akitafuta kura kwa wananchi, hakuwa anazungumza lugha anayoitumia hapa Ukumbini ya kibeberu na ya kikoloni. Alikuwa anatumia lugha ambayo mama mboga na watu wa kawaida wanazungumza – lugha tunayo jivunia na ambayo ina umuhimu duniani – Kiswahili. Kiswahili kinatambuliwa na kuzungumuzwa katika Afrika Mashariki katika nchi kama vile Tanzania, Uganda, Msumbiji, Somalia, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Zambia, visiwa vya Komoros na Ushelisheli. Unapotembea katika nchi hizi, hautahitaji kutafuta mkalimani. Duniani na pia Marekani, zaidi ya watu laki moja wanazungumza lugha ya Kiswahili. Hivi majuzi, tulienda Uchina kwa matembezi kama wabunge, na tulishangazwa sana na Wachina wenye vyeo vikubwa katika Serikali vile walivyozungumza Kiswahili. Mabalozi wengi wanaotumwa katika nchi yetu… Sasa hivi ukizungumza na Balozi wa Japani, Uingereza na Ujerumani, utakuta kwamba ni wazungumzaji wa Kiswahili. Kwa hivyo, hii ni lugha ya kidiplomasia, utamaduni, sayansi; na ni lugha inatumika katika sehemu mbalimbali duniani. Hii ni lugha ambayo tunahitaji kuikuza na kuiendeleza. Ni lugha ya kipekee ya Kiafrika ambayo inazungumzwa kwa wingi zaidi duniani. Kuna watu 200,000,000 ambao wanaizungumza, na inatambuliwa kama lugha rasmi ya Umoja wa Mataifa, nchi za Afrika Mashariki na Afrika Kusini. Sasa hivi, Kiswahili kimeanza kufundishwa katika zaidi ya vyuo elfu mbili mbalimbali duniani, kwa mfano Havard na Oxford, ambapo watu wanafundishwa Kiswahili kama lugha muhimu duniani. Kiswahili kinatangazwa katika redio na televisheni mbalimbali duniani kama British Broadcasting Corporation (BBC), Voice of America (VOA), vituo vya redio vya Urusi, Uchina na India.
Kiswahili kimechangia pakubwa katika ukombozi wa uhuru wa Mwafrika, uhuru wa kisiasa pia katika harakati za mapambano ya uhuru wa fikira na utamaduni; na pia mentaldecolonization, yaani ukombozi wa akili. Huwezi ukapata maendeleo ama kumfundisha mtoto wako na apate akili ya kimaendeleo ikiwa anatumia lugha ya kigeni ya wabeberu. Ukitazama nchi zilizoendelea duniani, zinatumia lugha za kiasili; kwa mfano India, Uchina, Vietnam na
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Japan. Hakuna nchi iliyojiendeleza kwa kutumia lugha ya kibeberu. Kwa hivyo, Kiswahili ni lugha ya ukombozi, haswa ukombozi wa kifikira, na kitatupeleka mbele. Pia, Kiswahili kimetumika katika mapambano ya kuondoa ubeberu na ukoloni mamboleo katika maisha na hali ya kila siku ya Mkenya na Mwafrika. Hili lilifanyika ili tuweze kupata uhuru kamili wa kifikira na kuzatiti mila, utamaduni na fikira zetu za kiasili za Kiafrika. Tunahitaji kukuza Kiswahili kama msingi wa maendeleo yetu ya kibinadamu. Tukifanya hivyo, tutatambuliwa, tutaheshimiwa, kutukuzwa na kuwa na utu kamili katika dunia hii, ikiwa tutakuwa na fahari ya kuendeleza na kutumia lugha yetu. Mwisho, Kiswahili kinatumika kuleta umoja, ushirikiano, mashikamano na undugu katika Nchi ya Kenya. Sisi ni watu wa makabila mbalimbali hapa Kenya, lakini jambo moja ni kwamba ukienda Turkana, Kwale, Moyale ama Marsabit na kwote ulipo, Kiswahili kinatuunganisha, na ni lugha ya umoja na maendeleo. Badala ya kusambaratika kupitia tofauti za kikabila, Kiswahili ni daraja inayo tuunganisha na tunasafiri pamoja kama Wakenya. Kenya itakuwa na nguvu zaidi ikiwa tutazatiti na kulinda lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha yetu ya kiasili. Ningependa kuwaomba Wabunge wenzangu kuwa tubuni Baraza la Kiswahili ambalo litazindua sheria, mipango na utaratibu wa kuendeleza Kiswahili. Baraza hili litakuza, litaimarisha na kujenga lugha yetu muhimu ya Kiswahili. Tuwe na fahari, uwezo na tujikomboe kiakili na kifikira; na pia tuzatiti lugha hii katika sheria, maendeleo na maisha ya Wakenya. Baraza la Kiswahili litachangia na kusaidia katika kukuza Kiswahili na Afrika. Itaimarisha umoja wa Afrika Mashariki na Afrika kuu katika mapambano ya lugha na maendeleo duniani. Kwa hivyo, nawashukuru na ningependa tuunge mkono kwa kubuniwa Baraza ka Kiswahili la kitaifa. Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa fursa hii.
Mhe. Yusuf, kwanza tafadhali lazima upendekeze, kwa hivyo lazima umaliza kwa kusema kwamba ungetaka kupendekeza, halafu umuombe ambaye atakuafikia.
Nashukuru Mhe. Spika wa Muda kwa kunielekeza. Naomba kupendekeza Hoja hii, na ningependa kuomba watu wawili, wakiwa Mhe. Korere na ndugu yangu, Mhe. Mohammed Ali wa Nyali.
Mhe. Hassan, hiyo nafahamu itaenda kinyume na kanuni zetu za Bunge hili. Lazima uwe na mmoja wa kuafiki.
Mhe. Sarah Korere ndiye aliye hapa.
Mhe. Sarah Korere wa Laikipia Kaskazini
Shukrani, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuafiki Hoja hii na kumpongeza Mhe. Kaka Yusuf kwa kuwakilisha Bungeni Hoja ya kutaka Bunge hili kupendekeza kuundwa kwa Baraza la Kiswahili katika nchi yetu tukufu ya Kenya. Ukitazama Sura ya pili, kifungu cha saba moja katika Katiba ya nchi yetu, kinasema kwamba lugha ya Kiswahili ni lugha ya Kitaifa. Pili, Katiba inaendelea kusema kwamba Kiswahili na Kingereza ni lugha rasmi. Kwa hivyo, kwanza ni jambo la busara kutilia maanani lugha yetu ya kitaifa ambayo ni Kiswahili; kisha lugha rasmi ambayo ni Kiswahili na Kingereza. Nilitazama wakati Wabunge wa Kaunti wakiapishwa, na nikaona dada mmoja ambaye katika mitandao ya kijamii, aliweza kukejeliwa na kudhihakiwa sana kwa sababu ya kushindwa kuchukua kiapo kwa lugha ya Kimombo. Inatakiwa ifahamike kwamba huwezi pima akili, busara na hekima ya mtu kupitia lugha ya Kimombo. Nilipokuwa natazama kanda ile, nilijiuliza swali. Iwapo Mfalme William angeapishwa kwa lugha ya Kiswahili, je dhihaka na kejeli zingekuwa kama zile tulizoshuhudia yule mwanadada akidhihakiwa? Ningeomba Wabunge wenzangu na taifa letu la Kenya kwamba lazima tukikuze Kiswahili, na tuwe na fahari yetu, ambayo ni Kiswahili.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Leo ukienda Uingereza, Waingereza wanazaa kwao Uingereza wanakuza na kuwafunza watoto wao Kiingereza, na sisi twataka kupima hekima zetu kulingana na lugha ambayo si yetu. Ukienda Ufaransa, ni vile vile. Wanafunzi wetu wanapoenda kusoma Ujerumani, sharti kwanza wasome lugha ya Kijerumani ili waweze kufunzwa kwa Kijerumani. Kwa hivyo, litakuwa jambo la busara sana kama sisi Wakenya na wanajumuia wa Afrika Mashariki kuweza kujivunia na kukikuza Kiswahili kama fahari yetu. Hii ni muhimu ili wengine wanapokuja kusoma katika Bara la Afrika na haswa katika Kanda ya Afrika Mashariki, sharti waweze kujifunza lugha yetu ya Kiswahili. Wakenya wengi, haswa wale ambao labda hawajasoma vile, ama hawana mazoea ya lugha hii ya Kimombo, wameweza kutapeliwa katika biashara ya mashamba kwa sababu ya kutia sahihi katika mambo ambayo hawaelewi. Iwapo mawakili wetu watakuwa na mazoea ya kuandika hata mikataba katika lugha ya Kiswahili, watu wataweza kuelewa vilivyo ni nini wanatia sahihi.
Tukizungumzia mambo ya ukoloni, twajivunia kwamba tumepata uhuru. Lakini, bado kuna ukoloni mamboleo. Akili zetu bado hazijakombolewa. Tunaamini sana mambo ya nje kuliko yale ambayo tuko nayo hapa ndani. Ninatoka Laikipia. Katika miaka hio ya ukoloni, mkoloni aliita mzee mmoja Maasai, akatia sahihi kitu ambacho kiliandikwa kwa lugha ya Kimombo, na ardhi yetu yote ikachukuliwa. Kama huo mkataba ungeandikwa kwa lugha ya Wamaasai, labda huyo mzee hangelipeana ardhi yetu bure. Naomba Wabunge wenzangu, Wakenya wazalendo na wanakanda wa Afrika Mashariki, iwapo tutaimarisha mahusiano yetu, lazima tuwe na lugha ambayo inatushikanisha. Lazima tujikomboe na zile fikira za kikoloni za kufikiria kwamba kuzungumza Kiingereza kingi ndivyo kujua. Hata wale ambao wanazungumza lugha za kiasili, wao bado wanajua. Wabunge wenzangu ambao wameketi hapa watakubaliana nami kwamba ni nadra sana watoto wetu kuzungumza kwa Kiswahili. Mtoto akifika miaka miwili, ameanza kuzungumza kwa Kiingereza. Kiswahili ni nadra; lugha ya mama hamna tena. Kwa hivyo, hii ni Hoja muhimu sana. Naomba Wabunge waiunge mkono ili tuweze kubuni baraza la Kiswahili, tukuze nchi yetu, mahusiano na uhusiano wetu wa Kanda ya Afrika Mashariki.
Naomba nikome hapo. Shukrani.
Ahsante sana Mhe. Sarah Korere.
Nafasi hii nitampa Mbunge wa Kilifi Kaskazini ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Wengi kwenye Bunge, Mhe. Owen Baya.
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nafurahia sana leo kwamba katika Bunge hili mwanzo, tumeanza vizuri na lugha yetu ya Kiswahili. Hoja ambayo tunaizungumzia leo ni kuhusu hii lugha yenyewe. Kwa muda mrefu, taifa la Kenya limeachwa nyuma na mataifa ya Afrika Mashariki katika maneno ya lugha ya Kiswahili. Tanzania imekuwa mstari wa mbele. Pia, Zanzibar imekuwa msitari wa mbele. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akija hapa Kenya, anaongea lugha safi ya Kiswahili ilhali sisi wenyewe bado tunaongea Kiingereza katika mikutano mikubwa kama yeye yuko. Rais Paul Kagame wa Rwanda huongea kwa Kiswahili akija hapa Kenya. Lakini sisi wenyewe katika ile mikutano yuko, tunaongea Kiingereza. Ni muhimu tujue kwamba lugha ya Kiswahili ni unganishi katika Afrika Mashariki. Vile Baraza la Afrika Mashariki linazidi kuongezeka—sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeingia na mataifa mengine yanaingia—ni vizuri tuwe na lugha ambayo inaweza kuunganisha Afrika Mashariki, na lugha hiyo ni Kiswahili. Ni vizuri taifa hili la Kenya libuni Baraza la Kiswahili ili hiki Kiswahili tunachoongea kiwe ambacho kinaeleweka. Hatuna baraza la lugha ya Kiswahili hapa Kenya. Kila wakati Kiswahili kinadhihakiwa. Unasikia mara watu wametoa maneno mapya, mara kinakuwa
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
kombokombo. Hakikuwi katika ile itikadi ya Kiswahili yenyewe. Unasikia kila mtu anaongezea maneno yake, kwa sababu hakuna baraza. Katiba ya Kenya inatambua kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa, lakini ukienda kwa ofisi ya Waziri ama uende kwenye idara zetu za kitaifa, utapata kwamba yule anayeongea Kiswahili hatasikizwa. Yule atakayeongea Kiingereza ndiye atasikizwa, ilhali hawa wote ni Wakenya na lugha ya Kiswahili inatambuliwa katika Katiba. Tukiwa na baraza kuu la Kiswahili hapa Kenya, hii lugha ya Kiswahili itatambulika katika maofisi. Leo hii, Mkenya akienda kwenye ofisi ama mahakamani, anaandikiwa stakabadhi zake zote kwa Kiingereza, ilhali yeye haelewi hiyo lugha. Akiingia ndani ya korti, yule hakimu naye anaongea kwa Kiingereza. Hivyo basi, Mkenya ambaye yuko katika taifa lake ambalo lina lugha asilia ya Kiswahili anashindwa kuendeleza kesi yake kwa lugha anayoitambua, ilhali hii lugha inatambuliwa kwenye Katiba. Hili baraza litahakikisha kuna mahakama ambazo ukitaka kuendeleza kesi yako kwa Kiswahili, unaenda huko an ukitaka kesi yako iendelezwe kwa Kiingereza, unaenda mahakama ya Kiingereza. Mahakimu na mawakili watashurutishwa na hili baraza kwamba lazima wawe wanajua Kiswahili sanifu. Leo hii ukienda katika hii shule ambayo inafundisha mawakili hapa Kenya, utaona wale mawakili wengi wanaanguka mitihani kwa sababu ya lugha ya Kiingereza, ilhali wako na lugha yao ambayo wanaweza kutumia kuendesha taratibu za korti. Jambo lingine muhimu ni kwamba Kiswahili ama lugha yoyote huwa ni ya kuendesha biashara. Afrika Mashariki ikiwa na lugha moja, biashara hapa kwetu itanoga, na kila mtu atakuwa na nafasi ya kufanya biashara bila kuwa na pingamizi. Kila mtu atakuwa na nafasi ya kufanya biashara bila kikwazo cha lugha. Leo hii, ukitaka kwenda kufanya biashara Sudan Kusini, utapata shida sana kwa sababu hamutaelewana kilugha. Lakini iwapo Afrika Mashariki yote itatumia lugha moja ya Kiswahili katika mawawsiliano, biashara katika nchi hizi itazidi kudumishwa, na watu watapata manufaa.
Mwisho kabisa, katika mpango wa Kenya Kwanza wa “ Bottom-Up”, lazima kuwe na lugha inayojumuisha kila moja ili hata ‘hustlers’ walioko chini waweze kutembea nchi nzima kutoka Kirinyaga, Kisumu hadi Somalia wakifanya biashara bila pingamizi ya lugha kwa sababu Kiswahili kitakuwa kimedumishwa. Wabunge wenzangu, ningependa Kiswahili kitukuzwe na kiheshimike kwa kudumisha Baraza la Kiswahili la Kenya, na kushurutisha Serikali kuhakisha kuwa Baraza hili limebuniwa na Kiswahili kueleweka.
Siku hizi, utapata kuwa wazazi wanafahamu Kiswahili na pia lugha za mama, lakini watoto hawajui lugha hizi, na wanazungumza Kiingereza peke yake. Kina nyanya wanapowatembelea, wanatatizika kuwasiliana na wajukuu kwa sabau wajukuu wanazungumza Kiingereza ambacho mara nyingi kina nyanya hawakifahamu. Mara nyingine, mama ni Mkikuyu na baba ni Mjaluo, lakini badala wafunze watoto Kiswahili, wanawafunza Kiingereza. Basi mababu wanapowatemebelea, wanashindwa kuzungumza na wajukuu. Utapata watoto wanakosa itikadi na nidhamu kwa kuwa hamna lugha ambayo wanaweza kutumia katika mafunzo na mababu wao.
Ningependa kuhimiza Bunge hili liunge mkono Hoja hii ambayo Mbunge wa Kamukunji ametuletea. Ameona mbali, na naunga mkono kwa dhati. Tudumishe Kiswahili na Kiswahili kitukuzwe.
Ahsante sana. Mbunge wa Nyali, Mhe. Mohamed Ali.
Ahsante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, naunga mkono Hoja hii. Vile vile, kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya kutaleta mabadiliko kabambe nchini Kenya. Kwa mfano, dhana ya kuleta uzalendo katika nchi hii ni kuhakikisha kwamba sisi sote tunazungumza lugha moja. Leo hii, wameondoka makaburu, wakaingia makaburu weusi ambao hawaipendi lugha yao – waafrika
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
wanaojifanya kuwa wazungu katika nchi zao. Lugha ya Kiswahili, ambayo inapaswa kuunganisha Wakenya, haiheshimiwi, haipewi hadhi yoyote, na imedharauliwa sana na watu wachache. Leo hii Kenya ina mayatima wa lugha ya Kiswahili, lugha ya uzalendo. Kuna ukabila Kenya kwa sababu tumekubali lugha zingine ziteke nyara lugha adhimu ya Kiswahili; lugha teule ya kitaifa ambayo sasa inatumiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ukabila utaisha katika nchi hii wakati ambapo sote, kwa kauli moja, tutakubali kuzungumza lugha hii adhimu ya Kiswahili, inayounganisha kila mtu. Mfano mzuri ni wanasiasa tunapoenda kufanya kampeni Mashinani tukiomba viti mbali mbali, hatutumii Kiingereza, kwa sababu tunajua hatutafua dafu. Tunajua vyema kuwa sera tunazouza hazitaeleweka zikiuzwa kwa lugha ya Kiingereza. Tunapofika mashinani, sisi hupiga siasa na kuomba kura kwa lugha ya Kiswahili. Lakini pindi tu tunapoapishwa na kuvaa masuti na kuja katika Bunge hili, tunajifanya wazungu zaidi ya wazungu wenyewe. Kiswahili kimedharauliwa hadi shule za kibinafsi ambazo hazifunzi lugha hii. Leo utakutana na vijana na wazee ambao ukiwazungumzia kwa Kiswahili, wanakwambia, e xcuseme; kwa kuwa hawaelewi lugha ya kitaifa ya Kiswahili. Leo hii, unapozungumza Kiswahili au kuomba kazi kwa lugha hii, unaonekana kuwa mjinga kwa sababu hujui lugha ya Kimombo. Huo ni ukoloni mamboleo. Tunapozidi kudharua lugha hii, ndivyo tunavyozidi kujidharau wenyewe kama Wafrika kwa kukataa lugha yetu. Lugha hii ni adhimu, na ndio lugha tamu duniani. Ukienda Ujerumani, Marekani na kote duniani, wote wanajifunza lugha ya Kiswahili. Mwaka uliopita, Afrika Kusini walijadiliana kuifanya Kiswahili lugha ya Afrika nzima. Lakini sisi wenye lugha ambayo ni kiio cha jamii ya Afrika, hatutaki kutumia lugha hii vizuri ili iweze kuunganisha Afrika yote. Lugha hii inaunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na ya Kati. Sasa hivi Jumuiya ya Afrika imekuwa kubwa. Kama alivyosema mwenzangu, Mhe. Owen Baya, Marais wa mataifa mengine wakizuru nchini Kenya, wanazungumza lugha ya Kiswahili kwa sababu nchi zao zimeongozwa na mabaraza ya Kiswahili, kama vile BAKITA, ambazo zinahakisha kuwa lugha hii imeheshimika na inaendesha Mataifa hayo. Kwa mfano, nchini Tanzania, watu hujadiliana kwa Kiswahili, shule wanafunza kwa lugha ya Kiswahili; na wameunganishwa na lugha moja. Hayati Julius Kambarage Nyerere aliondoka kama ameunganisha nchi ya Tanzania, ndio maana leo hakuna ukabila katika nchi hiyo. Tanzania mtu hakuulizi wewe ni wa kabila lipi. Hapa Kenya, utaulizwa unatoka katika kabila lipi; ila Tanzania unaulizwa “Kaka, unatokea sehemu ipi ya Taifa hili?” Hii ni kwa sababu hatuna lugha ya kutuunganisha. Hatuna heshima, hatuna mapenzi na hatuelewani. Lugha inayotawala ni lugha ya Kiingereza. Bi. Spika wa Muda, hapa Kenya watu wanapozungumza Kiingereza, wanaonekana wasomi. Ila mtu asiyejua lugha yake ya taifa si msomi; ni mjinga. Ni mjinga kwa sababu haelewi lugha yake, na anataka kujilazimisha kwa lugha nyingine huku akijiona msomi. Kiingereza si elimu tosha. Mtu asiye na elimu ya lugha yake amepotoka. Hata katika mahamaka zetu, asilimia kubwa ya wanaofungwa na kuwekwa katika magereza ni watu ambao hawajui kujitetea. Hii ni kwa sababu, wanapopelekwa kizimbani, wanasomewa mashataka kwa lugha ya Kiingereza. Mara nyingi hawaelewi kinachosemwa, na wanakubali tu. Wanasikiza mawakili wao bila kujua cha kusema. Asilimia kubwa katika jela hizi zetu wamefungwa kwa lugha ya mkoloni. Wao huitikia tu pasi na kujua. Lakini, hukumu ikitolewa na majaji ambao wanaelewa lugha ya Kiswahili, itakuwa ni rahisi kwa hustler pale kizimbani kujitetea na kueleza mambo yalivyokuwa. Bi. Spika wa Muda, sitaki kunena sana, lakini ninataka kumpongeza Mhe. Yusuf kwa kuleta swala hili la Kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya. Kongole sana. Natumahi Bunge hili litapitisha na kuhakikisha kuwa nchi inaunganishwa na lugha teule ya Kiswahili. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii.
Ahsante sana. Mbunge wa Seme, Mhe. James Nyikal.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuchangia Hoja hii. Ninaunga mkono Hoja hii ya kubuni Baraza la Kiswahili la Kenya kwa sababu ya shida moja kubwa kuliko shida yoyote nyingine tuliyonayo hapa Kenya. Shida hii ni kutoongea lugha moja. Pengine ni ukabila umetuzuia kuendeleza nchi hii yetu ya Kenya. Tukiweza kumaliza shida hizi, Kenya itaendelea. Tunahitaji chombo ambacho kitaunganisha Kenya iwe kitu kimoja. Tukiwa na lugha moja ambayo sisi sote tunazungumza itatusaidia. Ukiangalia vyama vyetu vya siasa, vyote ni vya ukabila. Watu wakiajiriwa kazini, wao huajiriwa kwa misingi ya kikabila. Katika ofisi za serikali, pia watu wameajiriwa kwa misingi ya kikabila. Kwa sababu hii, tunarudi nyuma. Kwa hivyo, chombo ambacho kitatuleta pamoja, kitasaidia sana. Kama chombo hicho kitakuwa ni kubuni baraza la Kiswahili hapa Kenya, basi nami ‘nafunga’ mkono Hoja hii. Mimi ‘nafunga’ mkono.
Lazima mjue hapa leo si mambo ya grammar, bali ni mambo ya kusema vile tunataka. Lazima tuelewane. Wacha grammar; kitu tunataka ni kuelewana. Watu wengi Kenya nzima wanazungumza Kiswahili; wengi kushinda wale ambao wanazungumza Kiingereza.
Mhe. Nyikal, Mhe. Wangwe anaomba akufahamishe. Unakubali akufahamishwe?
Nakubali.
Mhe. Emmanuel Wangwe.
Shukran, Mhe. Spika wa Muda na Mhe. (Prof) Nyikal. Napendekeza useme ni ‘kuunga mkono,’ bali sio ‘kufunga mkono.’ Kwa sababu yeye ni msomi, naomba tu tuelewane kwamba ile nia yake ilikuwa ni kuunga mkono. Asante sana Mhe. Spika wa Muda.
Endelea, Mhe. Nyikal.
Asante sana. Mimi naunga mkono na kukubali pia. Lengo la mazungumzo yetu leo si kujifundishisha grammar au ni nani anajua
bali ni kusema yale mambo yatawasaidia watu wa Kenya na Afrika nzima.
Subiri, Mhe. Nyikal. Mheshimiwa wa Dagoretti Kusini, John Waweru, hoja yako ya nidhamu ni gani?
Mhe. Spika wa Muda, ningependa nifahamishwe na nijue kama Mjumbe wa Seme yuko hakika kwenye Kanuni zetu za kudumu anapokejeli taaluma kama uigizaji. Hilo ni kwa sababu anaposema kwa njia ya kudhalilisha kwamba leo hatuko hapa kuleta drama . Drama ninavyoifahamu ni kuigiza. Na hakika uigizaji ni taaluma ambayo inaheshimika nchini. Wengine wetu tumekuzwa na taaluma hii ya uigizaji. Kwa hivyo, singependa taaluma hii ya uigizaji idhalilishwe na Mjumbe huyu wa Seme anaposema kwa kejeli kwamba leo hatuko hapa kufanya drama . Drama kwa Kiswahili ni uigizaji ama sanaa ya uigizaji. Mheshimiwa Spika, ningependa nijulishwe kama huyu Mjumbe yuko mbali na Kanuni zetu za kudumu anapodhalilisha taaluma ya maana kama hii ya uigizaji. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda.
Wewe hukusikia vizuri. Nilisema grammar sio drama .
Tena kwa sababu ya ukabila, watu wakifanya mitihani au kutafuta kazi, badala ya kuangalia mtu ana uwezo gani, tunaangalia anatoka upande gani. Kwa hivyo, saa nyingine watu ambao wako na ujuzi wananyimwa kazi, na watu ambao hawana ujuzi wanapewa kazi. Hio
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
kweli itaendeleza Kenya hii? Haiwezekani. Kwa sababu hiyo, ni muhimu sana tutafute njia ya kuunganisha Wakenya wote ili wawe kitu kimoja. Na kama ni lugha ya Kiswahili itakayofanya hivyo, basi tuendelee njia hiyo. Mimi sikatai; tumeendelea kukuza Kiswahili iwe lugha muhimu. Kiswahili kiko katika Katiba yetu. Sivyo? Tena, hata shuleni watoto sasa wanafundishwa Kiswahili vizuri kushinda wakati sisi tulikuwa shuleni. Sasa ukienda Nyanza, usifikiri utapata watoto wanazungumza Kiswahili vile mimi ninazungumza hapa. Watashinda hata wale watoto wanaotoka Pwani. Na juzi tu, mtoto ambaye aliongoza kwa Kiswahili nchini si alitoka Maranda? Hiyo ni sawa na hakuna neno.
Siku hizi tumetambua kuwa Kiswahili ni miongoni mwa mahitaji ya masomo unapoingia kazini, na hata katika vyuo vikuu. Zamani tulikuwa tunahitaji Kiingereza na Hesabu peke yake, lakini sasa tunahitaji Kiingereza au Kiswahili na Hesabu. Si tumeendelea? Si lazima tuendelee kufanya hivyo ili Kiswahili kiwe na umuhimu ambao unatakikana na utaonyesha ni lugha yetu. Wengine husema ni lugha ya mama, lakini si ya akina mama wote. Akina mama wengine hawakuwa wakizungumza Kiswahili. Hata Afrika au dunia nzima, watu wengi wanazungumza Kiswahili. Kwa hivyo, hata tukitaka kuunganisha Afrika nzima, ile lugha ambayo itatusaidia ni Kiswahili. Ukienda East na Central Africa, karibu nchi zote zinazungumza Kiswahili. Tunajua Tanzania inaongoza. Ukienda DRC, Rwanda, Burundi na Central African Republic, sote zinaongea Kiswahili. Kwa hivyo, tukitafuta ile lugha ambayo itaunganisha Afrika nzima, itakuwa ni Kiswahili. Unajua udhaifu mkubwa sana wa Afrika nzima ni kutokuwa pamoja. Tujenge lugha, pia tujenge barabara na uchumi ili watu watembee Afrika yote. Ukitembea nchi yoyote, kile kitu unahitaji sana ni lugha. Kwa hivyo itakuwa rahisi ikiwa watu wote Afrika watazungumza lugha ya Kiswahili. Watu watatembea, watafanya biashara na Afrika itakuwa kitu kimoja. Nguvu ya nchi ni watu kuwa wengi. Kama Afrika ingekuwa pamoja na sisi sote kuwa kitu kimoja, tungeendelea. Ukienda nchi kama India, imeendelea kwa sababu ina watu wengi. China ina watu wengi; Russia ina watu wengi. Kwa hivyo, tunahitaji Afrika iwe na umoja na watu wake wazungumze lugha moja. Napendekeza hiyo lugha iwe Kiswahili. Hata hapa, tuko na Kiswahili katika kitabu chetu cha Kanuni za Kudumu za nidhamu. Na hili lilikuja mwaka jana tu. Tunaendelea vizuri. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, naunga Hoja hii mkono kwamba tubuni baraza la Kiswahili la taifa la Kenya. Asante sana.
Asante sana Mhe. Nyikal. Nafikiri umewashangaza wengi kwa ufasaha wako wa lugha ya Kiswahili. Waheshimiwa Wabunge, ningependa kutambua waalimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Serare, kutoka eneo Bunge la Kajiado Kaskazini katika Kaunti ya Kajiado, ambao wameketi kwenye eneo la Spika. Tuwakaribishe hapa wanapofuatilia mjadala katika Bunge hili.
Mbunge wa Mathare, uko na hoja ya utaratibu?
Asante, Mhe. Spika wa Muda. Nilichotaka kuweka wazi ilikuwa kwa Mbunge wa Dagoretti wakati alikuwa analeta hoja ya nidhamu kwa Mhe. Nyikal. Nilitaka kumfahamisha rafiki yangu, Mhe. KJ, kwamba Mhe. Nyikal amejaribu sana. Unajua ‘Kiswahili sio mdomo chetu,’ vile tunavyosema kwa Kijaluo. Ndilo nilikuwa nataka kumfahamisha.
Nafasi hii tutaitoa kwa Mbunge wa Imenti Kaskazini, Mhe. Rahim.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Nashukuru, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii kuzungumza. Baadhi ya Waheshimiwa wengine wanafikiri kuwa siwezi kuzungumza Kiswahili. Ningependa kumpongeza Mhe. Daktari Nyikal vile ameweza... Tukiwa kwenye mkutano na ndugu yangu, TJ Kajwang’, alisema kuwa wao hawajui hii lugha, na wanakumbana na changamoto nyingi sana. Nakubaliana na Mhe. Yusuf kuhusu kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Kwa kweli, wakati huu tusipoboresha Kiswahili, sijui ni lipi tutakuwa tukifanya. Watu wengi katika maofisi ya kiserikali hawajui kuzungumza Kiswahili. Wafanyikazi hawa hushindwa kuwasaidia wale ambao hawajui Kizungu. Labda kule Nyanza ndiko wanazungumza Kizungu kuliko Kiswahili. Kenya nzima tunafaa kujivunia lugha ya Kiswahili, kwa sababu tunaweza kuiongea mahali popote. Mhe. Nyikal amesema mambo ya Uhindi, lakini hajafahamu kwamba kule wanazungumza lugha zaidi ya elfu moja. Hata Uchina labda kuna lugha aina tofauti. Lakini ni muhimu lugha yetu ya Kiswahili itumiwe katika nyanja zote, haswa katika ofisi za Serikali. Ukienda town, watu huzungumza Kiswahili tofauti kulingana na mahali wametoka. Ukienda kwa duka la Mhindi, atakuongelesha Kiswahili ambacho hautaelewa. Ukienda Eastleigh, Kiswahili cha Msomali ni tofauti. Naomba tuweze kubuni baraza hili ili watu wote wafunzwe Kiswahili sanifu, na tuweze kuboresha mawasiliano.
Kama vile, Mhe. KJ ametuelezea mambo ya drama, ni muhimu baraza hili libuniwe ndio kila mtu aweze kufunzwa Kiswahili shuleni. Siku hizi ukienda shuleni, utapata ubaoni wameandika kwa Kizungu peke yake. Tunafaa kuwaweka watoto wetu maanani, na kitu cha kwanza ni lazima wafunzwe Kiswahili kisha waendelee na Kizungu huko mbele. Wizara ya Elimu na Kamati ya Elimu hapa Bungeni zinafaa kuangalia kwamba watoto wakiwa wachanga kabla wafike gredi ya nne, wasifunzwe Kizungu peke yake. Inafaa wafunzwe Kiswahili pia, ndio kila mtu hapa nchini aelewe Kiswahili. Namshukuru Clerk wetu, bwana Kirui, kwa sababu tukiwa naye katika Kamati ya kutengeneza Kanuni za Kudumu, yaani
, kwa Kiswahili, ilikuwa vigumu sana kwa watu wengi kutafsiri maneno. Hii Hoja ni muhimu sana. Namshukuru Mhe. Hassan, na asiiwachie hapa, lakini afanye mpango na Wizara ya Elimu pamoja na Kamati ya Elimu ndiyo iweze kufanywa sheria. Mhe. Spika wa Muda, sitaki kuongea zaidi ya hapo. Ningependa wenzangu wote waunge Hoja hii mkono ndiyo tuipeleka mbele, ili watu waweze kuongea Kiswahili. Ni muhimu sana kuongea Kiswahili. Nikiwa kwenye kampeni, sijawai kuongea Kizungu. Watu wa eneo langu la Bunge hawafahamu Kizungu; labda niongee Kimeru ama Kiswahili. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga Hoja hii mkono. Nataka kuwachia hapo. Asante sana.
Mbunge wa Moiben, Phylis Bartoo.
