Ali Menza Mbogo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 292.

  • 25 Sep 2024 in National Assembly: Mhe. Spika wa Muda, itabidi unilinde dhidi ya hawa ambao wanazungumza hapa. Zile fedha zikienda mashinani… view
  • 25 Sep 2024 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa ulinzi huo. Acha nisiwaseme tena. view
  • 25 Sep 2024 in National Assembly: Hizi fedha, kama zingelikuwepo tangu kubuniwa kwa taifa hili, mambo yangelienda vizuri. Shida hizi zote hazingekuwepo. Hata hatungekuwa na sehemu yoyote ya nchi inayosemekana kuwa nyuma, ilhali wengine wamesonga mbele. Hawangelalamikia ukosefu wa barabara ama ukosefu wa shule. Hii inatokana na mgao wa fedha kupunguzwa kiubaguzi na ndiyo sababu sasa hivi kutolewa kwa stakabadhi kama paspoti kumepelekwa katika sehemu tofauti. Shughuli hiyo ilipokua hapa, ilikua nzito. Kwa hivyo, hizi fedha zinastahili kupelekwa maeneo ya chini. Mahali pema ambako fedha zitaweza kusaidia zaidi ni katika NG-CDF. Mbunge apewe fedha na hata aongezewe mradi kuwe na utaratibu wa shule ambazo ziko katika ... view
  • 25 Sep 2024 in National Assembly: itapungua tukifanya hivyo. Lakini kama tutachukua hizi fedha tuzilete tena katika sehemu moja, nina hakika watu wataumia zaidi. view
  • 25 Sep 2024 in National Assembly: Kuna hazina nyingi za kifedha ambazo zinahusiana na mambo ya ufadhili wa shule kama karo lakini watu Mashinani hawajui vile watazipata; hawajui hata vile watatuma maombi yao na hawajui watakaribia vipi ufadhili huo. Wanakokujua ni hapo kwa Mjumbe na kwa Women Representative. Kwa hivyo, hizo fedha zote zitolewe huku Nairobi. view
  • 25 Sep 2024 in National Assembly: Mhe. Spika wa Muda, kuna fedha Wizara ya Elimu inapewa za kujenga shule lakini hakuna jengo linajengwa kutoka Wizara. Majengo shuleni yamejengwa na hazina ya NG-CDF, na National Government Affirmative Action Fund (NGAAF). NG-CDF ndiyo inayojenga shule lakini si Wizara. Juzi walituahidi watatupatia madarasa mawili kila Mjumbe. Hakuna hata moja ambalo wamejenga. Nimesimama hapa kupinga mapendekezo ambayo yametolewa. Tunataka elimu iwe kwa watoto wote; maskini na matajiri. Hii ni kwa sababu ni haki ya kila mtoto Mkenya kupata elimu. Nimesimama hapa kusema fedha hizo zipelekwe kwa Mjumbe. Fedha zipelekwe mashinani kusudi watoto wasome. Asante sana Mhe. Spika wa Muda. view
  • 7 Aug 2024 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Mishi kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja hii kuhusu jambo ambalo linafaa kuangaliwa kwa makini sana. Ni haki ya kila Mkenya kupata matibabu yeyote yale kulingana na maradhi yanayompata. Maradhi ya akili yana daraja na sana sana yanaanzia katika msongomano wa mawazo. Yanaanzia mtu kusema peke yake and kuwa na uzito wa jambo fulani ambalo limemshinda kutekeleza. Inamtokea mtu anapigwa dafrau ukifikiria hakuona lakini kumbe akili yake ilikuwa haipo. Kama kila sehemu ingekuwa na zahanati katika taifa hili ambalo lina madaktari na wataalamu ambao wanaweza kushugulikia jambo hili, haya mambo yasingefikia pabaya. view
  • 23 Jul 2024 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii nami nipenyeze sauti yangu. Nasimama kupongeza hazina ya NG-CDF kwa miradi inayofanya mashinani. Kwa kweli, miradi ya NG-CDF ndiyo inayoonekana kila mahali. Ukitembea katika maeneo bunge, utaona bango au ishara zinazoonyesha majengo yaliyojengwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 23 Jul 2024 in National Assembly: na hazina zipi. Ukweli ni kuwa, shule nyingi ambazo hazikuweko zimejengwa. Kabla ya NG-CDF kuja, eneo langu la bunge lilikuwa na shule zilizojengwa wakati wa ukoloni. Hazikuwa nyingi. Ilibidi wanafunzi watembee kwa umbali mkubwa wakienda kutafuta elimu. Haya yote yalisababishwa na umaskini mkubwa. Mchana hawangeweza kurudi nyumbani kula chakula cha mchana. Walibaki shuleni na njaa mpaka jioni ilihali wengine hawakula asubuhi. Hata hivyo, hazina ya NG-CDF ilipokuja, mashule ya karibu yalijengwa na imekuwa rahisi kwa wanafunzi kwenda shuleni na kurudi nyumbani ili wapate kopo la uji na wanaporudi huwa wana makini katika view
  • 23 Jul 2024 in National Assembly: zao na wanapata elimu. Hazina ya NG-CDF imekatiza mambo mengi sana. Kama ingekuwa haipo, nakuhakikishia kuwa viongozi ambao wanawakilisha maeneo Bunge wangelazimika kwenda kulalamika kwa Mtukufu Rais na kusema kuwa wako chini ya miguu ya Rais. Badala ya kuwahudumia wananchi Jumamosi, wangelazimika kwenda kubisha kwa milango ya Ikulu wakiomba wajengewe view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus