All parliamentary appearances
Entries 1281 to 1290 of 1711.
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
(3) Serikali-
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
(a) itazikuza na kuzilinda lugha tofauti za wanainchi wa Kenya; na,
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
(b) italinda na kustawisha matumizi ya lugha za kiasili, lugha ishara ya Kenya, breli na njia nyingine za mawasiliano na teknologia zinazoweza kufikiwa na watu wenye ulemavu.”
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
mhe Naibu Spika, ukiviangalia hivi vipengele katika Katiba yetu, utaona kwamba sisi kama Wakenya tumekubali kwamba lugha ya Kiswahili ndiyo lugha ya kitaifa. Hiyo ni kumaanisha kwamba lugha hii ina maana zaidi kushinda hata lugha ya Kiingereza, ambayo imetujia sisi kutokana na historia yetu – tulikuwa koloni la Uingereza. Jambo la kushangaza ni kwamba lugha ya Kiswahili bado haijatiliwa maanani kama inavyopaswa. Ndiposa namshukuru mhe Lay kwa kufikiria jinsi hii.
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
Tukianzia hapa kwetu Bungeni, kanuni za Bunge haziko katika lugha ya Kiswahili. Kamati ya Kanuni, Itifaki na Mienendo ya Bunge inafaa kuangazia umuhimu wa kutafsiriwa kwa kanuni za Bunge kwa lugha ya Kiswahili. Mhe Lay amethibitisha kwamba unapotunga Hoja na Miswada kwa madhumuni ya kuileta Bungeni, ni lazima uandike kwa lugha ya Kiingereza. Hilo ni jambo la kufedheesha. Mimi mwenyewe nimejaribu kubuni Hoja kwa lugha ya Kiswahili lakini maafisa wa Bunge wanaopaswa kutusaidia kufanya hivyo, hawaielewi lugha ya Kiswahili. Hili ni jambo ambalo tunapaswa kuliangazia ili tuweze kuwa na wafasiri ambao wanaweza kutusaidia sisi Wabunge kujieleza rasmi katika Bunge hili.
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
Jambo lingine la kushangaza ni kwamba hata nakala ya Katiba ambayo nimetumia, niliponukuu Kipengee cha 7, ni nakala rasimu; siyo ile ambayo tayari imefasiriwa rasmi kama Katiba ya nchi hii. Hii ni kumaanisha kwamba tangu tulipopitisha Katiba hii mwaka wa 2010, hakuna juhudi zozote zilizofanywa na Serikali kuhakikisha kwamba Wakenya wanaweza kupata katiba hii rasmi katika lugha ya kitaifa. Ni fedheha iliyoje?
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
Kiswahili ni lugha ambayo ina mashiko makuu sana katika historia ya Kenya. Kiswahili ni lugha ya kiafrika. Wengi watakubaliana nami kwamba Kiswahili kimetiririka kutoka kwa lugha za kiafrika. Ukitembea katika nchi nyingi za kiafrika utapata maneno mengi ambayo yanawiana na lugha yetu ya Kiswahili. Kwa mfano, lugha ya Kizulu kule Afrika Kusini, lugha za kizambia kule Zambia na hata humu nchini, zinawiana na Kiswahili. Mimi mwenyewe, nikiiangazia lugha yangu asilia, kuna maneno mengi sana ambayo yanawiana na Kiswahili. Sembuse kusema kwamba jina “Swahili” limetokana na jina la kiarabu ‘sawahil’ – watu ambao wanaishi katika ufuo wa bahari.
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
Jambo muhimu ni kwamba ukiitizama lugha hii, utaona kwamba haina watu ambao unaweza kusema haswa ndio watu ambao wanaweza kuienzi kama lugha zingine za Kikuyu, Kiluo, Kiluhya na kadhalika. Kwa hivyo, ni lugha ambayo inaweza kutujumuisha sisi kama Wakenya bila ya watu wengine kuhisi kwamba wao, kwa sababu ya lugha hii, wako sawa zaidi kuliko watu wengine. Ukiangazia changamoto ambayo sisi kama Wakenya na pengine watu ambao wametumia lugha za kigeni kama lugha zao za kitaifa, ni kwamba kunakua na kukanganya kidogo wakati dhana zako ziko katika lugha ile halafu wewe mwenyewe unajieleza katika lugha yako ya Kiswahili. Mara nyingi, ...
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
jinsi unavyoizungumza lugha ya Kiswahili haijalishi; hata kama umeathiriwa na lugha yako ya asili.
view
-
25 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe Naibu Spika, lahaja ya Kiswahili tunayotumia ni ya kizanzibari. Kuna lahaja nyingine za Kiswahili kama vile Kimvita, Kimtang’ata, Kipemba na kadhalika. Hata kule pwani, lugha ya Kiswahili ambayo inazungumzwa kule Mombasa ni tofauti sana na lahaja ya Kiamu, ambayo inatumika kule Lamu. Kwa hivyo, hii njia ni ya kuweza kusema kwamba watu hawawezi kujieleza kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu katika kufundisha lugha hii kule shule, kuna mtazamo wa kuisanifisha lugha – mtazamo ambao unawafanya watu kuhisi kwamba hawawezi kuizungumzia lugha hii kwa misamiati. Kwa hivyo wanaogopa. Lakini la hasha! Ninaikataa dhana hiyo. Mara nyingi sisi, kama wanasiasa, tunapoenda ...
view