15 Oct 2024 in National Assembly:
Kwa hivyo,, ni sawa kukiwa na utaratibu wa kuwalinda wananchi kwa sababu wanalipa ushuru wakitegemea kuwa Serikali ina Shirika la Viwango. Wao hawajui ni kitu gani kinachoendelea. Mboga zinazopandwa mashambani, zinanyunyiziwa kemikali fulani ambayo pia inatakikana kukaa kwa muda fulani. Kemikali hiyo inafanya jani liwe kubwa kwa haraka na wakati huo huo, mboga zinatolewa shambani na kupelekwa sokoni ambapo mwananchi wa kawaida anauziwa. Unapata watoto wako na vitumbo vikubwa unafikiria kuwa wameshiba ilhali ni maradhi tu. Yote yanasababishwa na Shirika la Viwango katika Kenya. Kwa hivyo, kama Shirika hilo halina wafanyikazi wa kutosha, waseme hivyo. Hawana
view
15 Oct 2024 in National Assembly:
ya kutosha ili watembee katika mashamba kukagua mifugo wanapokamuliwa na kuhakikisha kuwa wanakamuliwa katika mazingira mazuri. Isiwe kuwa mifugo hao wanakamuliwa na watu wamejaa matope kisha maziwa hayo yanapelekwa mahali ambapo yanauzwa. Lazima kuwe na utaratibu wa kumlinda mwananchi ili awe na uhakika. Hata watalii wakija hapa nchini na wakule vyakula bora, hiyo ni mojawapo ya njia za kuwavutia. Wanajua kuwa ukitaka kula vyakula bora, nenda Kenya. Lakini ikiwa hatutakuwa tumejipanga vizuri, basi mambo mengi yataharibika na maradhi yatakuwa mengi.
view
15 Oct 2024 in National Assembly:
Kwa hivyo, Mheshimiwa Spika wa Muda, nimesimama…
view
25 Sep 2024 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa ili nichangie Hoja hii muhimu sana kuhusu elimu. Kwanza, ninampongeza Mhe. Passaris kwa kuileta hapa ili watoto wote wapate elimu ya bure. Lakini, ninataka kukosoa ule mfumo ambao anautaka. Haya mambo yamejaribiwa katika taifa hili; kuwa na mfuko moja katika kila sehemu. Hii imesababisha kuzorota kwa taifa zima. Katika sehemu zingine unaskia wakisema wako nyuma ilhali wengine wako mbele. Hii ni kwa sababu ya mfumo wa zile fedha kuwa katika sehemu moja halafu zinagawanywa vile wanavyotaka wao - kisiasa na kwa njia isio sawa. Ikiwa pesa zitaenda mashinani, kila sehemu itapata ...
view
25 Sep 2024 in National Assembly:
Mhe. Spika wa Muda, itabidi unilinde dhidi ya hawa ambao wanazungumza hapa. Zile fedha zikienda mashinani…
view
25 Sep 2024 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa ulinzi huo. Acha nisiwaseme tena.
view
25 Sep 2024 in National Assembly:
Hizi fedha, kama zingelikuwepo tangu kubuniwa kwa taifa hili, mambo yangelienda vizuri. Shida hizi zote hazingekuwepo. Hata hatungekuwa na sehemu yoyote ya nchi inayosemekana kuwa nyuma, ilhali wengine wamesonga mbele. Hawangelalamikia ukosefu wa barabara ama ukosefu wa shule. Hii inatokana na mgao wa fedha kupunguzwa kiubaguzi na ndiyo sababu sasa hivi kutolewa kwa stakabadhi kama paspoti kumepelekwa katika sehemu tofauti. Shughuli hiyo ilipokua hapa, ilikua nzito. Kwa hivyo, hizi fedha zinastahili kupelekwa maeneo ya chini. Mahali pema ambako fedha zitaweza kusaidia zaidi ni katika NG-CDF. Mbunge apewe fedha na hata aongezewe mradi kuwe na utaratibu wa shule ambazo ziko katika ...
view
25 Sep 2024 in National Assembly:
itapungua tukifanya hivyo. Lakini kama tutachukua hizi fedha tuzilete tena katika sehemu moja, nina hakika watu wataumia zaidi.
view
25 Sep 2024 in National Assembly:
Kuna hazina nyingi za kifedha ambazo zinahusiana na mambo ya ufadhili wa shule kama karo lakini watu Mashinani hawajui vile watazipata; hawajui hata vile watatuma maombi yao na hawajui watakaribia vipi ufadhili huo. Wanakokujua ni hapo kwa Mjumbe na kwa Women Representative. Kwa hivyo, hizo fedha zote zitolewe huku Nairobi.
view