Ali Menza Mbogo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 169.

  • 23 Aug 2023 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kutupatia nafasi ya kusema pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Mhe. Ndzai. Ninaomba utupatie nafasi tutoe rambirambi zetu. view
  • 23 Aug 2023 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Spika. Pia mimi ninasema pole. view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Asante sana Mheshimiwa Spika wa Muda… view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Mhe Spika wa Muda, ninakushukuru kwa mwongozo huo. Nitaenda kwa haraka ili wenzangu pia wapate muda na fursa ya kuchangia. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu niko na imani kwamba umetoka kwa Wizara mbili muhimu – Wizara ya Afya, na Wizara ya Kilimo – ambazo zilikaa chini zikakubaliana. Kwa hivyo, niko na imani kuwa hili ni jambo muhimu ambalo litasaidia taifa. Ubora wa chakula ni jambo muhimu sana. Pia, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu utahusisha serikali za ugatuzi katika jitihada za kuboresha chakula kabla ya kukipeleka kwenye masoko yetu. Tuko na imani kuwa wakihusishwa, mambo mengi pia yatakwenda sawa. ... view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Wananchi wanategemea mashirika ya kiserikali kuwasaidia kwa sababu hawana uwezo wa kuchunguza vile chakula kimetolewa shambani. Hiyo ni kazi ya mashirika ya kiserikali. Lakini kwa sababu hawashughuliki, na kwa sababu ufisadi umekuwa mwingi, mwananchi anapata chakula kisicho salama kinachosababisha ugonjwa wa saratani na magonjwa mengine. Kwa mfano, kuku wa gredi hupewa dawa fulani, na inabidi wakae siku saba kabla ya kuchinjwa. Lakini kwa sababu hakuna mtu anayechunguza jambo hilo, wale kuku wanachinjwa na kuletwa sokoni ilhali ile sumu bado iko kwenye nyama hiyo, na watu wanakuja wanaitumia. view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Mboga zinanyunyizwa dawa na kabla muda wa kuuzwa kufika, mtu anazivuna na kuzipeleka sokoni kwa sababu hakuna mtu anayeshughulikia jambo hilo. Taifa ambalo liko na chakula bora hupata watalii kwa maana chakula kikiwa bora, wageni watatoka sehemu tofauti kuja katika taifa letu kwa sababu wako na imani kwamba chakula chetu ni bora na salama. view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Lakini leo kama walivyosema wazungumzaji wengine, mtu akishamaliza kunywa chai, anaona kwenye runinga kwamba kuna sukari ya sumu ambayo imeingia nchini. Hicho ni kitu cha kustaajabisha. Watu wetu wanapata shida kwa kula sumu baridi. Watu wetu ni wagonjwa. Wewe ingia kwenye matatu, kama hujaingia siku nyingi, uone mtu anatoka kule tumbo languruma utafikiri kwapigwa ngoma ndani. Hii ni kwa sababu chakula ambacho amekula sio salama. Wale wanaotaka kutengeneza ofisi hii wawe ni watu ambao watajitolea. Sisi tunakubali ofisi hii iundwe, lakini wale watakaotekeleza kazi zao ndio hatujui. view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Sasa, miraa na muguka zinapigwa dawa na kuletwa sokoni. Vijana wetu wengi sasa ni wenda wazimu kwa sababu ya dawa za sumu ambazo wanatumia kila siku. view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Mheshimiwa Spika wa muda, ninakomea hapo ili nitoe nafasi kwa wenzangu kuchangia Mswada huu. view
  • 15 Aug 2023 in National Assembly: Ninaunga mkono. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus