15 Mar 2023 in Senate:
Bw. Spika, sisi ni watu wazima lakini tunabishana kuhusu mambo ambayo hayafai. Ningependa leo - si kesho - ikiwezekana hata saa hii jambo hili litatuliwe. Wengine wetu wamechoka. Niko na Hoja kuhusu bei ya nguvu za umeme. Wananchi wameshindwa kulipia nguvu za umeme. Baadhi ya Maseneta hawajakuwa wiki mbili sasa. Hatuwezi kuendelea hivi. Tafadhali Bw. Spika, nakusihi kwa niaba ya wananchi na kukuomba kwa kuwa leo uko na uwezo. Usipendelee upande mmoja kwa kuwa wewe ni mwamuzi na unaweza kuamua haki, na hakuna atakaye kulaumu. Usiyafuate mambo ya kesho; yamalize leo ili tuendelee na kazi yetu. Shukran.
view
9 Mar 2023 in Senate:
Shukran sana, Bw. Spika. Ninashukuru Kiongozi wa Walio Wengi kwa kuleta Petition hii leo. Hii Petition inazungumzia mambo ya zamani. Mimi nimetoka kaunti inayoitwa Marsabit. Zamani tulikuwa tunaita Northern Frontier District (NFD). Tulifungiwa huko kabisa na Wakoloni na tukaitwa marginalized community . Tukapewa jina ambalo ni kama watu disabled . Baada ya kuitwa marginalized community, Serikali ya Kenya ikapata Uhuru na Rais hayati Jomo Kenyatta akaingia mamlakani. Tuliendelea kufungiwa huko NFD na kuitwa marginalized. Serikali ya hayati Rais Moi ikaingia mamlakani bado tukaitwa marginalized . Serikali ya hayati Kibaki ikatuita bado marginalized . Serikali ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta bado ...
view
9 Mar 2023 in Senate:
. Wakoloni wametusumbua sisi. Saa hii tunapozungumza, ardhi inayoitwa Lake Turkana, watu fulani wazungu wameangalia atlas- map ya dunia, wakajua upepo mzuri uko mahali panaitwa Sarima
view
9 Mar 2023 in Senate:
. Wemekuja na kuchukua ardhi yote. Ardhi kutoka hapa mpaka Nakuru kupitia Nanyuki, Machakos hadi Kajiado, imechukuliwa. Bw. Spika, Warendile ndio wanaoishi Katika eneo Bunge la Laisamis. Malisho ya ngamia, mbuzi na ng’ombe ni kule. Sasa hivi tunavyozungumza, hawa watu wetu
view
9 Mar 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
9 Mar 2023 in Senate:
wanaongea mambo ya Kipsigis ya zamani. Waafrika wenyewe wametuletea huo ukoloni, ardhi imechukuliwa na hatuna mahali pa kulisha mifugo wetu. Wale watu ambao wanafanya kazi huko ndani, ni Wazungu. Hata seremala anatoka Afrika Kusini kuja kuwa meneja wa kambi nzima---
view
7 Mar 2023 in Senate:
Shukrani, Bw. Spika. Nimeshangaa kusikia Sen. Munyi Mundigi akisema kwamba korosho ilikuwa inanunuliwa kwa zaidi ya Ksh100 na leo, inanunuliwa na Ksh30 peke yake.
view
7 Mar 2023 in Senate:
ya Kenya Kwanza inasema itasaidia ukulima. Saa hizi, kuna shida Kenya. Nimetoka Kaunti iliyo kwa mpaka wa Ethiopia. Ukulima Kenya ulikwisha, ukafa na ukazikwa. Saa hizi wakaazi wa Marsabit na Moyale wanatoa chakula kutoka Ethiopia. Mpaka unaoitwa Moyale... Bw. Spika, bei ya unga wa ngano na mahidi nchini Ethiopia ni nusu ya bei ya unga huku Kenya. Bei ya maharagwe pia ni hivyo. Vitunguu na viazi hutoka Tanzania. Vyakula vingi vinatoka Tanzania na Uganda.
view
7 Mar 2023 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Mahali nimetoka, hatuna korosho, makadamia ama vitu kama hivyo. Nitafurahi sana akinifunza. Sen. Kinyua akiniuliza maneno ya nyama, nitamwambia hiyo ni ya ngamia au mbuzi kwa kunusa tu bila kuonja. Sen. Ali Roba ni shahidi wangu hapo. Ninashukuru amenieleza. Bw. Spika, shida tuliyo nayo - ukiangalia upandaji wa korosho na makadamia - ni kwamba ukulima umekuwa na shida sana. Mashamba za kahawa zote zimebadilishwa kuwa biashara za nyumba. Kahawa na majani chai zinaendelea kupotea. Ile shida tuko nayo ni kwamba wakati huu maziwa tunayotumia yanatoka Uganda. Kwanza, maziwa haya yanatoka Uropa na kupelekwa Kampala yakiwa maziwa ...
view
7 Mar 2023 in Senate:
Thank you Mr. Speaker, Sir. I come from Marsabit County. We have wind power called Lake Turkana Wind Power in Marsabit. I think it is the largest wind power in Africa. In support of this Bill, I would like to say that our children in Turkana, a place called Sarima where the offices of the Lake Turkana Wind Power are being operated from, the children living there have no clothes, no place to sleep, no food, no water, no survival at all. If you look at the investors who invested in this Lake Turkana Wind Power, they are mainly from ...
view