25 Nov 2024 in National Assembly:
Tukienda kwa upande wa chakula, bei za chakula zimeshuka. Unga zamani ilikuwa inanunuliwa kwa Ksh160. Mhe Rais alisema ukweli kuwa bei ya unga imeshuka lakini shida iliyoko ni kwamba uchumi wa taifa unaimarika ikiwa pesa imeingia katika mifuko ya wananchi. Ikiwa wananchi wana fedha, basi uchumi huwa mzuri. Lakini kama mwananchi hana fedha, uchumi utakuwa wa kuzungumziwa tu. Mwananchi hatakuwa na faida.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Nikimalizia, kwa sababu muda wangu naona umekwisha, ningependa kuzungumzia kazi katika mataifa ya nje. Kweli, zimekuja juzi na zimesaidia watoto wengi. Lkini kuna watu ambao…
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Naomba dakika moja.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Kwa hivyo, vijana wapelekewe kazi kule waliko ili ziwasaidie. Ama watu watasema kwamba zile kazi zimekuja kwa ubaguzi. Kwa hivyo, kazi zingine kule Ujerumani, Uajemi ama nchi zingine zikija, zote zigawanywe katika maeneo yote, ili kila mmoja aweze kufaulu. Kwa haya mengi…
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia Mswada huu. Mazingira ni kila kitu. Katika taifa lenye afya na nguvu, ni lazima mazingira yapewe kipaumbele ili vitu vingine vipatikane. Ninamuunga mkono na kumshukuru Mhe. Mayaka kwa kuuleta Mswada huu wa kuyalinda mazingira. Kama nilivyosema hapo awali, mazingira ni muhimu. Hata kama mti wa mkalatusi una faida zake, pia una madhara yake. Ni vyema kulinganisha faida na hasara ya kitu ili kujua ni ipi imezidi. Kama vile Mhe. Mayaka alivyotaja, huo mti unakausha maji kwenye mito na kutoa nguvu kwenye mchanga. Hiyo ni hasara kubwa kwa taifa. ...
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
mengi. Kwa hivyo, mti huo upandwe kando ya bahari lakini sio katika ardhi ambayo tunategemea maji yaliyomo chini ya ardhi. Nimesimama kuuunga mkono Mswada huu na kuhakikisha kuwa mti huo uondolewe. Ingawa wakati uliletwa nchini ulifanyiwa utafiti, kila siku utafiti hufanywa duniani na kuna vitu ambavyo tulikuwa tunavitumia zamani lakini sasa havifai. Kwa mfano, zamani tulikuwa tukitumia asbestos lakini baada ya utafiti, ilisemekana kuwa inasababisha ugonjwa wa saratani. Vile vile, watu wameona kuwa mti huo wa mkalatusi una hasara kubwa. Kwa sababu hiyo, inabidi tuache kufanya vitu ambavyo tulikuwa tukifanya mwanzoni bila kujua. Utafiti wa kileo unatofautisha vitu vingine ambavyo ...
view
13 Nov 2024 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia fursa ya kuuliza swali la ziada. Je, Waziri ana ufahamu wa barabara katika Eneo Bunge la Kisauni ambayo imeanza Kiembeni kupitia Mwakirunge kwenda Rabai? Mhe. Rais alikuja kuanzisha rasmi ujenzi wa barabara hiyo inayojengwa na KeRRA. Alipoondoka, matingatinga yote yaliondoka yakamfuata. Je, Waziri ana habari hizo? Ana mipango gani ya kuendeleza ujenzi wa barabara hiyo badala ya kumwekea aibu Mhe. Rais?
view
15 Oct 2024 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa kuweza kuchangia huu Mswada wa Nyongeza ya Fedha kwa serikali za ugatuzi. Nimesimama kukubaliana na Kamati ya Bajeti kwa hali ilivyo sasa katika taifa kushindwa kupeleka fedha hizo katika serikali za ugatuzi. Ingawa kwa sasa naweza kukubaliana kwa vile hali ni ngumu kidogo, lakini wakati hali itakuwa nzuri ni vyema fedha zishuke kule mashinani kwa sababu serikali za ugatuzi zinapopata fedha, mambo mengi huendelea katika sehemu tofauti katika taifa. Hata sasa mabadiliko yale ambayo yako katika taifa ni kulingana na serikali za ugatuzi. Wakati wa zamani, fedha zote ziliwekwa katika hazina ya ...
view