HTTP 200 OK
Allow: GET, POST, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"count": 1608389,
"next": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154024",
"previous": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=api&page=154022",
"results": [
{
"id": 1558422,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558422/?format=api",
"text_counter": 243,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninaona Seneta wa Narok leo amepewa jina kuwa yeye ni simba. Sijui ni simba dume au jike? Naarifiwa ni simba jike."
},
{
"id": 1558423,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558423/?format=api",
"text_counter": 244,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mumma",
"speaker_title": "The Temporary Speaker",
"speaker": null,
"content": " Order, Senator. Withdraw that."
},
{
"id": 1558424,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558424/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi. Spika wa Muda, nimetoa na kuomba msamaha. Sen. Olekina amekuwa na wasiwasi ni kwa nini tunatoa fedha hii asilimia mia moja kwa ule mgao ambao unakwenda moja kwa moja kwa kaunti zetu. Amependekeza tuweze kufikiria njia mbadala za kuongeza kitita hiki. Ninakubaliana na mawazo yale. Hata hivyo, ni lazima tuanzie mahali fulani kwa sababu tunaona kero ambayo vijana wetu wamepitia."
},
{
"id": 1558425,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558425/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Leo hii kuna timu pale Kaunti ya Kwale inayojiita SS Asad. Timu hii inashiriki katika ligi kuu ya kitaifa ama daraja la pili ama la kwanza. Inafaa kusafiri kutoka Kwale takriban kila wikendi kwenda maeneo ya kaunti tofauti. Timu ile imepata shida sana kupata ufadhili."
},
{
"id": 1558426,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558426/?format=api",
"text_counter": 247,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Serikali ya Kaunti ya Kwale imejaribu kuipatia ufadhili lakini haujatosheleza timu ile. Kila wikendi, ninapata maombi kutoka kwa maofisa wa klabu kile wakiniomba msaada. Mimi ni mchezaji wa timu ya Bunge FC tukiongozwa na Sen. Cheruiyot. Nimewahi kucheza soka tangu nikiwa kijana mdogo."
},
{
"id": 1558427,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558427/?format=api",
"text_counter": 248,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ni lazima nichange kila wikendi ili kuhakikisha timu ile imepata usafiri. Vile vile, kuna timu inayojiita Samburu Lions. Ni timu shwari kabisa iliyojaza talanta kedekede pale lakini wanashindwa kuendelea katika michezo kwa kukosa ufadhili."
},
{
"id": 1558428,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558428/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nina imani kupitia Mswada huu wa Sen. Sifuna, timu zile nimetaja na zinginezo na wale wanamichezo wa aina tofauti watapata ufadhili ili waweze kuendelea kuonyesha talanta yao. Mwishowe, nina imani pengine talanta ile itageuka na kuwa ajira."
},
{
"id": 1558429,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558429/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi. Spika wa Muda, kwa wale watakaopewa majukumu ya kuchunga fedha inayokuja kwa makundi ya michezo ya kaunti, ninawapa ilani kuwa fedha hii sio ya kutumiwa vibaya. Ipo kuhakikisha kwamba wale vijana wetu ambao tunawapenda; ambao tumekuwa tukiwasaidia kupitia vifaa au pesa, wapate fursa ya kushiriki katika michezo yao kikamilifu."
},
{
"id": 1558430,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558430/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninajua asili mia moja hii ni nyingi kwenu. Ninafahamu mnafaa kutoa huduma mbalimbali kama vile afya, maji na kilimo bora. Vile vile, vijana wetu wanahitaji usaidizi na ufadhili. Zile pesa zikikufikia pale kwa Wizara ya Michezo katika kaunti zetu, ninaomba magavana, mawaziri wa fedha na wale wa michezo wawe wepesi kuhakikisha fedha zile zimefikishwa kwa makundi ya vijana pasipo na utepetevu wowote wala kucheleweshwa ili tuone matunda yake."
},
{
"id": 1558431,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1558431/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi. Spika wa Muda, hivi punde pengine nikipata fursa, hata mimi nitachangia katika Mswada wangu ambao pia tumesukuma na Seneta Ojienda ambao unahusu michezo. Nina imani kupitia sheria zote hizi za michezo, lengo letu ni kuhakikisha The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}
]
}