All parliamentary appearances
Entries 491 to 500 of 1050.
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, hilo ni swali nzuri. Tumekuwa tunawaza kama tunaweza kushirikisha, si Wizara ya Maji pekee bali Wizara ya Mazingira na Madini, Wizara ya Ardhi na Wizara ya Kilimo ili tushirikiane na kupambana na mafuriko ya mvua kwa sababu yanaharibu barabara sana. Kwa hivyo, hilo ni swali nzuri na ninalitilia maanani. Ninasema hivyo kwa sababu ukiangalia Barabara ya Narok-Mai-Mahiu inahusu Wizara hizo zote. Wakati ilipotengenezwa hawakuzingatia milima na wakati maji yalikuja yalibomoa barabara kama bado inajengwa. Kwa hivyo, tuko na hilo wazo na tutalifuatilia ili tusaidiane.
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, upungufu wa pesa hauturuhusu kutengeneza barabara zote ambazo zimeharibiwa na mvua. Lakini ningependa kuwahakikishia kwamba tunaendelea kukarabati barabara na pesa tunazopewa na Hazina kuu ya Serikali.
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Asante, Naibu wa Spika. Sijasema nimetenga Kshs60 milioni. Nimetenga Kshs30 milioni mwaka huu na nimetoa awamu ya kwanza ya Kshs14 milioni na kazi hiyo inaendelea. Sijasema kwamba hizo Kshs30 milioni ni mwisho. Tunafanya kazi na tukiona kuna haja ya kuongeza, tutajikaza kutafuta pesa ili ujenzi huo ukamilike.
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Ni kandarasi ya miezi sita hadi tisa.
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Asante, Bwana Naibu Spika. Hilo ni swali nzuri sana. Hivi karibuni, nitawasilisha Mswada hapa Bungeni; Engineers Bill. Ninawaomba Wabunge wapitishe Mswada huo. Uhandisi ni muhimu sana kwa utekelezaji wa barabara. Kwa hivyo, tumeunda sheria ya kuhakikisha kwamba mhandisi ambaye anafanya kazi katika sehemu fulani anatii sheria hiyo na anakuwa na heshima kwa kazi yake. Pili, wakati kazi inaendelea kwa barabara, inabidi mhandisi huyo afanye kazi jinsi inavyotakikana bila kuchelewa. Hivyo ndivyo ilivyo katika sheria hiyo. Ninaomba Wabunge wapitishe Mswada huu utakapowasilishwa hapa Bungeni ili tuwe na barabara nzuri.
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Bwana Naibu Spika, maswali yote ni swali moja. Hivyo ndivyo nimesikia mimi mwenyewe. Ningetaka kutoa hakikisho kwa Mheshimiwa Leshomo. Kama ni kwenda kwa mguu, awe tayari aende na miguu, twende pamoja; kama ni kwenda kwa piki piki awe tayari ili twende pamoja; kama ni kwenda kwa gari awe tayari twende pamoja. Niko tayari kwenda huko. Pili, barabara itakarabatiwa kutoka Rumuruti mpaka Maralal lakini tumeanzia Naibor wakati huu. Hiyo haimaanishi kwamba tutamalizia Naibor. Itaenda kutoka Maralal mpaka Rumuruti na itabidi tutumie pesa ambazo tumetenga mpaka mwisho wake. Ikiwa hazitatosha, itatubidi tutafute pesa zingine ili tumalize ukarabati huo vizuri. Ningetaka kuwapa pole ...
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Bwana Naibu Spika yule ambaye ameniomba---
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Na mhe. Karua yuko tayari!
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Bwana Naibu Spika, lazima nirudi kwa Wizara ili niangalie vile kazi ilivyo huko halafu nitarudi hapa Bunge kutoa tarehe yenyewe ya kuenda huko.
view
-
25 Aug 2010 in National Assembly:
Asante, Bwana Naibu Spika, naitikia mwito wako.
view