14 Mar 2018 in National Assembly:
side now co-operating with the Government side, we can work together and have some Chairpersons of Committees from the Orange Democratic Movement Party (ODM) to help.
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Hoja haijawasilishwa kikamilifu katika ule mnyambuliko ambao Mheshimiwa amesema. Unapokuwa na Hoja ni lazima useme “ I beg to move ” yani “nasongesha”.
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Lakini labda mwenzetu amesahau sheria na tamaduni za Bunge. Ukileta Hoja ni lazima “usongeshe”. Mwenzagu amesahau “kusongesha”. Lazima “asongeshe”.
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Asante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja hii. Kwanza ningependa kumshukuru Mhe. Mohamed Ali Mohamed kwa kuwasilisha Hoja hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Hii Hoja ni muhimu sana kwa sababu tuko na hospitali za rufaa mbili Kenya nzima. Tuko na Hospitali ya Rufaa ya Mafunzo ya Moi ambayo inasaidia watu wakutoka eneo la Magharibi na eneo la Nyanza. Vile vile, tuko na Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta.
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Vile vile, tuko na Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta ambayo inajali masilahi ya wagonjwa kutoka eneo la Kati, Nairobi na eneo la Mashariki. Vile vile, hii Hoja ya kuwa na Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa kule Mombasa itasaidia sana kwa sababu kuna wagonjwa wengi wanaotoka kaunti za Lamu, Mombasa, Kwale, Kilifi na Taita Taveta. Ukiangalia ajenda ya jubilee, utapata kwamba matibabu yamepewa kipaumbele. Isitoshe, kuhusu Malengo Endelevu ya Maendeleo, hasa lengo la tatu (SDG-3), mambo ya universal healthcare yamezingatiwa. Mwenzangu Mohamed Ali ameongea kiswahili mufti. Tulijaribu kumfuatilia ikawa vigumu lakini katika zile pilkapilka za kumuelewa tukagundua kwamba tunaendelea kujifunza kidogo ...
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Wajua kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa. Mimi naomba tutenge angalau siku moja ili Wabunge waongee Kiswahili. Hii ni kwa sababu wakati tunaongea Kiingereza hapa, yule nyanyangu aliye nyumbani haelewi tunachosema. Kulingana na Katiba mpya, mambo ya Bunge lazima yajadiliwe hadharani ili mwananchi wa kawaida afuatilie na apeane mawaidha yake. Nikimalizia, yafaa tutenge pesa katika Bajeti kwa sababu mara kwa mara Hoja nzuri kama hii zinaletwa hapa, tunazipitisha lakini hakuna mtu wa kuzifuatilia ili zitekelezwe. Sisi tukiwa Wabunge hatuwezi kupitisha Hoja na hiyo Hoja isitiliwe maanani.Ndiposa nimeangalia humu ndani nikamwona mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji. Katika Kiswahili ni “implementshoni”
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Hii Hoja ikipita, yafaa aifuatilie ili tuwe na Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa kule Mombasa.Wengine labda wanasema Mombasa si Kenya. Sisi tunajua Pwani ni Kenya. Ni vizuri hospitali iwe hapo karibu ili iwasaidie akina mama, watoto na wagonjwa kwa ujumla. Wakenya wanatumia pesa nyingi kuenda ng’ambo kutafuta matibabu. Wengine wanaenda kule India ilhali matibabu wanayotafuta huku yanapatikana hapa nyumbani. Ukienda kule Kenyatta, wagonjwa wamejaa sana. Tukitaka hospitali ya Kenyatta isiwe na wagonjwa wengi, lazima tuanzishe hospitali nyingine za rufaa. Kule Eldoret, kuna Hospitali ya Rufaa na Mafunzo. Tunataka hospitali ya rufaa kule Mombasa ijengwe ili wagonjwa wa saratani waende pale. ...
view
14 Mar 2018 in National Assembly:
Mhe. Mbadi amesema kulingana na kule anakotoka hawezi kuongea kiswahili maana ni kigumu sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view