3 Aug 2021 in National Assembly:
Nawasii na kuwarai tuangalie sheria hii tukipanua mbavu zetu, tuangalia sheria hii tukiwa tumekubali ya kuwa ni sheria ambayo tayari iko. Lile linafanyika ni kuibadilisha iweze kulingana na Katiba ya sasa.
view
3 Aug 2021 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, maneno yako ni kuntu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, nilitunga sheria hii kwa sababu tulikuwa tumeona yaliyoko kuwa hakuna hesabu zinazowekwa katika mambo ya waqf. Tuliona yale yaliyoko. Ni mikakati gani zitatumika kuchagua makamishna? Nilipoleta sheria hiyo, Serikali, kupitia kwa aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi katika Bunge, Mhe. Aden Duale, aliniambia kuwa kuna sheria nyingine tayari inajadiliwa, kwa hivyo, ili tusishindane, nikubali yangu iwe nyuma. Nakubaliana na vinara wote walioko katika Bunge na nafurahi. Hata juzi tulikuwa Mombasa tukihudhuria sherehe fulani ya Idd pamoja na Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi na akaahidi atahakikisha ...
view
3 Aug 2021 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
8 Jul 2021 in National Assembly:
Asante sana Bwana Spika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
8 Jul 2021 in National Assembly:
Kupitia kwa Kanuni za Kudumu 44(2)(c), ninaomba jawabu kutoka kwenye Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kuhusu mambo ya waendeshaji wa mabasi ya abiria wakati huu wa janga la COVID-19 katika nchi yetu. Twakubali na hatupingi kuwa reli na usafiri wa anga unabeba wateja wasafiri zikiwa zimejaa wakati huu wa janga la COVID-19. Lakini, gari za abiria, zinazofika zaidi ya elfu moja, mia mbili na sitini kupitia kampuni arobaini na mbili, zinabeba zikiwa na nusu abiria na wamekatazwa usafiri wa usiku. Kampuni kadhaa zimefungwa, watu hawajalipwa mishahara, wengine wamefutwa kazi, na hali yazidi kuwa ngumu kwao. Washika dao wakiwemo NTSA na ...
view
7 Jul 2021 in National Assembly:
Mhe. Spika natoa kongole na kukubaliana na mwenzangu Mhe. Tandaza. Kama walivyozungumza Wajumbe kadhaa, masuala ya ardhi ni tetesi, hususan huko kwetu maeneo ya Pwani. Nataka kutoa mfano wa eneo lile natoka mimi la Mvita. Kihistoria, kuna baadhi ya watu waliopatiwa ardhi hizi sio kwa sababu nyingine lakini walipatiwa kwa niaba ya wakaazi wa Mvita na Mombasa kwa jumla. Na hii ilikuwa kabla Kenya kupata uhuru. Ardhi hizi walipatiwa watu waliokuwa wanaitwa sultan kwa sababu walikuwa na mamlaka ya maeneo yale. Wakati wa aliyekuwa Mbunge wa Mvita, marehemu Shariff Nassir, Mungu amuweke pema palipo na wema, alihakikisha Wizara ya Ardhi ...
view
1 Jul 2021 in National Assembly:
Thank you very much, Hon. Speaker. I had asked two questions. The first one was to the Cabinet Secretary on his roadside declaration about students being sent home. The response coming here is different from what was translated by the head-teachers. He talked about students from public schools and students whose parents are able to pay. What was being relayed was that a majority of Kenyans can educate their children at a time like this when we have the COVID-19 pandemic. Equally, he talked about public day schools being totally free except for the other issues that come with school ...
view
1 Jul 2021 in National Assembly:
be fueling issues. We should allow KNUT to continue with those negotiations. When I asked the question, KNUT and TSC had not yet started those engagements. They are actually late.
view
1 Jul 2021 in National Assembly:
Actually, it was not related to this. However, if you allow me, I would like to contribute after the Chair has spoken and the other response has been given. It is with regard to something else.
view
1 Jul 2021 in National Assembly:
Mhe. Spika, nilijaribu kwa muda kupata jicho lako. Nataka kujulisha Jumba hili ya kwamba tarehe 8 Juni, nilileta ardhilhali kuhusu wachuuzi ambao wako katika eneo la Mama Ngina Drive. Kumetokea matokeo kadhaa. Ni muhimu kupata mwelekeo wako. Kamati iliyopelekewa ni ya Idara ya Uchukuzi lakini Kamata inayohusika na utalii waliwasiliana na Wizara ya Utalii na Wizara ikafungua rasmi lakini ufunguzi wake sio vile unavyotakikana. Nahofia isije ikaonekana tumeridhika kwa vile imefunguliwa lakini kiasi. Masuali yalioko bado yanaleta kero kwa sababu huwezi kufungulia watu kwa ubaguzi, wengine wanakubaliwa kufanya biashara lakini mwenye ushanga ama mwenye biashara ndogo ndogo hakubaliwi. Mhe. Spika ...
view