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kumpatia kongole Mhe. Hassan kwa kuleta Hoja hii ya Kiswahili hapa Bungeni. Katika vifungu vya 7 (1) na (2) vya Katiba ya Kenya, lugha ya Kiswahili imepewa kipao mbele katika taifa la Kenya, haswa matumizi yake. Kwa mfano, Kiswahili kimetambuliwa kama lugha ya taifa la Kenya. Katika vyuo vikuu vya kitaifa na shule za sekondari, Kiswahili pia kimepewa kipao mbele. Ndipo sasa tunahitaji baraza la Kiswahili, ili liweze kushughulikia lugha ya Kiswahili ipasavyo. Tukitengeneza baraza la Kiswahili hapa Kenya, litaweza kushughulikia mambo mengine ambayo hayajatambuliwa. Nimesikiza kwa makini vile Mhe. Hassan amepiga debe, na vile Wabunge wenzangu wamechangia. Hii inamaanisha kwamba sasa ni wakati mwafaka wa kupeleka Kiswahili kiwango kingine. Sitaki kusema mengi, ila kumpatia Hassan kongole, na kuwasihi Wabunge wenzangu kuunga mkono Hoja hii ndio Kiswahili kiendelee mbele. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda.
Asante. Nampatia nafasi hii Mbunge wa Sigor, Peter Lochakapong.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Asante sana, Mhe.Spika wa Muda kwa nafasi hii. Naunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na mwenzetu Mhe. Yusuf Hassan, Mbunge wa Kamukunji, ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya. Mhe. Spika wa Muda, kabla niendelee na Hoja hii, kwa sababu nimepata fursa ya kuongea mara ya kwanza katika Bunge hii ya kumi na tatu, niruhusu niwashukuru watu wa eneo Bunge la Sigor kwa kunichagua mara ya pili mfululizo. Wamenipatia nafasi ya kuwahudumia kwa mara ya pili katika Bunge hili la kitaifa. Kwa hivyo, ninawashukuru wote ambao waliniunga mkono na kunipigia kura, haswa watu wazuri wa eneo Bunge la Sigor kwa kuweka historia na kunichagua kwa mara ya pili, jambo ambalo halijawahi kufanyika katika miaka 35 iliyopita. Kwa hivyo, ninaahidi kwamba katika muhula huu ama kipindi hiki cha miaka mitano ambacho niko katika Bunge hili kuwawakilisha watu wangu wa Eneo Bunge la Sigor, nitaendeleza ile kazi nzuri ambayo tulikuwa tumeanza. Nawashukuru sana kwa nafasi hii. Nikirudi kwa Hoja iliyoko mbele yetu, ningependa kusema kwamba Kiswahili kinatambuliwa na Katiba ya Kenya kama mojawapo ya lugha za taifa. Kwa hivyo, tumechelewa kubuni Baraza hili ambalo litashughulikia mikakati, kubuni sera na kuweka utaratibu wa kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa ajili ya watu wetu. Lugha ni muhimu katika jamii. Lugha inapokuzwa inasaidia sana kuunganisha jamii na kuendeleza biashara. Jambo la muhimu ni kwamba Baraza hili litakapoweka mikakati ya kuendeleza lugha ya Kiswahili katika Jamhuri ya Kenya, watu wengi wataelewana. Hii ni kwa sababu lengo kubwa la lugha yoyote ni kuwawezesha wanaotumia lugha hiyo kuwasiliana na kuelewana. Kubuniwa kwa Baraza hili, ambalo kazi yake itakuwa ni kuhakikisha kwamba Wakenya wanaelewa, wanaongea na wanawasiliana kwa lugha ya Kiswahili, ni jambo muhimu litakalonufaisha Wakenya wote.
Najua kwamba wengi wetu katika Bunge hili hutumia lugha ya Kiswahili tunapoomba kura na tunapokutana na watu wetu kule vijijini. Sisi hutumia Kiswahili tunapowasiliana na wakazi katika maeneobunge na kuwasilisha hoja zetu. Lugha ya Kiswahili ni muhimu kwa sababu inawawezesha watu kuelewa ni nini hasa tunachowaambia. Ndio maana namshukuru Mheshimiwa Yusuf Hassan kwa kuileta Hoja hii na ndiposa naiunga mkono. Jambo lingine muhimu ni kwamba lugha ya Kiswahili inaunganisha watu wa Afrika Mashariki. Watu wa Afrika Mashariki watakapoungana, itakuwa rahisi kufanya biashara na majirani wetu. Mhe. Spika wa Muda, umesikia kuwa watu wengi, hata humu Bungeni, wanasema kwamba lugha ya Kiswahili ni ngumu kwa sababu Kiswahili ambacho tumezoea kuzungumza ni kile ambacho tunatumia tunapoomba kura kule nyanjani. Lugha ambayo watu wanaamini sana si Kiswahili sanifu. Kwa hivyo, tunapokuja hapa na kusema kwamba ni wakati wa kila mtu kuzungumza Kiswahili sanifu, hali hiyo huleta utata kidogo na wengi wetu tunasema kwamba lugha hiyo ni ngumu. Hiyo ndio sababu kuu zaidi ya kubuni Baraza hili la Kitaifa kupitia Hoja hii – ili wale watakaopewa nafasi ya kuendeleza lugha hii waweze kutoa mwongozo ambao utatusaidia sisi sote kujifunza Kiswahili vizuri ili tuweze kuwasiliana na watu wetu kwa njia bora zaidi. Tunapowasiliana na Wakenya ambao tunawakilisha hapa Bungeni huwa tunatumia lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, tukiendeleza lugha ya Kiswahili katika taifa hili, tutawaleta Wakenya wote pamoja tunapowasiliana nao kwa lugha ambayo wanaelewa. Ikiwa Wakenya wataelimishwa kuhusu sera za Serikali kwa lugha ambayo wanaielewa, itakuwa rahisi sana kwao kuiunga mkono Serikali. Wenzetu katika mataifa jirani tayari wamebuni mabaraza ya Kiswahili. Inaonekana sisi tumechelewa kidogo. Sisi, viongozi tulioko hapa, tukiipa lugha ya Kiswahili kipaumbele, viongozi wengine Serikalini watatuiga na kuendeleza Kiswahili kwa njia moja ama nyingine. Jambo hili litachangia kuwepo kwa uzalendo katika taifa letu kwa sababu sisi sote, kama
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
viongozi, pamoja na wale tunaowaongoza, tutakuwa tunaongea kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, naomba sisi sote tujitahidi kuzungumza kwa Kiswahili. Tukipata nafasi yoyote ya kuhutubia wananchi, tufanye hivyo tukitumia lugha ya Kiswahili, ikiwezekana, ili watu wetu pia waige mfano huo. Sote tunapoongea kwa Kiswahili, tutaweza kuiendeleza lugha hii. Tarehe saba, mwezi wa saba ni siku ya Kiswahili duniani. Hiyo ni siku ambayo imetengwa kwa ajili ya lugha yetu ya kitaifa ili dunia nzima iweze kuitambua. Kiswahili kitawaunganisha wakazi wa Afrika Mashariki na bara zima la Africa. Kama viongozi, tunapaswa kuendeleza na kukikuza Kiswahili ili tusonge mbele. Nawahimiza viongozi wote katika Serikali wawaelimishe Wakenya kuhusu sera za umma wakitumia lugha ya Kiswahili. Wakenya wanaielewa lugha hiyo. Nashukuru sana kwa sababu Bunge letu limeweza kuchapisha Kanuni za Bunge – The
– kwa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, si Wabunge wengi ambao wameziangalia, kuzisoma na kujaribu kuzitumia. Hii ni nafasi mwafaka ya kuwahimiza Waheshimiwa wenzangu wazisome Kanuni za Bunge wazielewe na wajaribu kutumia Kiswahili katika Bunge hili. Kwa hayo machache, naiunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Mheshimiwa Yusuf Hassan, Mbunge wa Kamukunji.
Mhe. Martha Wangari): Asante sana. Waheshimiwa Wabunge, ningependa kuwatambua wanafunzi na waalimu wa Makini School kutoka eneo bunge la Dagoretti Kaskazini, Kaunti ya Nairobi, ambao wameketi kwenye Public Gallery . Kwa niaba yangu na ya Bunge la Taifa, nawakaribisha watazame shughuli za Bunge ukumbini. Nitampa nafasi Mbunge wa Likoni, Mhe. Mishi Mboko.
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Leo ni siku ya furaha na bashasha. Nampa kongole Mbunge wa Kamukunji kwa kuleta Hoja hii inayopendekeza kubuniwa kwa Baraza la Kitaifa la Kiswahili. Kwa hakika, pendekezo hili lingekuja kitambo sana. Lakini Waswahili wanasema kawia ufike. Hayawi hayawi, huwa. Leo tunaona kuwa mwanzo wa ngoma ni lele mama, na lele mama la kuweka Baraza Kuu la Kiswahili katika Taifa la Kenya limeanza. Tunajua pia ngoma itafika wakati mwafaka. Kwanza, tunatambua kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa. Vile vile, ni lugha rasmi ya kitaifa sawia na lugha ya Kiingereza. Ajabu ni kuwa tumeendeleza ukiritimba wa lugha ya Kiingereza ilhali lugha ni mbili – Kiingereza na Kiswahili. Kwa hivyo, jamani wakati umefika, na ni sasa. Kama si sasa, ni sasa hivi. Tuitukuze lugha yetu kwa sababu Kifungu cha 137 katika ule mkataba ama mapatano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kimezungumzia kuwa ni lazima tuitukuze na kuiboresha lugha ya Kiswahili kwa sababu ndiyo lugha ambayo inaweza kutupatia mawasiliano bora katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki. Tunajua kwamba katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki tuna mapatano mengi sana, ikiwemo mambo ya kilimo, ajira, biashara, mazingira na mambo mengi zaidi ambayo yanatuunganisha sisi kama mataifa katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Inafaa tutafautishe baina ya mtu ambaye ameelimika na mtu ambaye anajua lugha, tusiwe tunafikiria kwamba iwapo unajua Kiingereza basi wewe umeeelimika ama wewe una elimu ya juu. Unaweza kujua Kiingereza lakini ukawa huna elimu. Kuna yule anajua Kiswahili na akawa na elimu ya juu sana. Kiingereza ni lugha tu, si elimu. Tukiangalia Tanzania, kuna watu ambao wamebobea sana katika nyanja tofauti, lakini hawajui Kiiingereza, wanaongea lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, jambo hilo ni lazima kutofautisha. Jambo la pili ni kwamba lugha ya Kiswahili ndio lugha pekee ambayo inaweza kuondoa ukabila katika taifa letu la Kenya. Leo hii katika taifa letu la Kenya tuna lugha za kikabila zaidi ya 45 na hivyo basi zinazidi kututia katika mambo ya kikabila, iwapo hatutachagua lugha moja ambayo itatuunganisha. Tukiweza kutukuza lugha hii ya Kiswahili, mambo ya kikabila na tofauti zetu za kikabila zitapungua.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Katika kuendeleza elimu, Kiswahili ni lugha ambayo tungeweza kusaidia haswa wanafunzi ambao wamekuwa wazito katika kujua lugha ya Kiingereza ama wamekuwa na sintofahamu kuelewa mufti lugha ya Kiingereza. Iwapo pia tutaweza kuwafasiria kwa lugha ya Kiswahili, huenda wakaelewa zaidi na kubobea katika masomo yao. Nchi jirani za Rwanda, Uganda na Burundi haziko karibu sana na Tanzania lakini wameweza kukuza Kiswahili katika kiwango cha juu. Leo sisi Kenya na Tanzania ni kama mtoto wa mjomba na shangazi ama kama pua na ndevu maanake tuko hapo kwa hapo, sako kwa bako. Kwa hivyo, ni lazima tukuze lugha hii ili iweze kupata wasifa kama lugha zingine. Leo ukienda Ujerumani utapata wanaongea kijerumani na wana elimu na wanatukuza lugha yao. Ukienda Ufaransa, utapata wanaongea Kifaransa na wana elimu na wanatukuza lugha yao. Kwa hivyo, sisi pia ni lazima tutukuze lugha yetu. Tunapotukuza Kiswahili na kukiboresha, tutaweza kuboresha tamaduni zetu pia. Kiswahili kimechukua pia lugha za Kibantu na hapa tena katika taifa letu la Kenya tumeona lugha nyingi ni za Kibantu. Maneno fulani ya Kibantu yemechukuliwa na kuwekwa kwenye Kiswahili. Maneno ya Kiarabu pia yamechukuliwa na yameunganishwa pale ndiposa tumeweza kupata hii lugha ya Kiswahili.
Kwa hivyo, tukiweza kuitukuza na kuipa kipaumbele, tutaweza kuwa na mabadiliko mengi sana. Zaidi ya watu milioni 200 ulimwenguni wanaongea lugha ya Kiswahili, na lugha ya Kiswahili ni lugha tamu! Unajua, kuzungumza Kiswahili pia si kuzungumza tu, ni lazima utoe ile lafudhi na ile sauti, kwa Kiingereza tunayosema ni the tone, lakini kwa Kiswahili ni lafudhi; na sauti ni lazima iwe inaambatana na lugha hii, basi unapoizungumzia utasikia ni lugha tamu sana. Hata ukizungumza kwa ile lafudhi ya sawa katika mambo yetu ya kinyumbani, mambo ya kimapenzi, unaona ni lugha ambayo inatoa ushawishi na inatoa furaha na bashasha kuliko lugha nyingine. Naona Mhe. Didmus anacheka lakini kwa upande huo pengine ukinifuata ninaweza kukuelimisha zaidi ndiyo unielewe kinaga ubaga ninamaanisha nini. Kwa hakika sisi tunahitajika tuingie katika historia. Kama wenzetu wa Tanzania na Zanzibar wameweza kutengeneza baraza hili la Kiswahili na sisi ni wale wanaita kwa Kiiingereza the big brother ama wale makaka wakubwa katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, tunatakikana kuwa sisi ndio tunaongoza katika mipango kama hii ili tuweze kuboresha muungano wetu na kuweza hata kuboresha mambo yale ya kisiasa ambayo yanahitaji kujumuishwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa wale ambao hawajaelewa, kwa Kiingereza ni Political Federation . Tukitaka kuiweka iwe sawia na sisi, ni lazima lugha ya Kiswahili iwe sawia. Kwa sababu hata tunapoomba kura, hapo ambapo tunatoa hotuba zetu za kisiasa tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili. Tunapokwenda kwa vyombo vya habari kuzungumzia sera, shabaha na malengo yetu, tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili. Na iwapo mambo mengi katika shughuli zetu za kijamii tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili, kwa nini lugha hii tusiipatie kipaumbele? Kwa nini lugha hii tusiitukuze? Kwa nini lugha hii isiwe na baraza lake? Baraza hili pia litaweza kukuza ajira. Leo tuna Wakenya wengi ambao wamebobea, ni mahiri katika lugha ya Kiswahili lakini wamekosa ajira kwa sababu pengine nafasi za kuweza kuonyesha umahiri wao ama ugwiji wa lugha hii ya Kiswahili hakuna. Kwa hivyo, tukiwa na baraza kama hili linaweza pia kutengeneza ajira aina tofauti katika taifa letu. Tukiwa sasa tuko kwa ugatuzi tunajua kwamba itaenda mpaka kule mashinani ili watu wajue kwamba lugha hii sasa ni lugha ambayo unaweza kuizungumzia katika mahakama, utaweza kuizungumza katika zahanati kupata afya, utaweza kuizungumza katika taasisi yoyote ya umma ili uwe na wepesi na upatiwe nafasi, na umekuwa huru kuzungumza lugha hii. Kwa hivyo, mimi nataka nimwambie Mhe Yusuf kuwa kuleta Hoja hii kwa hakika ametufurahisha sote kama taifa la Kenya, na kwa hakika umetufunza lugha ambayo itaweza kufanya tamaduni zetu ziweze kuheshimika, si katika Taifa la Kenya pekee lakini katika bara
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
la Afrika. Na bara la Afrika likiwa na lugha moja ya kitaifa, basi tutaweza kuwa na ule muungano wa Afrika yote na tutakuwa na nguvu. Asante sana.
Mhe. Martha Wangari): Asante Mhe. Mishi Mboko. Nafasi hii nitampatia mwanafunzi wako, Mhe. Didmus Barasa wa Kimilili, ambaye amekuwa mwanafunzi rasmi kwa mambo kadhaa wa kadha.
