18 Apr 2013 in National Assembly:
Sisi, wakazi wa Trans Nzoia, tunajivunia sana kilimo, na itakuwa vizuri sana iwapo masuala ya wakulima yataangaziwa. Kila kunapofika wakati wa musimu wa mvua, vifaa vya kilimo, na haswa mbolea, ambayo huletwa nchini kutoka ngâambo, vinakosekana. Itakuwa vizuri sana tukijiandaa mapema na vifaa vya kilimo ndiyo wakati wa kulima unapowadia wakulima wasihangaike kutafuta vifaa hivyo. Kwa mfano, mahindi hukuzwa Trans Nzoia lakini wakati wa upanzi ukiwadia, utaona kwamba hata mbegu za mahindi hazipatikani. Pia, bei ya mbegu huongezeka wakati huo.
view
18 Apr 2013 in National Assembly:
Nikizungumzia suala la barabara, miaka kadhaa iliyopita kuna sehemu ambako ngâombe na mbuzi walikuwa wakilala kwenye barabara lakini kwingineko hakukuwa na barabara za lami. Ukitembelea sehemu ya uwakilishi Bungeni ya Saboti, huwezi kuona hata barabara moja ambayo imewekwa lami kilomita tano. Kuhusu elimu, katika eneo langu la Saboti huwezi kuona shule hata moja yenye kiwango cha mkoa ama kitaifa.

Kwa hayo machache, ninaiunga mkono hoja hii.
view
18 Apr 2013 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninaiunga mkono hoja hii.
view