All parliamentary appearances
Entries 121 to 130 of 460.
-
24 Sep 2013 in Senate:
Tatu, Bw. Spika, ningependa kuwapongeza viongozi wote na wanasiasa wote wa Upinzani, wakiongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, aliyekuwa Naibu wa Waziri Mkuu, Seneta Orengo na Seneta Wetangula, kwa kuweka tofauti zetu za kisiasa kando na kusimama kwa umoja kama Wakenya kujumuika na Wakenya wengine kwa hili janga lililotupata.
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Kwa sababu ya wakati, Bw. Spika, ningependa kuwapongeza viongoizi wa vikosi vya usalama – Inspekta Jenerali wa Polisi, naibu wake, Madam Kahindi, mkuu wa kikosi cha wanajeshi, Bw. Karangi, na wale wengine wote ambao waliweza kusaidiana nao katika kuwaokoa manusura waliokuwa ndani ya jumba la Westgate.
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Lakini Bw. Spika, siko hapa kumlaumu mtu yeyote yule; huu sio wakati wa kulaumiana lakini kwa sababu maisha ya Wakenya ni muhimu kushinda siasa; usalama wa Wakenya ni kitu cha kuwekewa kipaumbele kuliko mambo mengine yote. Bw. Spika, ningependa kuvipongeza vikosi hivi vingine lakini swali langu liko kwa Kitengo cha Ujasusi kijulikanacho kama National Intelligence Service (NIS) . Walikuwa wapi mambo haya yote yalipokuwa yakipangwa? Niko ndani ya Serikali na nina imani na Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto. Lakini katika mambo ya uongozi lazima tuwe serious na maslahi na usalama wa Wakenya. Haya mambo ya ...
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Bw. Spika, majambazi hawa---
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Bw. Spika, huu si ule wakati wa kuogopana hasa tunapoangalia maslahi ya Wakenya. Ni wakati wa kusimama na ukweli. Niko ndani ya Serikali ya Jubilee na nitaiunga Serikali hii kwa njia yoyote ile, lakini ukweli ubaki ukweli na usemwe!
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, you will allow me to answer some of the points of order---
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, you will add me some three more minutes because they have taken a lot of my time. This issue concerns my county yet they have interrupted me.
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, the reason I want to respond and you have already given a ruling on this matter is because this is a matter of public importance. I was arriving at that point. I know I am going to shock the nation. I will surprise the nation.
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Bw. Spika, asante sana. Haya si maneno ya mzaha wala kucheka, bado Wakenya wana huzuni. Kwa hivyo, ningeomba tuendele.
view
-
24 Sep 2013 in Senate:
Kwanza, nimesifu vikosi kadha vya usalama na wakubwa wa polisi. Lakini tuna shida katika upande wa ujasusi. Ni kwa nini nasema hivi? Ninaposimama hapa, Wakenya, Maseneta na Wabunge wenzangu watashtuka. Nawapongeza Wabunge kwa ile kazi nzuri ambayo walitufanyia kwa kusimama na sisi wakati wa shida hii. Walituchangia damu na kutupatia pesa. Pia Maseneta walitoa damu kama Sen. Moi na wengine wote. Asante sana na Mwenyezi Mungu awabariki.
view