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuchangia Hoja hii muhimu ya kuirai Serikali ibuni Baraza la Kiswahili la taifa. Ninakubaliana na Hoja hii na ninaiunga mkono kwa sababu Wakenya wengi hawajui lugha ya Kiingereza lakini kila Mkenya, mpaka hata marafiki wetu, kama vile Mheshimiwa T.J. Kajwang’, siku hizi wanazungumza Kiswahili sanifu. Kama alivyosema Mhe. Mboko, ni lazima Kiswahili kiwepo ama kitambuliwe na mashirika tofauti ya Serikali. Ninakubaliana na hilo. Ili tukikuze Kiswahili, naweza pia kumwomba Mhe. Mishi Mboko kwamba kuanzia leo, akiniandikia jumbe fupi katika WhatsApp asitumie Kiingereza kama kawaida yake, bali atumie Kiswahili. Vilevile, nimefurahi siku ya leo kwa sababu miongoni mwa wanafunzi walioko hapa ni binti wangu wa kwanza anayeitwa Chelsea Didmus, kutoka Shule ya Serare. Yuko pale ananiona. Wiki iliyopita alishinda akinifunza Kiswahili na nafikiri hilo ni jambo zuri sana. Ninampongeza Mheshimiwa kwa kuleta Hoja hii kwa sababu wapo wagonjwa wengi ambao wakienda kutafuta huduma za matibabu, pengine wanapata daktari ambaye hajui ama haelewi Kiswahili na mara nyingi wakienda kutibiwa wanazungushwa. Mara nyingi ukienda kutibiwa huwa unamueleza daktari sehemu za mwili ambazo zina maumivu. Kwa hivyo, inakuwa vigumu kwa daktari yule na mgonjwa kuwawasiliana vizuri. Kuwepo kwa Baraza la Kiswahili katika nchi ya Kenya itawalazimisha hata wale wanaotoka nchi za ughaibuni na kufanya kazi katika nchi yetu ya Kenya, kuenda skuli wakajifunze jinsi ya kuzungumza na kuelewa lugha ya Kiswahili, kama ilivyo desturi ya Wakenya wengi wanaofanya kazi katika nchi ambako Kiingereza hakizungumzwi. Wakenya wanapowasili katika nchi hizo, inawabidi wajifunze lugha zinazozungumzwa huko, kama vile Kifaransa, Uturuki au Kiarabu. Kwa hivyo, itakuwa ni vizuri nchi ya Kenya iwe na baraza kuu la lugha ya Kiswahili. Vile vile, tunaomba kuwa kandarasi nyingi za zabuni zitayarishwe kwa lugha ya Kiswahili. Kuna bidhaa ambazo mwananchi wa kawaida huenda kununua ilhali hazifahamu kwa lugha ya Kiswahili. Nilijua hivi majuzi tu kwamba spare parts ni vipuri kwa lugha ya Kiswahili. Nilikumbushwa na Mhe. Mishi Mboko. Kuna siku gari langu liliharibika nikiwa Mombasa. Nilipoenda kutafuta gear box na plugs ikawa ni matatizo matupu kwenye mawasiliano. Baada ya siku mbili, rafiki yangu mswahili alimueleza mwenye duka kwa lugha aliyoielewa kwamba nilitaka vipuri vya gear box ndio gari langu likatengenezwa. Nina hakika kwamba kama kungekuwepo na baraza la Kiswahili katika nchi ya Kenya, singesumbuka. Ningeenda tu kwa duka niseme ninataka kifaa fulani na mambo yangekuwa mazuri. Jambo la mwisho, na ambalo ni muhimu sana, ni kuziomba taasisi za Serikali zitilie maanani Hoja ambazo hujadiliwa na kupitishwa na Bunge la Taifa. Tukizungumzia Hoja tofauti tofauti, wakuu serikalini, wakiwemo mawaziri wanaohusika, wanastahili kuhakikisha kwamba masuala yanayojadiliwa na kupitishwa hapa Bungeni yanafuatiliwa na kutekelezwa. Ninashukuru kwa sababu tunaye Bwana Spika ambaye lugha yake ya Kiswahili imeanza kuwa sanifu sana. Atakuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Serikali ya Kenya inahakikisha kwamba Hoja tunayoizungumzia hivi sasa imeweza kutimizwa ili kila Mkenya popote alipo aweze kuzungumza Kiswahili. Vile vile, Kiswahili ni lugha ya taifa, na inazungumzwa katika nchi nyingi ulimwenguni. Nilishangaa hivi majuzi nilipokuwa katika taifa la Afrika Kusini, nilipokuwana na wananchi wa taifa hilo waliokuwa wakizungumza Kiswahili. Pia, nilikuwa katika nchi ya Congo, ambako nilikutana na Wakongo waliokuwa
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
wakizungumza Kiswahili. Nimekuwa katika nchi ya Uganda, na Waganda pia wanazungumza Kiswahili. Kwa hivyo, ni lazima sisi pia, tukiwa nchi-mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tukikuze Kiswahili kikiwa mojawapo ya lugha za kuimarisha umoja wa Afrika Mashariki. Mhe. Spika wa Muda, kuweko kwa Baraza la Kiswahili humu nchini kutatoa nafasi kwa wageni kutoka mataifa tofauti kama vile Ufaransa na Nchi za Umiliki wa Kiarabu ili waweze kujifunza, kuzungumza na kukikuza Kiswahili. Ningependa pia Serikali yetu ifuatilie utekelezaji wa pendekezo hili. Kwa mfano, kukiwa na kongamano za kimataifa, ni muhimu kuwe na wakalimani watakaokuwa wakitafsiri lugha ya Kiswahili kwa lugha ya Kiingereza na Kifaransa ili washikadau kutoka nchi hizo waweze kuelewa yanayojiri kwenye kongamano, na pia waweze kushiriki kwenye mahojiano yoyote yale kupitia usaidizi wa wakalimani hao. Tukihudhuria kongamano katika nchi ambako Kifaransa ndiyo lugha rasmi, kama vile nchi za Africa Magharibi, mazungumzo yote hufanywa kwa lugha ya Kifaransa na wakalimani hutafsiri kutoka lugha ya Kiingereza hadi kwa Kifaransa ama kutoka lugha ya Kifaransa hadi lugha ya Kiingereza ili wanaohudhuria kongamano hilo waweze kufahamu yanayojiri. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza, tena kwa dhati, Mhe. Yusuf kwa kuileta Hoja hii muhimu sana Bungeni. Kwa mara ya kwanza, nimemuona rafiki yangu, Mbunge wa Embakasi Kaskazini, Mhe. Babu Owino, akiwa amebeba Kamusi ya Kiswahili. Mhe. Mishi Mboko alipokuwa akizungumza, Mhe. Babu Owino alikuwa akipekua kamusi hiyo. Mhe. Babu Owino amekuwa akiwafunza wanafunzi wa Kidato cha Nne kupitia akaunti yake ya Facebook . Ninamuomba kuanzia kesho aanze kuwafunza kwa lugha ya Kiswahili. Kuna wanafunzi wengi humu nchini ambao hawaelewi kile kizungu chake kikubwa. Mhe. Mishi Mboko, ninakupongeza. Nakuomba umuorodheshe Mhe. Babu Owino kama mwanafunzi wako wa Kiswahili kwa kuwa Kiswahili chake ni kibovu sana na hakieleweki. Kwa haya yote, naiunga mkono Hoja hii.
Nafasi hii ni ya Mhe. Josses Lelmengit kutoka Emgwen. Inaoneka Mhe. Josses hayuko. Kwa hivyo nampa nafasi Mhe. Robert Pukose.
Nashukuru, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Yusuf Hassan, Mbunge wa Kamkunji. Lengo lake ni kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa la Kenya. Lugha yetu ya Kiswahili ni safi. Itakuwa vyema lugha za Kiswahili na Kiingereza zikienda sambamba. Mambo mengi tunayoyafanya tunahitaji lugha itakayotuwezesha kufanya shughuli kadhaa wa kadha; haswa za kimasomo, kibiashara na kimatibabu. Mimi, kama daktari, mara nyingi napenda mgonjwa anieleze kuhusu ugonjwa alionao kwa lugha ambayo anaifahamu vizuri. Kuna watu ambao wanapoongea wanatumia lugha isiyoeleweka. Kizazi cha sasa kinatumia lugha ya mtaa ambayo inaitwa Sheng . Rafiki yangu, Mhe. Babu Owino na jirani yangu Mhe. Caleb Amisi, wanaongea lugha ya Sheng . Hawa vijana lugha yao ni sheng . Hivyo ndivyo tunapoteza lugha yetu ya Kiswahili. Lugha ya Sheng haieleweki miongo mwa Wakenya wengi na watu kutoka mataifa jirani. Inasemekana Kiswahili kilizaliwa kule Zanzibar…
Mbunge wa Embakasi Mashariki.
Ni Mbunge wa Embakasi Mashariki, Mhe. Spika wa Muda.
Okay. Mbunge wa Embakasi Mashariki.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nilikuwa nimekuomba nafasi nilete hoja ya nidhamu lakini siwezi...
Ni Hoja ya Nidhamu.
Siwezi kukulaumu, Mhe. Spika wa Muda.
Inabidi utuambie unaleta hoja ya nidhamu chini ya Kanuni gani.
Ahsante sana. Mhe. Spika wa Muda, Mhe. Pukose amesema mimi huongea Sheng, ambayo ni lugha isiyoeleweka. Nataka kukuambia kwamba leo hii nimejawa na bashasha, mpekwempekwe, chakari za kungulu…
Maanake tunatukuza Kiswahili lakini nimeona Wabunge wengi hapa hawaelewi hii lugha. Kwa hivyo, ni muhimu sana Wabunge warudi shule ili wasome lugha ya Kiswahili. La mwisho…
Mhe. Babu Owino, inafaa utueleze ni Kanuni gani ambayo unaeleza.
Nataka kujibu mwenzangu kwa sababu amesema mimi huongea Sheng.
Utamjibu nikikupatia nafasi ya kuchangia, tafadhali.
… (Aliongea nje ya rekodi)
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Lahaja ambayo Mhe. Babu anaongea ni Kiswahili ambacho hakijakuzwa kwa njia safi. Wanasema Kiswahili kilizaliwa kule Zanzibar na Tanzania. Kililelewa hapa Kenya, kikakufa kule Uganda na kikazikwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mimi ni jirani wa nchi ya Uganda. Kwa sasa, wameanzisha Kiswahili katika shule za msingi na sekondari. Kwa hivyo, Kiswahili kinaendelea kuamka sasa. Mhe. Hassan ameleta Hoja hii wakati unaofaa. Tukiwa na Baraza la Kiswahili la Kenya litashughulikia suala la kukizuza Kiswahili, na sio kulazimisha Kiswahili kitumike mahali ambapo hakifai. Baraza hilo litahakikisha kwamba Kiswahili kinachotumika ni nadhiri ama kinakubalika na kila mtu.
Kiswahili kilibuniwa kutoka kwa lugha za kibantu na Kiarabu. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba Kiswahili tunachotumia ni sanifu, ili kitumike kwa mambo yote. Jamii zingine zinatumia Kiswahili ambacho ni tofauti. Kwa mfano, majirani wangu kama Mhe. Kalasinga hapa, akitaka kusema anaenda, anasema “naendako” ama “nakujako”. Hapa unaona lugha ya Kiswahili haitumiwi vizuri.
Sisi, majirani wa Mhe. Kalasinga, tunaelewa akisema “ninakujako bwana”. Tunafahamu anakuja na anasema kwa njia nzuri. Lakini, mtu kutoka sehemu nyingine hataelewa. Tulipohudhuria michezo kule Tanzania, Wakenya tunapenda kusema ‘nipe’ kitu fulani, lakini Watanzania kwa lugha yao wanasema “tafadhali naomba”. Wakenya hatutaki kusema hivyo. Sisi tunasema “lete hii” na tunaona sio madharau. Lakini ukiambia Mtanzania “leta hii” hata kama ni kwa duka, anaona kama unmadharau. Kwa hivyo, ni lazima tujaribu kutumia Kiswahili sanifu, na kwa njia ambayo ni ya heshima, ili kila mtu aridhike katika nchi yetu.
Sitaki kusema mengi sana. Namshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii. Natarajia kwamba ataenda zaidi ya hapo na kutengeneza Mswada ambao tutaujadili na
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
kuupitisha hapa Bungeni ili uweze kuwa miongoni mwa Sheria za Kenya. Tukifanya hivyo, tutaliwezesha Baraza la Kiswahili lililopendekezwa hapa kufanya kazi ambayo tunaizungumzia. Tunapoileta kama Hoja sasa hivi, hatujafanya chochote. Pale tumeonyesha maoni ama nia yetu ya kufanya hayo. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda.
Ahsante, Mhe. Pukose. Nafasi hii ni ya Mhe. Abdul Haro kutoka Mandera Kusini.
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa adimu niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa bungeni na Mhe. Yusuf Hassan, ambaye namshukuru sana. Hoja hii inaihimiza Serikali, kupitia vyombo vya dola husika, kuanzisha Baraza la Kiswahili. Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu ya mambo kadhaa ambayo baadhi ya Wabunge wenzangu wamegusia. Mbali na kuwa lugha pekee ya Kitaifa, lugha ya Kiswahili pia huwa inatumiwa kama nembo ya umoja wa taifa, ama symbol of national unity kwa Kimombo. Pia lugha hii inazungumzwa na Wakenya wengi, hasa wale ambao wanaishi kule mashinani. Umuhimu wa Baraza la Kiswahili ambalo tunahimiza kubuniwa kupitia Hoja hii ya Mhe. Yusuf Hassan sio tuu litasaidia kukuza uenezaji wa uzungumzaji wa Kiswahiki katika Taifa hili, bali pia litasaidia katika kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili sanifu katika shule zetu.
Tusisahau kwamba somo la Kiswahili linahitajika, hasa wakati wanafunzi wanapotaka kuendelea na masomo katika taaluma zingine za juu. Kwa mfano, wanafunzi ambao wanataka kujifunza taaluma ya Kiswahili, somo la Kiswahili ni muhimu. Ni lazima uwe umefanya vizuri katika Kidato cha Nne ili uweze kuingia katika taasisi za kufunza taaluma ya ualimu. Hata wale ambao ni mawakili, tunafahamu kwamba lugha ya Kiswahili inahitajika katika taaluma hiyo.
Namshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya kusaidia kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Litakapobuniwa, Baraza hilo litachangia ukuzaji wa Kiswahili katika kuzungumza na pia itahimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli za kila siku serikalini. Kwa mfano, Bunge ama wizara za Serikali muhimu, zitatumia lugha ya Kiswahili kwa sababu hii ndiyo lugha ambayo inatumiwa na Wakenya wengi katika mawasiliano yao ya kila siku. Baraza la Kiswahili litasaidia kuhimiza matumizi ya Kiswahili sanifu katika taasisi zetu zote za elimu na ofisi zetu kama vile Bungeni na kwenye idara zinginezo. Baraza la Kiswahili pia litasaidia katika kutafsiri. Kwa mfano, litatafsiri ripoti ambazo zinatoka katika taasisi fulani, vitabu na pia sera za Serikali ambazo zinaweza kutumika mashinani na kueleweka vizuri na wananchi wetu wengi ambao wanategemea kuzungumza lugha ya Kiswahili.
Baraza la Kiswahili likibuniwa litasaidia kutoa huduma za tafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Ninafurahi kwa sababu lugha ya Kiswahili inazungumzwa na wananchi wengi katika kanda ya Afrika Mashariki, ambako tuko. Pia, ni lugha rasmi ambayo inazungumzwa katika Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.
Kwa hayo machache, Mhe. Spika wa Muda, namshukuru tena Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili.
Mhe. David Ochieng
Starehe, JP
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
hawajaenda shule na hawafahamu Kiingereza. Lugha mbadala ya kuweza kupata usaidizi katika ofisi ya Serikali ni lugha ya Kiswahili. Wananchi wanakuwa na changamoto kubwa, hasa vijana wenye umri mdogo ambao wanatumia Sheng, wanapokuja kwenye ofisi zetu kutafuta usaidizi. Ukiangalia pia kwenye sehemu zetu za uchuuzi, idadi kubwa ya wachuuzi ni watu ambao hawakuenda shule na hawafahamu Kiingereza. Wakienda sokoni kufanya biashara zao, wengi wao huenda na lugha ya asili kama vile Kikuyu, Kiluo, Kiluyhia na Kinandi. Wakiwa pale sokoni, inakuwa vigumu kufanya biashara kwa sababu hakuna lugha moja ambayo watu wanaweza kutumia kuwasiliana kuhusu mambo ya uchuuzi. Kulingana na mimi, Baraza la Kiswahili likibuniwa na Kiswahili kikiendelea kukuzwa, itakua ni njia moja ya kusaidia mawasiliano kwenye nafasi zetu za kazi. Mimi naunga mkono Hoja hii ya Mhe. Yusuf. Sheng ni lugha ambayo itakuja kunoga hapa Nairobi na huwa inabadilika kila mara. Wakati huu wanaongea hivi lakini baada ya miaka mitano, itakuwa imebadilika kwa kasi kikubwa sana. Kwa mfano, kitambo tulikuwa tunamuita Mhe. Yusuf kule mtaani bazenga lakini siku hizi vijana wanamuita mzimbitim . Hivyo ni vitu viwili ambavyo havieleweki. Lugha ya Sheng inafanya uhusiano kati ya wazazi na watoto wao kuwa mgumu. Hata kama watoto wanapanga mabaya, utakua katika maongezi yao lakini hutaelewa neno hata moja. Ukiangalia pia upande wa utamaduni, wakati tulipokuwa tukienda shuleni, tulikua na ubunifu wa hali ya juu katika sanii na uigizaji. Tulikuwa tunaona michezo mingi ya utamaduni kutoka kule Pwani. Kwa mfano, hivi majuzi kumekuwa na mchezo wa kuigiza uliokuwa ukiendele kwenye runinga, kuhusu Mekatilili wa Menza – ambao ulikuwa na mafunzo mengi sana ya utamaduni wa Mijikenda. Watu wengi walipitwa na utamaduni huu kwa sababu hawaelewi lugha ya Kiswahili. Itakuwa jambo la muhimu sana tukibuni Baraza la Kiswahili ili tuweze kurudisha ubunifu wa kitambo. Hii ni kama vile fasihi na michezo ya kuigiza zilivyokuwa, ili nchi yetu iweze kuendelea mbele vizuri. Kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, nimekuwa mfanyibiashara Tanzania, Uganda, Congo, na kadhalika. Changamoto kubwa imekuwa ni mawasiliano. Mawasiliano kwenye biashara imekuwa ngumu sana kwa maana Kiswahili kinachotumika Uganda na Tanzania ni tofauti sana ni kile cha Congo. Ukiangalia historia, utapata kuwa asili ya Kiswahili ni Kenya. Lakini mataifa jirani yameweza kuchukulia Kiswahili kwa umaarufu mkubwa zaidi. Kwa mfano, hata Rais wa kule Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, wakati wa mazishi ya marehemu Mhe. Magufuli, alisema kuwa ataanzisha somo la Kiswahili katika shule za nchi yake. Lakini upande wetu, Kiswahili hakitiliwi maanani sana ilhali ni lugha ambayo imetupa umaarufu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tukiweza kubuni Baraza la Kiswahili, naamini tutaweza kupata maprofesa kama Ali Mazrui, ambaye alipata umaarufu wake kwa kukuza Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inahifadhi sana mambo ya nidhamu. Inasemekana kuwa ukiongea lugha ya kigeni, unaongea kutoka kwa ubongo lakini ukiongea lugha ya asili unaongea kutoka kwa roho yako. Ndio maana kuna maneno ambayo unaweza kutumia rahisi sana kwa lugha ya Kiingereza lakini maneno hayo huwezi kusema mbele ya watu ukitumia lugha ya Kiswahili. Sitaki kutoa mfano lakini ni rahisi sana kusema kwa Kiingereza yale maneno ambayo tunasema ni wasio wa maadili lakini kwa Kiswahili inakuwa ni vigumu. Hii ni kwa sababu Kiswahili ina nidhamu zake. Ukiangalia pia kwa mitandao ya kijamii, kwa sasa hivi, lugha ya Kiswahili iko hali mahututi. Hii ni kwa sababu kwenye mitandao yote ya kijamii, kama vile WhatsApp, kama alivyosema Mhe. Didimus Barasa, kila mtu anatumia lugha ya Kimombo. Inaweza kuwa vyema Baraza la Kiswahili liweze kuangazia mambo kama hayo ili tuweze kurudisha umaarufu wa Kiswahili. Kwa hayo mengi, Mhe. Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa la Kenya. Naomba kumpa dadangu dakika zilizobaki.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Asante sana.
Mhe. David Ochieng): Mhe. Mwago, hauna dakika za kumpa mtu. Nafasi hii itamwendea Mhe. Mwangale Chiforomodo na atafuatwa na Mhe. Martha Wangari. Iwapo Mhe. Chiforomodo hayupo, nafasi ni ya Mhe. Paul Mwirigi.
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii. Kabla ya kutoa maoni yangu, nachukua fursa hii kuwashukuru wananchi wa Igembe Kusini kwa kunipa nafasi ya pili ya kuwawakilisha. Wengi walidhani kuwa sisi vijana hatuna ubunifu wa kufanya kazi na kuwasaidia wananchi. Wengi walidhani kwamba nitakuwa kiongozi wa muhula mmoja tu na baada ya hapo nitasahaulika. Nawashukuru sana wananchi wa Igembe Kusini kwa kunipa nafasi ya pili ili niweze kuwahudumia. Kama nilivyowaambia, nitawahudumia kwa uaminifu na kutenda kazi zaidi ya vile nilivyofanya katika muhula wa kwanza. Kwa hivyo, nawashukuru sana na naomba Mungu aweze kutupa nguvu kwa miaka hii mitano ili niweze kuwahudumia vyema. Mhe. Spika wa Muda, nampa kongole Mhe. Yusuf kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Unafahamu vyema kuwa lugha ya Kiswahili imedhalilishwa sana katika taifa hili ilhali tunajua kuwa ni lugha ya kitaifa na pia imekubalika katika Katiba yetu kutumika kama lugha rasmi. Kwa hivyo, kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa hili kutachangia pakubwa kuhakikisha kwamba lugha hii imeweza kupata nafasi yake katika taifa hili. Huwa tunasema kila wakati kuwa taifa letu limejengeka katika Kiswahili lakini wakati ambapo tunaenda katika mikutano mikuu, tunaendelea kutumia lugha ya wakoloni bila sisi wenyewe kujielewa kwamba tuko na lugha na utamaduni ambao tunafaa kuhifadhi. Baraza la Kiswahili likibuniwa, litasaidia taifa letu kushiriakiana kwa pamoja na pia kuleta umoja. Wakenya wakizungumza lugha moja na kutupilia mbali lugha za makabila yao, hii lugha itakuwa ni ya kuleta umoja. Wakenya wote tutakuwa kabila moja kwa maana wataunganishwa na hii lugha, itatusaidia pakubwa na itainua na kuimarisha utaifa wetu. Naibu Spika wa Muda, ninampongeza Mhe. Yusuf kwa kuleta hii Hoja Bungeni. Ninaiomba Wizara husika kuangazia na kutilia mkazo suala la kubuniwa kwa baraza lililopendekezwa punde tu Bunge litakapopitisha Hoja hii. Tutakapoipitisha hii Hoja, Serikali iichukulie kwa uzito ili iweze kuwasaidia wananchi. Vilevile, ningeomba sana Wakenya, na haswa taasisi za elimu, watumie lugha ya Kiswahili ili waimarishe utamaduni wetu na pia wanafunzi waweze kuelewa nchi hii imetoka wapi na inaelekea wapi. Wanafunzi wanafaa kuelewa kuwa hii si nchi ya ukabila kwa maana watakuwa wameunganishwa na lugha ya Kiswahili. Kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili ni jambo ambalo limechelewa sana na huu ni wakati mwafaka wa kulitekeleza jambo hili. Baadhi ya Wabunge wenzangu wamesema kuwa tulipokuwa tukiomba kura, tulitumia lugha ya Kiswahili. Tuliwasiliana na wananchi moja kwa moja na walituelewa. Sio vyema basi kila wakati kutumia lugha ya mkoloni, ambayo mwananchi haelewi. Kuna pendekezo kwamba lugha rasmi ya Kiingereza iwe inatumika kutoka Jumatatu mpaka Ijumaa. Ni vyema kuhimiza matumizi ya Kiswahili. Vilevile, Baraza la Kiswahili litakapobuniwa litasaidia mpaka vyombo vya habari. Lugha zinazozungumzwa kwenye vyombo vya habari sio sanifu. Baadhi ya wazungumzaji wanaharibu lugha. Baraza lililopendekezwa litasaidia kuwalazimisha wahusika kwenye vyombo hivyo kusanifisha lugha ya Kiswahili. Baadhi ya Wabunge wamegusia suala la vijana wanavyotumia lugha ya Sheng. Hili baraza litakapobuniwa, tutaweka kanuni mwafaka ili kutoa mwelekeo kuhusu matumizi ya Kiswahili. Hii lugha itajengeka vyema katika taifa hili na itasaidia kukua kwa hili taifa. Kwa hayo mengi, ninaunga mkono.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Waheshimiwa Wabunge, ningependa kuwaeleza kwamba aliye juu kwenye orodha yangu ni Mhe. Martha. Mtu yeyote asiseme nimemkatiza. Alitangulia kufika Bungeni.
Asante Mheshimiwa Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii. Ninampa kongole Mhe. Yusuf Hassan wa Kamukunji kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Nafikiri leo ni mara ya kwanza sisi wenyewe kuendeleza mazungumzo na mjadala karibu kikao kizima cha asubuhi tukitumia lugha hii ambayo tunaienzi. Sisi sote tumeweza kusoma mambo mengi. Tumeona kwamba baadhi yetu tumeshindwa kutumia dakika kumi tulizotengewa kuchangia Hoja hii. Hakuna hata mmoja wetu aliyewashiwa taa nyekundu wakati anapozungumza, kuashiria kumalizika kwa muda wake. Hii ni kwa sababu hatuna uzoefu wa kutumia hii lugha. Tunafaa kuwa kwenye mstari wa mbele kuendeleza na kuonyesha vile lugha ya Kiswahili inafaa kutumika. Mambo na historia ya Kiswahili yanajulikana tangu zamani. Lugha hii imetumika haswa kwenye taifa la Tanzania. Marehemu Mwalimu Julius Nyerere aliweza kutumia Kiswahili sana Tanzania ilipokuwa ikipigania uhuru kupitia chama cha TANU. Hatimaye, UNESCO ilitenga tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa siku ya ya kusherehekea Kiswahili duniani. Idadi ya watu wanaotumia Kiswahili ulimwenguni ni zaidi ya milioni mia mbili. Uzuri ni kwamba hili jambo limeweza kuchukuliwa kuwa la maana sana na UNESCO, ambayo imeidhinisha Kiswahili kitumike kama lugha ya kiasili na utangamano duniani. Hapa Kenya, tumeweza kuwa na utangamano wa jamii tofauti. Tumewahimiza watu kutoka jamii tofauti hata waweze kuoana na tumepoteza lugha zetu za kiasili. Lugha ambayo imebaki ni Kiswahili – ambayo inatuunganisha sisi sote. Baadhi ya Wabunge wenzangu waliotangulia kuchangia Hoja hii, wamesema kwamba wakati tulipokuwa tunapiga siasa muda usiokuwa mrefu, hatukuwa tunatumia sana lugha ya Kizungu. Tulitumia Kiswahili. Wakati unahudhuria mchanganyiko wa jamii nyingi unafaa kutumia lugha ya kiasili. Kwa mfano, ukihudhuria mkutano wa Wakikuyu, unafaa uongee Kikuyu. Unapohudhuria mkutano wa Wajaluo, unaongea Dholuo ama Kijaluo. Lakini unapokwenda kwenye mkutano unaohudhuriwa na mchanganyiko wa jamii tofauti, kama vile Wakisii, Wajaluo na Wakalenjin, itabidi utumie Kiswahili ndiyo muweze kuongeleshana na kusikilizana. Hapa Bungeni, tumeonyesha kuwa hii lugha inawezakutumika. Pia, tumeitumia lugha katika Kanuni za Kudumu za Bunge ama National Assembly Standing Orders . Nchini Tanzania, majina ya taasisi za umma na wizara za serikali yamenukuliwa kwa Kiswahili kwenya majengo ya serikali. Utaona jina la maabara ya sayansi limechapishwa kwa Kiswahili kwanza na kuwekwa kwa Kiingereza kwenye mabano. Hapa kwetu, hatuweki jina la taasisi ama wizara kwa Kiswahili hata kwenye mabano. Tunachapisha tu kwa Kizungu bila Kiswahili. Tunafaa kuwa kwenye mstari wa mbele kuonyesha kuwa inawezekana kutumia Kiswahili kama lugha rasmi. Tunafaa kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatumika katika jamii. Tunapaswa tuwafunze watoto wetu pia. Haswa, sisi ambao ni wazazi wa watoto wachanga wanaopitia mfumo wa elimu wa CBC, ni jukumu letu kwenda shuleni kuona kwamba watoto wanafunzwa lugha ya Kiswahili. Tukishazaa watoto, kabla wafikishe umri wa kisheria wa kuenda shuleni, inafaa wawe wanapata mafunzo ya Kiswahili. Tunafaa kutumia Kiswahili katika jamii zetu kwa sababu lugha usiokuwa na uzoefu wa kuizungumza itapotea kwa sababu haitumiki. Kwa hivyo, ni jukumu letu kama wazazi kuhakikisha kwamba tunaitumia vizuri na tunawafunza watoto wetu ndio wakienda shuleni waweze kuendeleza mazungumzo na lugha zingine. Uzuri wa watoto ni wanaweza kujifunza lugha haraka. Hata ukizaa mtoto Uchina na umlete Kenya leo, atafunzwa Kiswahili na atashika kutoka mwanzo wake. Kwa hivyo, ni jukumu letu tuanze pale mwanzo. Tuko na wakati mzuri sasa kwa maana tuko na Baraza jipya la Mawaziri.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Mhe. Spika wa Muda, kama kuna jukumu moja muhimu ambalo Waziri aliyetwikwa jukumu hilo ako nalo saa hii, ni jukumu la kukuza Kiswahili humu nchini. Hivi sasa kuna jopo linalozunguka nchini kupokea maoni kutoka kwa washikadau kuhusu mfumo wa elimu wa CBC. Wakati utakapofika wa kuupiga msasa mtaala huu, tunafaa kuhakikisha kwamba lugha ya Kiswahili imechukua nafasi yake katika mpango wote wa elimu ya watoto wetu kuanzia PP1, ama gredi ya kwanza, ama elimu chekechea ndiyo mtoto akifika kiwango cha elimu ya juu awe ameifahamu vizuri lugha ya Kiswahili ndiyo hata akibahatika kuja Bungeni kama wanafunzi ambao wanatutembelea hapa, na kutazama mijadala, ajue kwamba Kiswahili ambacho watafunzwa pale mwanzo kwenye elimu chekechea, kwenye shule ya upili na hata kwenye chuo kikuu, ni kilekile Kiswahili ambacho kitatumika Bungeni.
Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, namuunga mkono Mhe. Yusuf na kumuhimiza kwamba asikomee hapa. Kwa sababu, kutokana na historia ya Bunge – mimi na wewe tumekuwa kwenye Mabunge ya 11 na 12, na sasa tuko katika Bunge la 13 – mengi ya maazimio tunayopitisha kupitia Miswada yanakwama wakati wa utekelezaji. Unabaki ukiyafuatilia kwenye Kamati ya Utekelezaji. Kwa hivyo, ninamhimiza Mhe. Yusuf kwamba ahakikishe kwamba pendekezo limeendelezwa hadi kuwa Mswada ili aulete Bungeni tuupitishe uwe sheria ndiyo suala hili liweze kupata uzito linalostahili na kutengewa bajeti kuhakikisha kwamba lengo letu limetimia. Hatuwezi kuwa tunasema tuko kwenye Umoja wa Afrika Mashariki bila ya kutekeleza maazimio ya umoja huo. Ukiaangalia Umoja wa nchi za Afrika, (AU) na UNESCO wameweza kukitambua Kiswahili. Lakini sisi wenyewe hatujaweza kubuni sheria ya kuliwesha jambo litendeke. Namhimiza Mhe. Yusuf kwamba, wakati hii Hoja itapitishwa katika na Bunge hili, asikwame hapo; angalie ni vipi tunawezakuendeleza mpaka iweze kuwa sheria ya nchi hii ndiyo tuwe kwenye msitari wa mbele kuhakikisha kwamba swala la kukikuza Kiswahili limewezekana. Mhe. Spka wa Muda, pia sisi, kama Wabunge, tujue kwamba tunapozungumza kuhusu usanifu wa lugha ( grammar) kama alivyosema Mheshimiwa mmoja, tunapaswa kuzingatia kanuni zote za lugha.
(Mhe. David Ochieng’
Ninaifuata, Mhe. Spika wa Muda. Ndiyo maana ninaweka baadhi ya maneno kwenye mabano; haswa maneno ambayo ninayatoa kwenye lugha ya Kimombo. Nataka kusema kwamba tujihimize sisi wenyewe kama Wabunge, tuitumie hii lugha, sio hapa tu kwenye Bunge, lakini hata kwa nyumba zetu na kwa jamii zetu ili tuweze kupata uzoefu wa ulimi. Hii ni kwa sababu hata miongoni mwetu sisi Bunge, kuna wanaosema kwamba huu Mswada haueleweki vizuri. Hawajazowea mambo ya Kiswahili. Tukiendelea kuzungumza Kiswahili, tutapata uzoefu wa kuzungumza na hatimaye hata wanaotutazama, wakiwemo watoto, wajue kwamba Kiswahili ni lugha yetu sisi sote, na inatumika nchini kwote, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na vile vile katika Afrika nzima. Kwa hayo mengi, ninaiunga mkono Hoja hii.
Sasa twendeni Pwani, tumpate Bwana Bady Twalib kutoka Jomvu.
