Hassan Ali Joho

Born

1st January 1973

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

kisauni@parliament.go.ke

Link

Facebook

Telephone

0722162223

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 221.

  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Kwanza, ningependa kuunga mkono wale viongozi waliotangulia kusema mengi yametajwa. Nashukuru Rais kwa kutambua kwamba Bunge La Kumi limekuwa likifanya kazi ambayo ni muhimu ya kupeleka Miswada mbele, na akatambua ni Miswada gani. view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Jambo muhimu ambalo ningependa kusema ama ningetarajia kusikia likitiliwa shime na Mheshimiwa Rais hasa katika upande wa uchumi--- Kwanza, hata mimi ningependa kushikana na Mheshimiwa Rais kupongeza Wakenya na kuwashukuru katika uzalendo wao wa kulipa kodi, ili kufanya nchi yetu iwe ikijimudu kifedha na kuelekea na sera ya kujitegemea ili badaye tuweke kando pesa za ufadhili katika siku za usoni. Mheshimwia Naibu Spika wa Muda, kitu muhimu ambacho ningependa kuona kimezungumzia na Rais hasa ni katika fedha ambazo benki zetu zinalipisha katika mikopo - yaani rates za interest katika benki zetu. Ni kitu muhimu sana kuweza kupatia nafasi Wakenya kuendeleza ... view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Jambo muhimu ambalo Mheshimiwa Mung’aro na Mheshimiwa Nkaisserry walisema ni kwamba ukimwona Mkenya anaweza hata kutoka kwa runinga, kwa mfano MRC, na aseme yale anasema, ujue ni kuchoshwa. Ya kwamba pengine amevumilia kiwango mpaka sasa anasema: “Lile litakalokuwa na liwe.” Mimi ni mmoja wa wale ambao wanasema Pwani ni Kenya. Na ningependa Pwani iendelee kuwa Kenya bila kufikiria hata mara mbili. Lakini kitu cha muhimu ni kwamba tunataka kuona - na hili silo jambo jipya--- Ni jambo ambalo viongozi waliopigiwa kura Pwani, mwaka 2008 walikaa na Mheshimiwa Rais na wakamweleza zile issues ambazo zingali donda sugu katika maeneo ya Pwani. ... view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Bi. Naibu Spika wa Muda, naona kuwa ndugu yangu hajajua jambo la nidhambu ni nini. Nimesema hivyo kwa sababu sina raha kuona mtu anasema ati sisi ni GEMA; sisi ni KAMATUSA; tunataka tusikie kuwa sisi ni Wakenya. Ninasema hivi, hata kwa wale ndugu zangu walioko Mombasa; nawaambia wasiseme kuwa Pwani si Kenya. Ningefurahi hata viongozi wa kutoka maeneo ya GEMA, KAMATUSA na kadhalika wakisema kwanza wao ni Wakenya. Kwa hivyo hiyo isikutishe; pengine Kiswahili chakuchanganya. Baadaye tukitoka pale nje, nitakuambia kwa Kimombo ili uelewe vizuri. view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Kitu muhimu ni kwamba zile shida ambazo zinawapata watu – na mimi nimepata nafasi ya kutembea karibu nchi hii yote; shida zipo, lakini Serikali izungumzie namna--- Jana wakati Raisi alisema kwamba Pwani ni Kenya, mimi nilimuunga mkono kwamba Pwani ni Kenya. Ningependelea aendelee kusema kwamba zile shida za watu wa Pwani pia tutaziangalia na kuzipa kipaumbele, ndio Mkenya popote alipo, ajisikie kuwa yeye ni Mkenya. Si lazima atoke Thika Road peke yake; hata yule wa kutoka Miritini, kwa sababu ni wazi. Mimi ningependa kumuunga mkono Bw. Mung’aro kwamba pahali pa kutega uchumi kama Bandari ya Mombasa--- Niashukuru Wizara ya Uchukuzi ... view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Bi Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo Raisi alizungumzia jana, na ningependa kusema kwamba ni muhimu, ni kuwa Serikali inayokuja iwe na msimamo imara kuhusu pesa za Constituencies Development Fund (CDF); pesa hizi ni asilimia mbili nukta tano, lakini zimeonekana zaidi kuliko zile zingine ambazo hubaki katika mfuko mkuu wa Serikali. Ukiingia katika maeneo ambayo hata hayako katika miji mikubwa, utaona miradi ya CDF; lakini ni nadra sana kuona miradi ya Serikali kuu. Kuhusu barabara au miundo msingi, infrastructure, ni muhimu iangaliwe na ifunguliwe. Utakubaliana na mimi kwamba utalii unaleta karibu Ksh98 billion katika nchi hii, na bado hatujaona ... view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Bi Naibu Spika wa Muda, jambo muhimu ambalo mhe. Rais amelizungumzia katika Hotuba yake na ningependa waheshimiwa Wabunge na viongozi wingine kuliendeleza ni swala la usalama wa nchi yetu. Ninapenda sana kulishukuru jeshi letu la Kenya kwa kazi nzuri ya kulinda mipaka yetu na hasa vita vyao dhidi ya magaidi katika nchi ya Somalia. Ni kupitia juhudu zao usalama wa Wakenya wote utapatikana. Ningependa kumpongeza mhe. Rais juu ya msimamo wake kuhusu uchaguzi ujao. Yeye angependa kuona uchaguzi wa haki na amani. Msimamo wake ningependa sisi viongozi tuufuate ili kuwe na amani katika nchi yetu. Ninampongeza kwa kusema kwa uwazi ... view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Bi Naibu Spika wa Muda, ningependa kusema machache kuhusu siasa za nchi hii. Wengine wetu tumekuwa katika Bunge la Kumi--- view
  • 25 Apr 2012 in National Assembly: Asante, Bi. Naibu Spika wa Muda. view
  • 14 Mar 2012 in National Assembly: asked the Minister for Roads:- (a) whether he is aware of the encroachment on the road reserve land at English Point in Mkomani/Allidina, Mombasa on which the Old Nyali Bridge was situated and, if so, what measures the Government has taken to reclaim the land for public use; and. (b) whether he could confirm the details of ownership of the said parcel of land and also table ownership documents. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus