11 May 2021 in Senate:
On behalf of Orange Democratic Movement (ODM), the women of Kenya and the Nairobi women, I proudly vote yes.
view
11 May 2021 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, for the sake of Nairobians and the women, I vote yes.
view
4 May 2021 in Senate:
Asante Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia huu Mswada wa marekebisho ya Katiba, 2020. Naunga mkono Mswada huu. Ningependa kuwakumbusha wananchi mahali tumetoka na kwa nini Mswada huu uliwekwa ili tuweze kuujadili. Tukikumbuka wakati tunapo enda katika uchaguzi, baada ya miaka mitano sisi huwa tunapoteza watoto wetu na akina mama wanaaga dunia kwa sababu ya vita. Shida ni kuwa kuna upungufu fulani katika huu Mswada na katika Katiba ya nchi yetu. Ukiangalia Kifungu cha 23 wameweka ubunifu wa nyadhifa za juu. Katika hicho kipengele kuna viti ambavyo vinatakikana viongezwe kama kiti cha Waziri Mkuu na Naibu Waziri Wakuu ...
view
4 May 2021 in Senate:
Asante Bi Naibu Spika na Seneta wenzangu kwa kumrekebisha mwenzangu hapa ambaye alikuwa anajaribu kuingilia masaa zangu ambayo ninafaa kuchangia. Tukiangalia vizuri, katika Mswada huu kuna viti 70 za eneo bunge ambazo zita ongezwea. Ninaunga mkono kabisa kwa sababu katika jimbo la Nairobi tutaongezewa eneo bunge 12. Ukiangalia idadi ya watu ambao wako Nairobi ni wengi lakini hawajawakilishwa vilivyo kwa sababu zile pesa ambazo wanapata hazitoshi. Ninajua vizuri kwamba tukipata hizo pesa, huu Mswada ukipitishwa nina uhakika bara bara zetu za Nairobi zitakuwa nzuri, watoto wataenda shule, akina mama watapata maji na kutakuwa na maendeleo. Tukiangalia katika huu Mswada pia ...
view
4 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
4 May 2021 in Senate:
Asante Bi. Naibu Spika. Sitaki kuongezewa muda.
view
4 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika, sijui ni nani ana ingilia maneno yangu kwa sababu nilikuwa nazungumzia point nzuri zaidi. Nina shanga sana nikiwaona wale wanaume Wabunge ambao wako katika Bunge hili wakipinga Mswada huu. Wanaogopa nini? Kile ambacho wanaume wanafanya, wanawake watafanya bora zaidi.
view
4 May 2021 in Senate:
Wale Wabunge wanaume walio katika Bunge hizi wasiogope kwa sababu akina mama---
view
4 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika, hiyo si hoja ya nidhamu. Ningependa kumkumbusha ya kwamba ukiangalia katika Kaunti ya Kakamega, kuna wale Maseneta wateule ambao walikuwa wamepewa ruhusa ya kupiga kura kama Seneta wa kaunti hiyo hayupo. Tuliona katika kisa cha Kakamega ambapo Seneta wa hiyo Kaunti aliwanyima nafasi Maseneta wateule kupiga kura. Ndiyo nina sisitiza ya kwamba akina mama tujitoe kinaga ubaga ili tuweze kuenda katika viwanja tupiganie viti hivi sawa sawa.
view
4 May 2021 in Senate:
Bi Naibu Spika, nikizidi kuzungumza, hiki kiti cha Seneti cha akina mama kuna wale wanasema akina mama walio chaguliwa katika kaunti na walio kwenye Bunge la Kitaifa wataletwa hapa na hawatakuwa na pesa za miradi. Ninge penda kuwakumbusha kuwa hivyo viti wakati viliundwa havikuwa na pesa za miradi. Wenyewe walika chini na wakatengeneza mpaka wakapata hicho kitita cha pesa. Kuna uwezekano tukikuja hapa hata sisi, tutaka chini ili tujue jinsi ya kupata hiyo pesa ili iweze kusaidia wananchi wa Kenya.
view