Jomvu, ODM
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
BAKIZA. Tukiangalia katika kifungu cha saba cha Katiba ya Kenya, lugha mbili – Kizungu na Kiswahili – ndizo lugha rasmi humu nchini. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, pendekezo hili la kubuniwa kwa Baraza la Kitaifa, kama alivyosema mwenzangu, Mhe. Martha, lisiwe Hoja pekee bali lifuatiliwe mpaka tubuni sheria kamili, na tuhakikishe kwamba Baraza hilo limetengewa bajeti yake. Vile vile, katika Bunge hili la 13, tusifanye mambo ya kawaida kama tulivyokuwa tukifanya katika Mabunge ya 12 na 11. Katika Mabunge yaliyopita, Hoja zinapitishwa lakini kutekelezwa inakuwa shida. Kwa hivyo, wakati huu ni muhimu Kamati ya Utekelezaji ( Committee on Implementation) ihakikishe kwamba masuala yote yatakayopitishwa hapa yanatekelezwa. Mhe. Spika awa Muda, jambo hili la Kiswahili ni jambo ambalo litaweza kuunganisha Afrika Mashariki nzima. Tukiangalia nchini Tanzania, wanaongea Kiswahili. Waganda pia wanaongea Kiswahili. Na njia hii ya Kiswahili ndio itafanya iwe rahisi kwa watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya biashara na kuleta undugu. Tunajua kwamba hivi karibuni ndugu zetu wa kule Congo pia wamejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukiangalia Congo pia, watu wanazungumza Kiswahili. Ijapokuwa Kiswahili cha kule, kidogo ni tofauti na Kiswahili chetu. Kwa mfano, utamsikia Mkongo akisema, “Mimi nikiwa Papa Fulungenge, nasema kuwa batoto ba Congo na batoto ba Kenya, bote ni batoto bamoja. ” Hivyo ndivyo Wakongo wanavyozungumza. Sote basi ni watu wamoja, Wakenya na vile vile Wakongo. Mhe. Spika wa Muda, kubuniwa kwa baraza hili la kitaifa kutaweza kufanya biashara na mawasiliano kuwa rahisi katika nchi hizi zetu. Tunaona katika Vifungu cha 119 na 137, vya Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vimewajibisha mataifa wanachama kustawisha na kuendeleza Kiswahili kama lugha ya mshikamano wa nchi wanachama. Kwa hivyo, Mheshimiwa, ukiangalia jambo kama hili limeweza kueneza ubora wa kuinua Kiswahili. Miongoni mwa jamii za Afrika Mashariki kuna lahaja mbali mbali za Kiswahili, ikiwemo Kijomvu, lakini hakuna Wajomvu. Mhe. Spika wa Muda, naona wafurahi, wacheka lakini wako Wajomvu. Mimi najifuharisha na nafurahi kuwa ni mmoja wa hao Wajomvu. Leo hii, utamuona Mswahili wa Kijomvu akitaka kutoa mfano wa watoto wawili ambao wanacheza na kwa bahati mbaya mmoja anamchoma kisu kwa jicho mwingine. Mjomvu husema, “Huyu mwana mkunzu unamtopoa,” yaani maana yake ni kuwa huyu ameweza kumkwaza mwingine kwenye jicho. Na vile vile, wakiogelea baharini, utawaskia wakisema, “Mwana huyu anaoga kutoka uta tauta katika pwani hii.” Kwa haya yote twajivunia kwa sababu hii ni lugha yetu. Na leo Kijomvu nakizungumza katika Bunge la Kenya. Kwa hivyo, ninafurahi kuwa Kijomvu ni moja ya lahaja za Kiswahili. Na punde, kama alivyosema… Ndipo ukaona Mhe. Martha akizungumza Kiswahili kidogo. Nilijua ni yeye kwa sababu uswahili ulikuwa umemnogea mpaka nikaona nikama ambaye anatoka Pwani. Ukienda Dar-es-Salaam, utapata kwamba katika maeneo mengi sana, hata kama kunawekwa mabango yoyote pale, utapata yanaandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Wanajivunia lugha yao ya Kiswahili. Mawasiliano mazuri yatainua biashara na ajira Afrika Mashariki. Hii ni kwa sababu ni Baraza zima ambalo linahitaji huduma kwa watu kulishughulikia. Nampongeza sana Mhe. Yussuf Hassan kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili.
Nitakuambia mambo ya maajabu. Kati ya makabila madogo madogo 12 kule Mombasa, kuna makabila madogo ambayo kwa kimombo tunayaita minority tribes . Hayajulikani. Nataka kutaja katika kumbukumbu kwa kumpongeza kamishna mmoja wa polisi anayeitwa Murshid. Wakati uajiri wa polisi ulipofanyika katika sehemu yangu mwaka wa 2014, kuna mtoto mmoja wa Jomvu alitolewa kwa hesabu kwa sababu kabila yake haikuwa inajulikana. Nilipiga kelele kama Mbunge na nikafikisha barua kwa kamishna wa wakati ule. Ilidhibitika kuwa hiyo ndiyo moja katika kabila yenyeji ambayo inaishi sehemu hizo. Huyo mtoto alichukuliwa kama polisi. Leo hii anahudumia kitengo cha Kenya Police. Ni mtoto wa Mzee Salim.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Ni pongezi kwa Mhe. Yussuf Hassan kwa kuleta jambo njema. Sisi tunaotoka Pwani, ikiwa tumekuwa tukipata usingizi tukiwa tumejifunika blanketi nusu, leo tutajifunika blanketi nzima tukijua Kiswahili kinakombolewa nchini Kenya. Ahsante na Mwenyezi Mungu akubariki.
Vyema. Tuende kule Bonde la Ufa tumskize Bwana Francis Sigei kutoka Sotik, alafu atakayefuata ni Mhe. Lydia kutoka Taita Taveta.
Mhe. Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii kuchangia hii Hoja ya maana. Pia ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani kwa watu wangu wa Sotik walioona ni heri kunipatia fursa ya kuwahudumia. Nawapongeza. Baada ya kuwania hiki kiti mara tano, watu wa Sotik waliweza kunipa fursa hii. Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi hii ya kuwahudumia wao. Leo ni siku ya maana sana kwangu kama mwakilishi wa Sotik kwa kuweza kuzungumza na Wakenya.
Nikichangia huu mjadala, kwanza natoa shukrani za kipekee kwa Mhe. Yussuf Hassan. Najua yeye ni mkongwe. Ni mtu ambaye amefanya kazi nchini. Namtambua na nampa heshima. Namwona kama shujaa nchini kwa sababu ametetea tamaduni zetu. Mhe. Yussuf, tunakupongeza sana na Mungu akubariki.
Kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika nchi hii ni jambo la maana sana. Ningependa kuchukua hii nafasi kushukuru muanzilishi wa Taifa la Tanzania, Marehemu Nyerere, kwa kufanya jambo la maana sana. Alivyoanzisha utumizi wa lugha ya Kiswahili kwa nchi hiyo, alihakikisha wananchi wanaongea hiyo lugha. Tunajua kwamba umoja wa Tanzania ni dhabiti. Kuna Wakenya ambao wamechangia katika ubunifu wa lugha ya Kiswahili, mmoja wao akiwa marehemu Ali Mazrui aliyeandika vitabu. Pongezi kwake. Tungependa kuwa na watu kama hao. Jambo la maana kwa Baraza la Kiswahili ni kutoa mwelekezo, mikakati na namna ya kutumia lugha hii. Tungependa kulipatia nafasi hili kupanga hayo mambo. Tukipata baraza la Kiswahili, tutaweza kupata mwelekeo wa lugha ya Kiswahili. Naomba tushukuru wananchi wa Kenya. Wengi wanasubiri hii lugha iwe lugha ya taifa. Shida tuliyonayo ni mwelekeo na namna ya kutumia lugha sanifu. Lugha tunayoijua ni sheng . Mhe. Yussuf, tungependa uchukue hatua nyingine ili ulete Mswada. Lugha inayotumika mahakamani ni Kiingereza. Najua kwamba wanaohukumiwa wanahukumiwa bila kujua lugha iliyotumika. Wanaambiwa waaende jelani au wamepigwa faini halafu wakili wake anamueleza yaliyojiri. Inafaa tuanze kuchukua nafasi hii kama Serikali tuone kwamba lugha ya Kiswahili inatumika. Hata Kanuni za Kudumu tunafaa kuzitumia zile za lugha ya Kiswahili.
Mhe. Sigei, Kanuni za Bunge tayari ziko kwa lugha ya Kiswahili.
Hatuzitumii. Ningependa lugha ya Kiswahili itumike siku moja kwa wiki katika hili Bungeni. Naunga mkono Hoja hii. Napongeza mashirika kama BBC na Sauti ya Marekani kwa kutusaida sana kwa kuendeleza lugha ya Kiswahili. Nakushukuru, Mhe. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hi ya Mhe. Hassan.
Ahsante sana. Vyema. Tulisema kwamba nafasi hii ni ya Mhe. Haika.
Mhe. Spika wa Muda, nachukua fursa hii kukushukuru kwa kunipatia fursa ya kuzungumza. Nimekuwa nikisubiri kwa muda ili nipate fursa hii hata mimi niweze kuchangia. Namshukuru Mwenyezi Mungu ya kwamba leo imefika. Pia nachukua fursa hii kuwashukuru watu wangu wa Taita Taveta kwa kunipatia kipindi cha pili ili niweze kuwatumikia kama kiongozi wao tena. Nawashukuru sana na nawambia kazi ile njema tulioweza kufanya, tutaifanya tena na zaidi. Nikirudi katika Hoja yetu ya leo, kwanza nampongeza sana Mhe. Yusuf Hassan kwa kuileta. Hoja hii ni bora sana na inasisitisa kuundwa kwa Baraza la Lugha ya Kiswahili. Kiswahili jamani kitukuzwe. Kiswahili ni lugha nzuri na imetambulika katika nchi yetu ya
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Kenya kama lugha ya Taifa. Kiswahili kama lugha ya Taifa katika nchi yetu ya Kenya haijatiliwa maanani. Hakijaheshimiwa kulingana na vile kimetambuliwa kama lugha ya Taifa. Kukibuniwa Baraza hili, basi, litaweka mikakati dhabiti ambayo itasababisha lugha hii yetu ya Kenya iweze kupendwa; iweze kuwa na watu wengi ambao wanaienzi na watu wanaojivunia lugha ya Kiswahili. Kiswahili ni lugha ambayo inaweza pia kutumika kuunganisha Wakenya. Tunajua vyema ya kwamba yako makabila mbalimbali lakini kuna jambo moja ambalo linaweza kutuunganisha. Lugha ni mojawapo ya mambo ambayo yanaweza kuunganisha watu. Lugha ya Kiswahili inaweza kutuunganisha. Na sio Kenya pekee yake bali Africa nzima. Hata Africa Mashariki tunaweza kuunganishwa na lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, naunga mkono Hoja hii nikisema ni wakati wa usawa. Ya kwamba huu mpango mzima wa kubuni hili Baraza uweze kufanyika ili lugha hii iweze kutukuzwa katika Kenya nzima. Namshauri pia Mhe. Yusuf Hassan kwa kumueleza, baada ya hapa, tumekuwa tukizungumza hapa Bungeni na mara nyingi yanaishia hapa. Basi ni wakati tuweze kuenda hatua nyingine tena baada ya hapa tufuatilia yale tunayoyanena hapa tuyatende. Tuhakikishe kwamba lugha ya Kiswahili inazungumzwa na watu wanajivunia. Kuwe na mikakati bora na watu waweze kujifunza ili tuweze kuimarisha Kiswahili na kiwe bora katika nchi yetu na tuweze kuwa na Kiswahili cha kutuunganisha kama Wakenya.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa fursa hii na ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Pongezi kwa mheshimiwa aliyeleta Hoja hii. Ahsanteni sana.
(Mhe. (Dr.) Rachael Nyamai): Ahsante Mbunge wa Taita Taveta. Anayefuata ni Mbunge wa Ganze ambaye ni Charo Kazungu.
Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nitoe maoni yangu kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili hapa nchini Kenya. Pia nachukua fursa hii kumpongeza Mbunge wa Kamukunji, Mhe. Yusuf Hassan, kwa kuleta Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili hapa nchini Kenya. Kama vile wenzangu wametangulia kusema, ni kweli kabisa kuwa Kiswahili ni lugha ambayo inadhaminiwa sana hapa Kenya na watu wengi. Ni lugha ambayo inatumiwa na makabila karibu yote hapa Kenya. Sio Kenya pekee yake, lakini ukiangulia ukanda wote wa Africa Mashariki, ukanda wote wa Maziwa Makuu na Afrika nzima kwa jumla, sasa wamekubali lugha ya Kiswahili na wameanza masomo mbalimbali katika nchi zao kuhakikisha kuwa lugha inabobea katika nchi hizo. Lakini la kushangaza hapa nchini Kenya bado tunachukulia lugha ya Kiswahili kama lugha dhaifu kwa sababu wengi wanafikiria mtu akiongea Kiswahili huwa hajasoma vizuri ama ana elimu duni. Wananchi wa Kenya huwa wanashabikia Kiingereza sana kuliko hii lugha yao ambayo imetambuliwa na Katiba ya Kenya kama lugha ya Kitaifa. Pale Pwani ninakotoka, lugha ya Kiswahili inakejeliwa sana, hata ukiangalia kwenye mitihani ya Kitaifa ya Darasa la Nane na Kidato cha Nne. Ukiangalia vile wanafunzi wanavyofanya mitihani yao ya lugha ya Kiswahili, utapata hawapati alama nyingi sana ijapokuwa inasemekana wazi kwamba Pwani wanaongea Kiswahili. Lakini hali hii haionekani katika ile mitihani ya Kitaifa. Utapata wanaopita vizuri mtihani ya Kiswahili huwa ni shule za kutoka sehemu ya Bara wala siyo sehemu ya Pwani. Hili ni jambo ambalo ni lazima kama viongozi tulitilie maanani na ndio maana nasimama hapa kuunga mkono Hoja ya Mhe. Yusuf Hassan ya kusema ni lazima tubuni
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Baraza la Kitaifa ili tuweze kuhamasisha Wakenya tukijumuisha hata Wapwani ili waweze kuongea hii lugha na waweze kuisanifisha na kuongea kama vile ndugu zetu kule Tanzania tunawaona wakiongea. Hii lugha tukitumia vizuri inaweza kuunganisha Kenya. Tuna makabila zaidi ya 45 na kila kabila lina lugha yake. Tanzania wana makabila zaidi ya 50 lakini sio rahisi kujua Mtanzania ni wa kabila gani kwa sababu wote wameunganishwa na lugha ya Kiswahili. Naomba kama inawezekana, Baraza la Kitaifa hapa nchini liundwe ili liweze kuleta Wakenya wote pamoja ili waweze kusahau makabila yao, waweze kuwa na lugha moja ambayo itawaunganisha wote kama Wakenya. Mhe. Spika wa Muda, lugha ya Kiswahili haiongewi hapa Kenya pekee yake. Kama nilivyosema, hata Bara ya Ulaya na Uchina wanatumia Kiswahili. China wameandika walimu wengi wa Kiswahili wanaowafunza wananchi wao jinsi ya kuongea Kiswahili. Ukienda kule Marekani pia, utaona walimu wengi wa Kiswahili wamepelekwa huko. Wanafunza Wamarekani jinsi ya kuongea Kiswahili. Utaona kuna wasanii waliobobea Wamarekani ambao wameimba nyimbo kwa lugha ya Kiswahili. Msanii kama Michael Jackson aliwahi kuimba nyimbo kwa lugha ya Kiswahili. Msanii kama Lionel Richie pia aliimba wimbo katika lugha ya Kiswahili na hao ni Wamarekani. Msanii Rihana ameimba nyimbo katika lugha ya Kiswahili. Lakini hapa Kenya, sisi wenyewe tunadhalilisha lugha ya Kiswahili. Watu wanatoka nchi za mbali kuja Kenya kusoma lugha ya Kiswahili. Kuna wanafilamu waliobobea kutoka Marekani pia kama vile akina Forest Whitaker walikuja hapa Afrika, Uganda, wakasoma Kiswahili na wakatengeneza filamu kama vile The Last King of Scotland . Ni Wamarekani lakini wanaongea lugha ya Kiswahili na wanaongea Kiswahili sanifu. Kwa hivyo, mimi naunga mkono Hoja hii ya Mhe. Yusuf Hassan ya kuwa hapa Kenya pia tubuni Baraza la Kiswahili ili tuweze kuhakikisha Wakenya wanaongea lugha sanifu. Hapa Nairobi najua kuna shida kubwa sana kwa sababu wanaingiza sheng kwa Kiswahili kila wakati. Wenyewe wanasema ni Kiswahili lakini mtu ambaye anatoka Pwani akisikia vile wanaongea pengine hataelewa hata neno moja ambalo linaongewa pale. Kiswahili kinaunganisha wananchi na kinaleta identity na uniformity. Hii itawezekena kama kutakuwa na baraza rasmi ambalo litakuwa linahakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inapewa kipaumbele. Inahitajika ili iweze kuwa lugha nzuri. Na sio lugha rasmi pekee yake, lakini pia iwe lugha nzuri ambayo inakubalika kila pembe zote za Kenya. Kwa hayo machache, ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Nazidi kupongeza hatua ya Mhe. Yusuf Hassan kwa kuhakikisha kuwa Baraza la Kitaifa ya Kiswahili litabuniwa hapa nchini Kenya. Ahsanteni sana.
(Mhe. (Dr.) Racheal Nyamai): Mbunge wa Saboti, Caleb Luyai.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi mwafaka ya kujadili Hoja hii. Nampongeza rafiki yangu, Mhe. Yusuf Hassan, kwa kuwa na hekima ya kuleta Hoja kama hii. Lugha ya Kiswahili na lugha ya Kimombo zimeorodheshwa kama lugha rasmi za kitaifa katika Katiba yetu ya Kenya. Lakini miaka kumi na miwili imeisha na hatujaweza kuitafsiri Katiba hiyo ikawa katika lugha ya Kiswahili vile ilivyo katika lugha Kimombo. Hicho ni kinaya - kwamba tumeiweka lugha ya Kiswahili kipao mbele katika Katiba ilhali hatujapata nafasi ya kutafsiri Katiba ya Kenya katika lugha ya Kiswahili. Nikikumbuka wale ambao wako na umri kama huu wangu ambao wametoka shule hivi majuzi, kuna vile vitabu tumesoma. Kuna wale ambao walibobea katika lugha ya Kiswahili na wakawa mstari wa mbele kukuza Kiswahili. Mfano ni yule aliyekuwa anatambulika, marehemu Ken Walibora. Wale wanakumbuka Ken Walibora - Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - alikua mstari wa mbele kuikuza lugha ya Kiswahili. Tulimpoteza na hakuna mahali tunamkumbuka. Ni vizuri tungekuwa tunawakumbuka watu kama hao ambao wamekuwa
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
mstari wa mbele. Wale wanaokumbuka kitabu cha Siku Njema, siku njema itakuja lini? Ni kitabu ambacho kilisifika sana kwa wale walikuwa kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule za upili. Ni kitabu ambacho kilibuniwa na kupaliliwa katika masomo na hata mtihani wa kidato cha nne. Unakumbuka pia tulikuwa na Wala bin Wala na yule aliandika kitabo cha wale ni sisi na sisi ni wale. Yaani Walenisi . Wanaokikumbuka hicho kitabu, kilikuwa na hekaya na riwaya ambayo ukiisoma unapata kusisimka na inasisimua akili yako. Kimeandikwa kwa njia ya kukejeli lakini kina mafunzo. Wale wanakumbuka hivi vitabu, vilitufunza mambo mengi tukiwa katika shule za upili na tulitahiniwa. Unakumbuka kulikuwa na wanafunzi wanapenda kusoma hivi vitabu na kufurahia. Lakini tukishamaliza mtihani, huo ndio ulikuwa mwisho wa Kiswahili. Hatuendelei kukuza lugha ya Kiswahili ili tuweze kuiweka mbele kama lugha ya kitaifa. Pia kuna kitabu ambacho kilijulikana kama Kitumbua Kimeingia Mchanga. Ni kitabu ambacho kilisifika sana. Hatujawahi kuwasifu wale wameandika vitabu hivi. Hatujawaweka mstari wa mbele. Tunaongea kuhusu kubuni Baraza la Kiswahili la Kenya. Tungewaweka hao katika Baraza hilo ama kitengo cha kushughulikia maswala ya Kiswahili, na hivi tungeiweka Kiswahili mahali panapofaa.
Mhe. Spika wa Muda, leo asubuhi nimekuwa na mkutano na raia wa Uingereza. Ingekuwa jambo kubwa kwamba huwezi kupata Mkenya akisema anasomea somo la Kiswahili. Lakini inanishangaza kwamba huyu Muingereza amekuja hapa hivi maajuzi, hajamalizia hata mwezi mmoja, lakini anakwambia: “Niko katika somo la Kiswahili. Najifunza lugha ya Kiswahili”. Itakuwaje kwamba wale wa nchi za ughaibuni wanatamani sana lugha yetu? Wanapofika hapa, jambo la kwanza wanalokuambia ni ‘naam’ na ‘ahsante’, kwa kuwa wameshajifunza. Wanajua kwamba ukifika Kenya, hata balozi anapotumwa Kenya, salamu za huko ni ‘ahsante’. Wameshajua kwamba Kenya na Kiswahili ni moja. Lakini sisi hapa hatuitambui lugha hii ila nchi nyingine zinaitambua lugha ya Kiswahili. Wao wana hamu sana ya kuisoma na kuingia shuleni wakitaka kufahamu hii lugha kwa undani. Hiki ni kinaya kikubwa sana. Pia, twafaa kuweka vyuo vikuu viwe na vitengo mwafaka vya Kiswahili ili wanafunzi wanapojifunza lugha ya Kiswahili, wajue mwishowe watapata kazi. Watasema tulikua tunaimba: ‘Someni vijana, mwisho wa kusoma mtapata kazi nzuri sana.’ Lakini sasa watu hawajui ikiwa watapata kazi baada ya kusoma. Watu wanajua baada ya kusoma ni giza na hakuna kazi. Sasa inafaa tujue kwamba tukiviweka vyuo vikuu vya kusomesha Kiswahili, wanafunzi watajua wakisoma somo hili la Kiswahili wataingia chuo kikuu na watakua walimu wa lugha ya Kiswahili. Chambilecho wahenga: Cha mkufuu mwanafuu ha, na akila hu; cha mwanafuu mkufuu hu, na akila ha. Ahsante sana.
(Mhe. (Dkt) Racheal Nyamai): Ahsante sana Mheshimiwa. Nafasi inayofuata ni ya Mheshimiwa wa Turbo ambaye ni Mhe. Janet Sitienei.
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nichangie Hoja hii. Kwanza kabisa napenda kumpa kongole Mheshimiwa wa Kamukunji kwa kuleta Hoja hii. Hakika, katika karne ya ishirini na moja, ni bora kutukuza lugha ya Kiswahili ili itumike sehemu zote nchini. Pia, sisi kama Wabunge twafaa tuwe na uzoefu wa kutumia lugha hii ya Kiswahili katika mijadala yetu. Hii ni ili wenye-nchi wetu - wakiwemo wazee, akina mama, vijana, pamoja na watoto - waweze kuelewa ni nini kinachoendelea bungeni. Nikitambua Kifungu cha Saba cha Katiba ya Kenya kinabainishia Serikali kulinda, kuendeleza ama kukuza matumizi ya Kiswahili, ningependa kuunga mkono Hoja hii ili iboreshwe kwa manufaa ya sisi wananchi wa Kenya.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Mkutano wa mwaka wa 2021 wa Marais wa Umoja wa Afrika Mashariki walikubaliana kubuni tume ya baraza la Kiswahili. Basi hatuna budi kuunga mkono kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya kwa sababu hii itarahisisha wananchi kupata mawasiliano kamili. Pia itaboresha kufuzu kwa wanafunzi wetu wa kidato cha nne na kuingia chuo kikuu. Katika baadhi ya mahitaji ama masomo yanayohitajika kuingia chuo kikuu, wanaangalia sana lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa muda, kubuniwa kwa baraza hili kutasaidia zaidi. Nakumbuka wakati mmoja nilipigia mkaaji wa Mombasa simu. Nilipopiga simu, aliniuliza: “Ni nani mwenzangu?” Sikuelewa anamaanisha nini. Nilishinda nikimuambia: “Hapana! Mimi ni Janet!” Naye ananiuliza: “Ni nani mwenzangu?” Sikuelewa alimaanisha “ni nani anaongea”. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuweza kukuza lugha ya Kiswahili ili isaidie watu wengi. Itaboresha hata wanabiashara katika nchi ya Kenya. Kuna asilimia kubwa ya wanabiashara ambao hawawezi kuelewa ama kuzungumza lugha ya Kiingereza. Kwa hivyo kubuniwa kwa baraza hili itawawezesha kuweka mikakati bora ambayo itawasaidia wananchi wengi na kuwasaidia wafanyabiashara katika mawasiliano yao. Hivyo, uchumi wetu utakuzwa kupitia mawasiliano bora. Kubuniwa kwa baraza hilo kutachangia uhusiano, kuungana pamoja na mawasiliano bora kwa wenyeji wa Afrika Mashariki. Nasimama hapa kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa hapa Bungeni na mwenzangu Mhe. Yusuf, Mbunge wa Kamukunji.
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi nichangie.
(Mhe. (Dkt.) Rachael Nyamai): Ahsante sana. Anayefuata ni Mhe. Nabwera Nabii, Mbunge wa Lugari. Alafu Mbunge wa Tigania Mashariki, Mhe. Mpuru Aburi. Inaonekana Mhe. Nabii ametoka kidogo. Kwa hivyo, tutaenda moja kwa moja kwa Mhe. Mpuru Aburi, Mbunge wa Tigani Mashariki.
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kiswahili ni lugha ya maana sana kwa Wakenya wenzangu. Kwa sababu, ukiangalia kule mashinani, wakati tunakimbia huku na kule kuomba kura, hatutumii Kiingereza. Tunatumia Kiswahili. Siku hizi, hapa nchini Kenya, kila mtu ana runinga ndani ya nyumba yake. Lakini kule mashinani wanaoelewa Kiingereza ni wachache. Hata wenye pikipiki wakiwa na simu zao mkokoni husikiliza stesheni ya Bunge. Wabunge walikimbia huku na kule kuomba kura lakini hapa Bungeni, tunazungumza Kiingereza tu. Tukienda kunywa chai pale nje, hakuna yeyote anayeongea Kiingereza. Ni Kiswahili peke yake. Ndiyo maana naunga mkono ndugu yangu Bw. Hassan, kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Hii ni kwa sababu hakuna njia nyingine ya kuunganisha Wakenya ama mtu aliyesoma na yule hakusoma ila ni kupitia Kiswahili tu.
Tukiangalia mambo ya mashamba, maofisa kutoka Wizara ya Lands yani makarani, huenda mashinani kushugulikia mambo ya mashamba. Wakifika huko, wanaongea Kiingereza tu hata katika kesi zote za mashamba. Mzee na mama hawaelewi; wanatingisha vichwa tu. Kumbe hapo wanakuliwa na hao makarani. Ndiyo nasema Kiswahili ni lugha ya maana sana. Ukiangalia wenzetu Watanzania, wanazungumza Kiswahili na kimewaunganisha wote. Mtanzania hajali kabila lake ni gani. Yeye anajua ni Mswahili na hawezi kuzungumza lugha nyingine ila Kiswahili tu.
Lakini hapa nchini Kenya, ukienda kwenye ofisi za Serikali, unawapata watu wanazungumza Kiingereza. Hakuna lugha nyingine. Hata mtu akiwa anataka kuwaeleza kitu cha maana anashindwa, au kuskia aibu kwa sababu hatasikilizwa. Ukienda kortini au kwenye magereza kwa mfano Kamiti ama rumande huko Industrial Area, asilimia 80 ya wafungwa ni watu hawana makosa yoyote. Wakifika kortini, jaji, wakili na prosecutor wanazungumza Kiingereza. Sasa huyo jamaa anapanua mdomo tu mpaka anapelekwa ndani.
Ndiyo maana naunga mkono Hoja hii ambayo itatupatanisha. Chama chetu cha National
(NOPEU), ni cha mwananchi wa kawaida. Sisi kama viongozi wa chama hiki lazima tuunge mkono Hoja hii ndiyo mwananchi wa kawaida aweze
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
kuinuka. Ni yule ambaye amekaliwa ama kufinyiliwa na wakoloni Waafrika wanaosema wanaelewa Kiingereza tu. Wakati umefika tupendane, tusikizane ili tuwe kitu kimoja kama Wakenya.
Naunga Rais wetu mkono, kwa sababu wakati mwingine anaongea Kiingereza na akimalizia yale yote ameongea, anatafsiri kwa Kiswahili ndio mwananchi wa kawaida ambaye ni mzalendo na yule hustler aliyempigia kura afahamu alichosema. Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Mimi hula miraa siku ya Ijumaa na nikila ‘ veve’ zangu, tunaongea Kiswahili pale nyumbani na wenzangu. Hata saa hii tunapoongea, wale wanaokula miraa kule Meru na Mombasa…
Hoja ya nidhamu, Mhe. Spika wa Muda.
(Mhe. (Dkt.) Dr. Rachael Nyamai): Mhe. kuna hoja ya nidhamu kutoka kwa Mhe. Ndindi Nyoro.
Mhe. Spika wa Muda, niko na hoja ya nidhamu. Hii ni kwa sababu katika sheria za Bunge ama Kanuni za Kudumu hufai kuchanganya lugha. Nimemskia Mhe. akiendelea kukuita Madam na kusema for example . Kuchanganya lugha ndio ningetaka... Hii ni kwa sababu, siku ya leo wanafunzi wengi wamefika hapa kututazama. Ni vizuri wakirudi shuleni wajue kuna nidhamu inayofaa ndani ya hili Bunge.
(Tigania East,NOPEU
(Mhe. (Dkt.) Rachael Nyamai): Mhe. hakikisha unatumia lugha moja, halafu usirudie veve .
Ahsante Mhe. Naibu Spika. Mhe. Ndindi ni ndugu yangu mdogo mpendwa. Anajua wakati alipokuwa ameenda na maji kule, sikuruhusu abebwe na maji. Kwa hivyo, yeye hana maneno ya maana na si lazima aongee. Langu ni moja tu, kwamba naunga mkono Hoja hii ndiyo Kiswahili kienee hapa nchini na Wakenya wainuke. Nasema ahsante kwa watu wa Tigania Mashariki kwa kunipigia kura na kufanikisha kuja kwangu hapa Bungeni.
Pia nasema ahsante kwa ndugu zangu waliokuwa katika Bunge lililopita kwa kunipigia kura ndiyo nikaenda East Africa Legislative Assembly (EALA). Mimi sina vita na mtu yeyote, naungana pamoja na Wakenya. Kama nilivyosema Kiswahili ni lugha ya maana. Sina mtoto wa mgongo au wa tumbo ama anayetoa makamasi, wote nitawaunganisha kama Wakenya.
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Naunga Hoja ya ndugu yangu mkono ndio Kenya yetu iendelee mbele. Thank you so much.
(Mhe. (Dkt.) Rachael Nyamai): Ahsante Mheshimiwa. Tunapoendelea, ningependa kuwajulisha kwamba tuko na wanafunzi kutoka shule zifuatazo: Mugunda Girls High School, eneo Bunge la Kieni, Nyeri County; Nginda Girls High School, eneo Bunge la Maragwa, Murang’a Kaunti; St. Angela’s Girls High School, eneo Bunge la Kiambaa, Kiambu Kaunti na St. Regina Nairutia Mixed Secondary School, eneo Bunge ya Nyeri Mjini, Nyeri Kaunti. Karibuni katika Bunge.
Anayefuata katika mazungumzo yetu ni Mhe. Joyce Kamene, Mbunge wa Machakos Kaunti. Atafuatwa na Mhe. John Kiarie. Mhe. Joyce Kamene? Hayuko hapa Bungeni na nilikuwa nimemuona? Kwa hivyo, tutaenda kwa Mhe. John Kiarie kutoka Dagoretti Kusini.
