30 Jun 2015 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kupongeza Ripoti hii na kusihi wenzetu kutoka sehemu tofauti za Kenya waweze kuikubali. Maswala ya ardhi ni yenye chembechembe za historia kali katika Kenya.
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Pengine ungeweza kunisaidia na kikundi cha ndugu zetu walioko pale nyuma ambao wanaozungumza lugha ya short wave kidogo.
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Maswala ya ardhi kama nilivyosema yameweza kumwaga damu katika sehemu nyingi za Kenya. Kenya iliweza kupata Uhuru wake na jambo kubwa zaidi lilikuwa ni kuhusiana na maswala ya ardhi. Idadi ya Wakenya sasa hivi inazidi na kiwango cha ardhi ni kile kile. Dhuluma ambazo ziliweza kufanywa katika kihistoria hususan sisi kama watu wa Pwani, tusipoweza kuanza kuzitatua sasa hivi---Karne hii isipoweza kuwa ndio ya kutatua shida za ardhi zilizokuwa ziko, basi hatari yake itakuwa ni kubwa zaidi.
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Ningetaka kutoa mfano. Leo hii katika eneo Bunge langu la Mvita ambalo ni eneo linalojulikana ni eneo la kimji, matatizo ambayo yako na shida ambazo ziko pale zikiwemo watu wanaojiita mabwenyenye wa ardhi na wao wenyewe hawapo katika ardhi ile---
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda.
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Huwa tunafuraha sana kuona vizazi vinavyokuja vikiweza kuja katika Bunge na kuona yale mambo yaliyofanywa na wale waliopita na yale yanayohitajika kufanyika hivi sasa ili wao wahakikishe wasifanye makosa yale yale.
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Nikimalizia nilikuwa nazungumza kuhusiana na maswala ya ardhi katika eneo Bunge langu la Mvita. Mabwenyenye walioridhi ardhi wanasemekana ni wenye ardhi zile licha ya kuwa hawaonekani. Kuna watu wamekuwa wakilipa ada na kodi za ardhi kwa muda wa miaka na ikipigwa hesabu ya kodi ambazo wameweza kulipa pale na dhamani waliyoweza kuiweka katika ardhi ile, hivi sasa itakuwa ile ardhi kisawasawa inastahili kuwa ni yao. Nashukuru Mungu ya kuwa tume inayosimamia mambo ya mashamba imekubali kuja katika eneo Bunge la Mvita na kuweza kukaa chini pamoja na kila mitaa na watu waweze kuwaelezea shida za ardhi ambazo zinawakumba. Ningeomba maeneo ...
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Asante sana na ningependa kusisitiza yakuwa naipongeza na kuiunga mkono Ripoti hii kuhusiana na maswala ya ardhi.
view
30 Jun 2015 in National Assembly:
Thank you very much, Hon. Temporary Deputy Speaker. This is a very interesting Bill which comes at an interesting time. To take you back, the rise in number of firms and companies associated with security is directly connected to the erosion of the State’s ability in keeping its citizens safe and secure. I would like to give some figures which were taken from various organisations including the Human Rights Watch Africa, the Kenya Human Rights Commission and Amnesty International. According to these figures, 66 per cent of respondents who were interviewed in Nairobi were victims of some sort of crime. ...
view
25 Jun 2015 in National Assembly:
Thank you very much. This is something that is very heavy on us as Kenyans. We will recall in December last year when this House approved a debt ceiling from Kshs 1.2 trillion to Kshs 2.5 trillion. When we did that there were issues that were done including a Sessional Paper that was brought to the Departmental Committee on Finance Planning and Trade by the Cabinet Secretary. It was properly thrashed out. That matter was brought to this House, debated and approved by this House. Today we wonder why once again the Constitution is being violated. I know others have ...
view