All parliamentary appearances
Entries 311 to 320 of 612.
-
27 Feb 2018 in National Assembly:
Hon. Speaker, I beg to give notice of the following Motion: THAT, this House adopts the Report of the Departmental Committee on Labour and Social Welfare on the Vetting of Nominee for Appointment as Principal Secretary, laid on the Table of the House on Tuesday, 27th February 2018, and pursuant to the provisions of Article 155(3)(b) of the Constitution, approves the appointment of Ms. Safina Kwekwe Tsungu as the Principal Secretary, State Department for Gender.
view
-
26 Sep 2017 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii. Kwanza kabisa, nasimama kuunga mkono Hoja ambayo imeletwa na Kiongozi wa Walio Wengi. Kifungu cha kwanza cha Katiba ya Kenya kinasema mamlaka ni ya mwananchi. Anaweza kuyatumia moja kwa moja ama kupitia kwa viongozi waliochaguliwa. Kifungu 95(2) cha Katiba ya Kenya kinasema Bunge itajadili chochote kinachomwathiri mwananchi wa Kenya.
view
-
26 Sep 2017 in National Assembly:
Nataka kumpongeza Kiongozi wa Walio Wengi kwa sababu tangu uchaguzi uharamishwe tarehe moja ya mwezi wa tisa, kuna kila aina za habari hapa Kenya. Wengine wametishia eti nchi ya Kenya itavurugika karibuni. Kifungu 140 cha Katiba ya Kenya kinasema iwapo uchaguzi wa Rais utaharamishwa, basi kwa muda wa siku 60, uchaguzi mwingine ufanywe. Sasa babu ameanza yake. Akiamka leo, hataki Safran Morpho; kesho hamtaki Chebukati na kesho kutwa hamtaki Chiloba. Ajue kwamba siku ni 60. Wapende uwapendao na uchukie wale unaochukia lakini sheria imeamrisha, katika Kifungu 140 cha Katiba kwamba, marudio ya uchaguzi wa Rais ufanywe kwa muda wa siku ...
view
-
26 Sep 2017 in National Assembly:
Kunao wale wanaoota kule nje na kusema kwamba watafanya maandamano, walete vurugu na kutumia mbinu zozote ili siku 60 zipite. Nia yao ni kuona Serikali ikigawanywa kuwa serikali ya nusu mkate. Ng’o! Kwa bahati mbaya kwao, Kifungu 142 cha Katiba kimeleta suluhu kwa hayo matatizo. Nimesoma Kifungu cha 168 cha Katiba ya Kenya ambacho kinaongea kuhusu wakati kuna malalamiko juu ya Jaji wa Mahakama Kuu. Sheria iko wazi kuhusu hili jambo. Hiki Kifungu kinatambua uhuru wa mahakama. Kimeweka kiwango fulani cha vurugu ndiposa mtu aweze kupeleka malalamishi. Lengo langu halihusiani na hayo. Yaliyotokea tuko na dukuduku nayo na tumekubali hukumu ...
view
-
13 Sep 2017 in National Assembly:
Asante, Mheshimiwa Spika kwa fursa hii. Ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba anayetoa cheo. Pia, ningependa kusema kongole kwako. Kuchaguliwa kwako kunaonyesha ishara kwamba chama cha Jubilee kipo, kinatawala na kitatawala. Kwa mara ya tatu, watu wa Bura wamenichagua kuwawakilisha katika Bunge hili. Sina la kuwalipa kwa sababu ya mapenzi yao. Nawashukuru na ningependa kutangaza kwao leo kuwa nawapenda na nitawahudumia kwa haki. Nimesikia Hotuba ya Rais na inanifundisha ujasiri. Leo ukitangaziwa kuwa umepoteza kiti cha Ubunge, wengi watapelekwa hospitali. Lakini Rais wa taifa alipoambiwa kuwa uchaguzi utarudiwa, alisema kuwa ana shaka na maamuzi hayo lakini atayaheshimu na ...
view
-
13 Sep 2017 in National Assembly:
34C. Hizo ni kelele za chura. Natabiri leo kuwa Uhuru atakuwa Rais kwa mara ya pili katika miezi mitatu. Hiyo ndiyo ishara na tuko tayari kumpeleka na kucheza tena. Kongole kwako na asante, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii.
view
-
15 Jun 2017 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Chairman, it is not about being in good relations with the whips. The whips at times might decide who can best represent the interests of the parties. I do not see any problem there.
view
-
18 May 2017 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza kabisa, nimesimama kuunga mkono Ripoti hii kwa sababu mimi ni mwanachama wa Kamati ambayo imetayarisha na kuileta Ripoti hii mbele yenyu. Kufikia sasa, hakuna tetezi lolote kuhusu ugavi wa nafasi za Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Muungano wa vyama vya Jubilee imepewa nafasi tano na muungano wa vyama vya CORD umepewa nafasi nne. Kwa bahati mbaya, waaniaji wa kujisimamia ni wachache na hawakupata nafasi. Hapo hakuna tetezi. Tetezi letu liko wapi? Liko kwa mchakato wa vipi tutagawanya nafasi hizi kwa Wakenya ...
view
-
18 May 2017 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja iliyo mbele yetu. Kwanza kabisa, nimesimama kuunga mkono Ripoti hii kwa sababu mimi ni mwanachama wa Kamati ambayo imetayarisha na kuileta Ripoti hii mbele yenyu. Kufikia sasa, hakuna tetezi lolote kuhusu ugavi wa nafasi za Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Muungano wa vyama vya Jubilee imepewa nafasi tano na muungano wa vyama vya CORD umepewa nafasi nne. Kwa bahati mbaya, waaniaji wa kujisimamia ni wachache na hawakupata nafasi. Hapo hakuna tetezi. Tetezi letu liko wapi? Liko kwa mchakato wa vipi tutagawanya nafasi hizi kwa Wakenya ...
view
-
18 May 2017 in National Assembly:
I am only reading a small part of it, Hon. Temporary Deputy Speaker.
view