Nakushukuru sana, Mhe. Spika wa Muda. Siichukulii nafasi ya kuchangia Hoja hii kwa wepesi. Ningependa kwanza kumpongeza sana ndugu yangu ambaye pia ni Mjumbe wa Eneo Bunge lililo hapa mjini katika Kaunti ya Nairobi. Nampongeza sana Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya maana zaidi. Nafahamu kuwa Mhe. Yusuf Hassan ni mwanahabari anaye uzoefu mkubwa katika uhariri wa habari. Ni desturi na historia yake iliyomshawishi kuleta Hoja hii muhimu ya kutupendekeza tubuni Baraza la Kiswahili hapa nchini. Kwanza kabisa, nampongeza Mhe. Yusuf Hassan kwa wazo hilo bunifu na la maana zaidi kwa nchi yetu na lugha tukufu ya Kiswahili.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Mwimbaji wa wimbo aliimba na kusema Kiswahili kitukuzwe kwani ni lugha ya Taifa. Akasema pia watu wanapokutana bila lugha, watakwama. Hakika, chambilecho wahenga, mwacha mila ni mtumwa. Kunaye msomi tajika kwa jina la Leo Mohammed ambaye hufunza desturi za jamii, watu na mataifa. Katika mafunzo yake, mwalimu Leo Mohammed anatushawishi kwamba adui wa mtu ni mtu. Anatushawishi pia kuwa anayetaka kukutelekeza, kukupokonya na hata kukutia utumwani, jambo analofanya kwanza ni kukunyang’anya lugha yako. Mwalimu Leo Mohammed hufunza kwamba yeyote anayetaka kukufanya mtumwa, huwa kwanza anakunyang’anya jina la babako. Jina la babako ndilo hubeba asili yako. Kisha, anakunyang’anya lugha ya mamako kwa sababu hapo ndipo culture yako ipo. Hapo ndipo utamaduni wako upo. Anasema kwamba ni vizuri yeyote anayependa kuzingatia utamadani wake ahifadhi lugha yake. Nina hofu sana kwa sababu nchi yetu inatajika duniani nzima kwa sababu ya wanariadha wetu wanaotuletea sifa kuu. Lakini wanaposhinda na kukutana na wanahabari, huwa tunawaona wakijikanganya na lugha za kigeni. Wanapofanya hivyo, yule ambaye alikuwa amepata hadhi ya juu sana kwa kushinda mbio za riadha, anashushwa hadhi kwa sababu anajaribu kuongea kwa lugha ya kigeni. Anapojaribu kuongea lugha ya kigeni, anakanganywa na ile ambayo tunaita lafudhi – athari za lugha ya mama. Hii ni kwa sababu wengi wao wanatoka katika sehemu za Bonde la Ufa na Mlima Kenya. Wakijaribu kuongea lugha za kigeni, lafudhi inawatatiza, na wanapata athari kubwa sana za lugha ya mama. Napendekeza kuwa kupitia Baraza hili litakalobuniwa, tuwahimize wanariadha wetu kwamba lugha yao iwe ni Kiswahili. Yule ambaye anataka kumhoji ajifunze lugha yetu. Wagiriki wakishinda, wanaongea lugha yao. Wafaransa wakishinda, wanaongea Kifaransa. Huyo mwanahabari achukue jukumu la kutafsiri lugha yetu ili wanariadha wetu waweze kuhifadhi hadhi yao wakishinda mbio hizo. Wasishushe hadhi yao wakijaribu kuongea lugha zinazowatatiza. Ni jambo la kustaajabisha kwamba hapa nchini, tunaenzi mashirika na taasisi za kigeni ambazo zimebuni mabaraza ya lugha zao zilizo hapa nchini. Sio jambo baya kuwa na mabaraza hayo. Hapa Nairobi, tunazo British Council, Goethe Institute na Confucius Institute. British Council inaenzi lugha ya Kiingereza. Inaiimarisha na kuiweka katika safu za juu sana, na pia kutuhimiza tuongee lugha yao. Kwa hivyo, hili ni jambo la busara ambalo limeletwa hapa na Mhe. Yusuf. Tukiwa na taasisi yetu ambayo kazi yake ni kuhimiza watu waenzi lugha yetu, tutakuwa tumechukua hatua ya maana sana kama nchi. Pia, tutapeleka taasisi hiyo katika nchi za mbali ili tuhimize wananchi wakienzi Kiswahili. Tutakapobuni Baraza hili, itabidi tuwakumbuke wale magwiji wa lugha ya Kiswahili ambao walitutangulia. Kunao wasomi tajika. Tutaweza kumkumbuka msomi Ali Mazrui, aliyefanya kazi kubwa sana ya kuimarisha lugha ya Kiswahili na kueneza dini ya Kiislamu katika bara letu la Afrika. Tunahitaji mahali ambapo tunaweza kumuenzi msomi huyu. Kuna wasomi wa hivi punde kama vile Ken Walibora, ambaye vitabu vyake vilikuwa katika mtaala wa masomo ya nchi hii. Hatungependa kumsahau. Kando na wasomi, tuna watangazaji tajika kama Leonard Mambo Mbotela, ambaye ni gwiji wa lugha. Tunaye mwanahabari Swaleh Mdoe, na wengine wengi, ambao wameibuka kama watu tajika ambao wamemezea lugha yetu ya taifa. Baraza hilo la lugha ya Kiswahili lichukue jukumu hilo la kuwaenzi hao wasomi na magwiji wa lugha ya Kiswahili. Jambo lililonifadhaisha sana ni kuwa katika Kongamano la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wetu wa awali alikuwa Mwenyekiti katika kikao kilichopitisha hoja kuwa Kifaransa kijumuishwe katika lugha za nchi za Afrika Mashariki. Jambo hilo lilinifadhaisha sana kwa sababu katika nchi zetu za Jumuiya ya Afrika Mashariki, tuna lugha yetu ya kiasili ya Kiswahili. Hao tunaowaenzi zaidi na kutumia lugha zao, tusiwahi sahau hata siku moja kwamba walikuwa wakoloni waliotuweka utumwani. Kwa kuenzi lugha zao, tunaendeleza zile itikadi zao za kikoloni. Nahimiza Bunge hili lisimame kidete na kuiambia
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Jumuiya ya Afrika Mashariki ikosoe pendekezo hilo lililopitishwa kwamba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitumie lugha ya Kifaransa kama mojawapo ya lugha rasmi. Tuinue Kiswahili mahali ambapo tulitaka kuweka lugha hizo za kigeni. Mwisho kabisa, kila mtu ana jukumu. Hata tunaposubiri Baraza hilo libuniwe ili tukuze lugha yetu, itatubidi sisi wenyewe tuchukue jukumu. Bunge hili litenge siku moja ya kujadiliana katika lugha ya Kiswahili. Tunazo Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Kwangu nyumbani, nimewahimiza watoto wangu wajue lugha ya kiasili ya mama na wanaiongea. Pia wanaiongea lugha ya Kiswahili. Wakienda shuleni, watafunzwa Kifaransa na Kizungu. Lakini nyumbani, mimi ni mwalimu wa kwanza wa lugha na nahimiza lugha zetu zienziwe daima na daima. Ahsante sana kwa kunipa nafasi hii, Mhe. Spika wa Muda. Nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwa lugha ya kitaifa tunayoienzi sana. Kiswahili kitukuzwe.
(Mhe. (Dkt) Rachel Nyamai): Waheshimiwa Wabunge, naona watu wengi walikuwa na haja ya kuzungumzia Hoja hii, lakini muda ambao ulikuwa umetengewa umeisha. Ningependa kumuita Mtoa Hoja ahitimishe mjadala wake. Mhe. Yussuf.
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Kwa sababu ya hamu kubwa imeonyeshwa na Wabunge, ningependa kuomba niwape Wabunge watatu ambao wameniomba wakati mdogo. Hao ni Mbunge wa Nandi, Cynthia Muge; Mbunge Rashid Bedzimba wa Kisauni; Mhe. Julius Sankuli wa Kilgoris; na Mheshimiwa wa eneo Bunge la Masinga. Naomba niwape hao wanne dakika moja moja ili waweze kuchangia.
Katika orodha ambayo imetolewa na Mhe. Yusuf, tutaanza na Mhe. Cynthia.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya umuhimu kabisa katika Bunge hili inayohusu kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili nchini Kenya. Kiswahili kama vile Wabunge wenzangu wamesema ni lugha ya maana sana ambayo inazungumzwa na watu wengi duniani. Naunga mkono Hoja hii nikisema kwamba tuhakikishe ya kuwa lugha ya Kiswahili imetukuzwa. Pia, pale kwenye Bunge za Kaunti, bado wanatumia Kanuni za Kudumu. Hawana chapisho kwa lugha ya Kiswahili. Hoja hii ni muhimu na itatusaidia sana. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kiasili ya Kiafrika na inatusaidia sisi kama Waafrika. Lugha ya Kiswahili ina heshima na hili Baraza litatusaidia tuhakikishe kwamba kila wakati tunadhibiti na kukuza lugha ya Kiswahili nchini Kenya. Nashukuru Mhe. Yusuf kwa kunipatia hii nafasi niweze kuichangia na naiunga mkono Hoja hii kwa dhati. Ahsante.
Mhe. Bedzimba.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nachukua fursa hii kumshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kunipa hii fursa ili niweze kupenyeza sauti yangu katika Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Naunga mkono kwa sababu wakati Baraza hili litakapobuniwa, nina imani kwamba Kiswahili kitashamiri na kitakuwa lugha muhimu katika Taifa letu. Mataifa mengi yaliyondelea yalitumia lugha za mama. Ukiangalia Uingereza, Urusi na Bara la Arabu, wanatumia lugha zao na nchi hizo zimeendelea zaidi. Ukiangalia Taifa Jirani letu la Tanzania, limeweza kuwa na maendeleo mengi kwa sababu ya kutumia lugha zao. Ningeomba kwamba almashauri zote za kiserikali ziweze kuweka maandishi katika milango kwamba unapoingia katika jumba hili, unaweza kutumia lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kiswahili. Lugha ya Kiswahili si mawasiliano tu mbali lugha nzuri kwa Wakenya na Afrika Mashariki na haswa Pwani ambako ni kitovu cha Kiswahili. Lugha hii ni fursa ya vitu vingi.
Mheshimiwa Sunkuli.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Namshukuru Mhe. Yusuf Hassan. Kungekuwa na mengi ya kusema lakini kwa kuunga mkono Hoja hii, ningependa tu kusema mambo mawili mafupi. Baraza la Kiswahili litakuwa na jukumu la kupa makaazi Kiswahili. Wakati huu hatujui Kiswahili kinahifadhiwa katika wizara gani. Ingekuwa ni Wizara ya Elimu lakini wengine wanasema ni Wizara ya Utamaduni. Baraza likija, tutajua ni nani atakua akikikuza Kiswahili. La mwisho, Baraza la Kiswahili litazawasisha Kiswahili na litatia muhuri Kiswahili sanifu hasa katika vyombo vya habari na pia vile viongozi walivyozungumza. Najua katika awamu ya…
Mhe. Yusuf, malizia.
Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Leo tumekuwa na kikao cha kihistoria na naona kwamba tumefanikiwa katika kulizungumzia na tumekuwa na mjadala wa kusisimua. Tumekuwa na ari, mori na hamu kubwa sana ya kuweza kulizungumzia swala hili la Kiswahili. Tumetambua kwamba Kiswahili ni lugha muhimu ambayo ina hadhi na majukumu mbalimbali. Ni lugha ya kitaifa ambayo ni rasmi na ni lugha ya kimataifa. Ni dhahiri kwamba lugha hii ni muhimu sana na ina mawanda mapana ya kimatumizi kuliko lugha yoyote ya kiasili. Naomba tuipeleke mbele Hoja hii na ninataka kuweka swala hili mbele yako Mheshimiwa Spika wa Muda ili tuweze kuipeleka mbele katika Kikao kijayo. Nawashukuru wote ambao waliweza kuchangia na kulizungumzia. Nawapa hongera wanafunzi ambao wameweza kuhudhuria kikao cha kihistoria cha kwanza tangu niingie Bungeni. Nimekuwa katika Bunge la Kumi, Kumi na Moja na Kumi na Mbili. Ni mara ya kwanza ambapo tumetumia wakati mwingi kama huu kuzungumzia hii lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili. Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda.
Ahsante Mhe. Yusuf Hassan. Waheshimiwa wa Bunge nitahairisha pendekezo la kutoa Hoja iamuliwe.
Hon. John Kiarie.
Thank you, Hon. Temporary Speaker. I beg to move the following Motion: THAT, aware that there are many talents amongst the youth of this country; noting that these talents have been severally displayed through various inventions and also innovations by the artisans in platforms such as the Annual Youth Innovation Week and profiled on social media; concerned that most of those innovations and artworks do not go beyond making sensational stories in their localities, local dailies and social media mentions; noting that most of those innovations and artworks are crucial in ideas promotion, intellectual development and at creating employment and addressing the problems that affect us as Kenyans on a daily basis; concerned that there is inadequate support and administrative measures to support the artisans; cognizant of the fact that the Kenya Vision 2030 seeks to make our country an industrialized middle-income economy in the next nine (9) years; aware of the immense potential for wealth creation and job opportunities through our own local production generated if well-developed and commercialized; also recognizing that our imports are well in excess of Kshs2
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
billion shillings and most of these imports are not relevant to the Kenyan market, noting that home-grown technology would be region-sensitive and appropriate for the environment, social economic dynamic and suitable for our utility; further concerned that most of those artisans lack appropriate technology, skills, capital and tools; this House resolves that the National Government, through the relevant Ministry, formulates a policy ring-fencing two per cent (2%) of the monies allocated under the National Government Constituencies Fund and UWEZO Fund for the purposes of equipping artisans with the necessary skills, technology and tools. I appreciate this opportunity to move this Motion. This is a Motion that is aimed at the empowerment of artisans by the National Government. This House is populated with Members of Parliament who have a responsibility of lobbying and oversighting the NG-CDF Fund which, at the moment, is limited to the functions of education, security, infrastructure and a bit of youth development through sports and conducive environment. The intent of this Motion is to persuade MPs to see it fit to expand the mandate of the NG-CDF to accommodate some skills development and facilitation of tools for our own hustlers who are struggling when they step out of training, apprenticeship and Technical and Vocational Education and Training (TVETs) institutions. When they step out of TVETs, they are not able to go into the market because they are deficient in skills and they do not have the tools and equipment that are required. I stand here to persuade my fellow MPs to see it fit for us to expand the mandate of the NG-CDF to cover those areas. Each one of us can tell stories from their constituencies of great innovations, skills and talents of young people who, if they were to be supported, they would end up going to the global stratosphere in terms of fame. Those skills exist in our country and many youths are talented. Young artists and artisans are doing wonders, but they have a limitation on start-ups. They are not able to step out of college and go into practice. So, if we expand the mandate of the NG-CDF to accommodate those artists by providing them with the necessary skills and tools, we will be equipping our young people to be fit for a time such as this. We are going to the technological world and digital age. We are going into an age where each and every person shall be remunerated for the ideas that they bring forth. They shall be remunerated commensurate to the problems that they are solving. The bigger the problem you solve, the bigger the pay. To equip our people for such a time as this, it will be in order for us to ask the NG-CDF patrons to expand its mandate to allow us to equip our own people; our young artists and artisans to live in this world. Hon. Deputy Speaker, we have a new Government. The Head of State made proclamations and he gave a vision for this country. When the Head of State sat where you are sitting, he stood up and gave us his vision for this country. Among the many things that the Head of State said were going to be the key pointers of his Government, is the creative and the digital economy. Also of importance is that the Head of State told us that he is seeking to get this country to digitalise and automate the operations of Government. Who are the people who will be digitalising and automating Government operations? If we are looking at moving to e- Government, who are the people who shall do that? It is our young people. By equipping them with skills and tools, we are enabling them to contribute to the development of this country as aligned in Vision 2030, the vision of Kenya Kwanza Government and the bottom-up approach. We will have the artists and artisans developing and pulling themselves by their bootstraps from the bottom.
Kenya is a net importer of commodities. Some of them that land in this market are not fit for our environment and utility. The amount of plastic pollution in this country is chocking. We chock our soils and rivers and, in the process, we chock ourselves. If we equip our young people to manufacture toothbrushes, toothpicks, toilet and tissue papers, as well as serviettes
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
and many other small things that we use in this country, we shall prosper. We do not need to import things like cups, plates, tiles, fittings for our houses, lamp shades and bulbs. If we equip our young people with the necessary skills and tools that they need to innovate and develop, those are things that can be readily made in our counties and constituencies.
Hon. Temporary Speaker, there was a big drive by the Deputy President who has now ascended to the Presidency, to construct Technical and Vocational Education and Training Institutions (TVETs) in our constituencies. They churn out graduates who find themselves like a deer in the headlights, when they land in the market and realise that despite being equipped with necessary training, they are unable to practise because they are limited by their skills and lack of tools. If we expand the mandate of the National Government – Constituencies Development Fund (NG-CDF) to cover skills training and tools provision, then we would have a ready industry for the graduates who come out of TVETs.
Some of the technology that we import is not fit for this country. It is developed, but it specific to the region or areas where it emanates from. When it lands in Kenya, it has to be modified to be fit for this country. It is this time that we should now start developing appropriate technology for this country. I urge Members of Parliament to see the import in us equipping our young people with skills and tools. The Bible reminds us that when Moses was called, he said that he was not fit to lead the people. He said that he was a stammerer; unable to speak. The good Lord asked him what he had in his hands. He said he had a rod. He was told to take it and lead the people out of captivity into the promised land.
For the people in Parliament, the rod or stuff that they hold is the NG-CDF. Even as we, Members of Parliament, urge Government ministries and the Executive for policies, we can take the first step in faith by using what is in our control and hands to start walking towards a journey of equipping our young people with skills and required tools, so that they can offer appropriate technology that is fit for a time such as this in the history of our country. We are speaking about the future. We call ourselves to be alert that we are now in the fourth industrial revolution where Africa can leapfrog to the front. We were borrowers of technology in the first, second and third industrial revolutions. However, in the fourth industrial revolution, Kenya is known to have invented financial technology that is acclaimed globally. We invented M-Pesa which is heralded and glorified as one of the finest inventions of our time. How about we develop more young people who can give us more M-pesas and innovations for the future?
Hon. Temporary Speaker, I take this opportunity to urge Members of Parliament to support this Motion. Because my time is up, I would like to request for your guidance because Hon. Professor is ready to second this Motion. I will seek guidance from you as to whether she will second it now or in the afternoon. Thank you very much, Hon. Temporary Speaker.
Thank you, Hon. Kiarie. That will be done in another sitting.
(Hon. (Dr.) Rachael Nyamai): Hon. Members, the time being 1.00 p.m., this House stands adjourned until this afternoon at 2.30 p.m.
The House rose at 1.00 p.m.
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.
Clerk of the National Assembly Parliament Buildings Nairobi
Nakala hii ya kieletroniki ya Ripoti Rasmi ni ya kutoa habari pekee. Nakala iliyothibitishwa ya Ripoti hii inapatikana kwa Mhariri Mkuu.