23 Jul 2024 in National Assembly:
s mbili au wasaidiwe vinginevyo. Hazina ya NG-CDF imesaidia na sasa hakuna mtu anayeenda Ikulu. Wabunge wana nafasi ya kusema ukweli wa mambo yalivyo. Kama kuna makosa, watasema hata kama ni kwa kiongozi wa taifa kwa sababu wanajua miradi ya hazina ya NG-CDF itaendelea bila ya kuenda kuomba omba. Naweza kuwaita wachawi au wanga wale wanaopendekeza hazina ya NG-CDF iondolewe. Watu wanasaidika kwa kupata bursaries za shule na pesa za kujifundisha ujuzi. Kazi ya Mbunge ni kuhakikisha kuwa watu anaowakilisha wanapata msaada na ikiwezekana, atafute mbinu ya watu hao kuendelea kupata fedha hizo badala ya kusema hazina ya NG-CDF iondolewe. ...
view
20 Jun 2024 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipa fursa niweze kuzungumzia Mswada wa Fedha. Nimesimama kupinga Mswada huu. Kama viongozi, tunapaswa kuheshimu malalamishi ya wananchi na kusikiliza vilio vyao. Kuongeza kwa ushuru wa mafuta kutapandisha bei ya kila bidhaa inayohusiana na mafuta. Jambo hili halifai kabisa, kwa sababu litapandisha gharama ya maisha. Ushuru uliopendekezwa kwa bidhaa zinazotoka ng’ambo kutaathiri wananchi kwa sababu bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini bado haziwezi kukimu mahitaji yetu; hivyo basi bado tutalazimika kuleta bidhaa kutoka ng’ambo. Kwanza tutengeneze viwanda vyetu kabla ya kuweka ushuru huu. Swali la fedha zitatoka wapi, basi wapunguze matumizi katika ofisi za serikali. Wametenga pesa ...
view
20 Jun 2024 in National Assembly:
kipengee kilichomo. Mnataka kuongeza ushuru wa tairi, vyombo vya kupima saratani, na mashine za X-rays ambazo tayari ni gharama. Watu wataumia zaidi ikiwa vipengee hivi vitapita. Watoto wetu wanajitoa uhai kwa sababu ya depression. Asante Mhe. Spika, ninaupinga Mswada huu.
view
18 Jun 2024 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa ya kuchangia Mswada huu. Nachukua nafasi kuwaombea nafasi ya pili wale watoto wetu wa kike ambao wanapata ajali ya kuwa wajawazito. Ni vyema wasiwachwe nje bali wapewe nafasi ili warudi waendeleze masomo yao. Vile vile, Mswada huu utahitaji fedha kwa sababu patahitajika majengo ya kutumika kuangalia watoto katika shule hizo. Mswada utachukuwa muda mrefu sana ndiyo upitishwe. Mhe. Zamzam alileta Mswada ambao utarahisisha shughuli za kuwalinda watoto wetu wa kike, lakini Mswada huo umekaa tu pale Table Office . Hauletwi hapa. Sioni tatizo liko wapi ilhali umependekeza njia rahisi ya kusaidia watoto ...
view
18 Jun 2024 in National Assembly:
kuwasaidia watoto zaidi ya 350 waliopata ujauzito kule katika Kaunti ya Mombasa. Tunaomba huo Mswada wake uharakishwe. Vile vile, watoto wetu wa kike mjisitiri msije mkapata mimba za mapema kwa maana haziwasaidii. Mhe. Naibu Spika nimesimama kuunga mkono kwamba watoto wa kike wapewe second
view
18 Jun 2024 in National Assembly:
lakini pia wajisitiri ili hili jambo lisije likawa la mazoea. Haya yote yanasababishwa na
view
18 Jun 2024 in National Assembly:
lakini tunawatakia kila la heri. Mungu awabariki wajisitiri ili waendelee na masomo hadi vyuo vikuu.
view
24 Apr 2024 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa niongeze sauti yangu katika Hoja hii.
view
24 Apr 2024 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa niongeze sauti yangu katika Hoja hii.
view
24 Apr 2024 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Kwanza, nampongeza Mjumbe wa Lamu Mashariki kwa kuleta Hoja hii. Anataka maafisa wa jeshi wapewe heshima zao. Ameleta Hoja hii kwa sababu ya mchakato unaoendelea katika eneo bunge lake. Pale ni karibu na msitu wa Boni. Anawaona wanajeshi wakihangaika na hawalali. Wakati wa mafuriko, wanaishi katika mashimo yaliyo na maji, wakishika doria kuhakikisha kwamba adui haingii kwetu. Kwa hivyo, kuwapatia heshima wanajeshi ni vyema zaidi. Ni watu wanaojitolea kukaa mbali na familia na watoto wao. Wanarudi baada ya mwezi mmoja au miwili. Kwa hivyo, ni vyema sana wapewe heshima zao.
view