6 Jul 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
6 Jul 2021 in Senate:
health, but I think that has now been dealt with. We need somebody with technical knowledge who can have a direct link with these people. In general, this Bill has been improved from the version that was read before the House last time. It is worth noting that we can now process and take it forward to the next level. The other thing I want to talk about is that there should be good budgetary allocation for these services. We urge governors not to just concentrate on Level 4 and 5 hospitals. They should also think about the common mwananchi ...
view
18 May 2021 in Senate:
Bi Spika, kwanza ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili nichangie katika kutoa shukrani kwa Rais Suluhu Hassan kwa Hotuba yake. Ninampongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Maswala ya Sheria na Haki za Binadamu, kwa kuzungumza Kiswahili sanifu mchana huu.
view
18 May 2021 in Senate:
Ninaungana na Maseneta waliyozungumza mbeleni kumpongeza Rais Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili, ninampongeza kwa kuanzisha urafiki na ujirani mwema na Taifa la Kenya kwa kututembelea. Waswahili husema: “Fimbo ya mbali haiui nyoka”. Hivyo basi, tukiwa na jirani ambaye ni Tanzania na tunahusiana vizuri, ni wazi kwamba tunaweza kumtegemea. Uhusiano wa hizi nchi mbili unaweza kuleta manufaa sana.
view
18 May 2021 in Senate:
Pia ninampongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpa Mhe. Rais Suluhu Hassan nafasi ya kipekee kuhutubia kikao cha Pamoja cha Bunge la Kenya. Marais wengi
view
18 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
18 May 2021 in Senate:
wametutembelea hapa Kenya lakini hawajawahi kupata nafasi ya kuhutubia Kikao cha Pamoja cha Bunge.
view
18 May 2021 in Senate:
Isitoshe, ninamshukuru Rais Mhe. Suluhu Hassan kwa mambo aliyozungumzia katika Hotuba yake. Ninampongeza kwa kuwa mstari wa mbele kutambua kwamba janga la COVID-19 limeleta madhara makubwa kwa watu wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Alizidi kusema tuungane sote kama Jumuiya, ili kuhakikisha tunapigana na janga hili lililosababisha matatizo mengi. Alihimiza haya mataifa mawili yapime wananchi wanaovuka mpaka wa Kenya na Tanzania ili kuhakikisha hakuna kusambaza hivi virusi. Rais Suluhu alitambua kwamba tusipoweka jitihada za kupambana na hili janga la COVID-19, huenda litatusababishia madhara makubwa sana. Tunapoangalia Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni vizuri pia tuangalie jinsi jumuiya zingine zimefaidika kwa kuwa ...
view
18 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
18 May 2021 in Senate:
hawa marais wawili. Wamejiweka mstari wa mbele kustawisha uhusiano wa karibu na kuboresha biashara na uchumi baina ya mataifa yetu mawili. Nikimalizia, ikiwa hizi nchi zetu zitakuja pamoja, hata kupigana na ufisadi itakuwa rahisi. Tukiwa na uhusiano mzuri, itawezekana kubadilisha habari za ujasusi kati ya mataifa yetu na haswa Jumuiya nzima ya Afrika Mashariki. Bi Spika wa Muda ninakupongeza wewe pia kwa sababu umeangazia sana faida tunazoweza kupata tukiwa na uhusiano mwema na Tanzania. Ninakumbuka nilipokuwa Mwenyekiti wa Shirika la Wanasheria nchini Kenya, tulisafiri hadi Uganda kukutana na Rais wa Uganda, Kaguta Yoweri Museveni na tukakubaliana kwamba mawakili wa Jumuiya ...
view