All parliamentary appearances
Entries 1441 to 1450 of 1711.
-
3 Jun 2014 in National Assembly:
Okay.
view
-
3 Jun 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Speaker. But, although you may have ruled that it goes to the Departmental Committee, LAPSSET is actually a multi-inter-ministerial project. But they can consult with other relevant authorities.
view
-
3 Jun 2014 in National Assembly:
Three weeks will suffice with the input of the Leader of Majority Party. Thank you.
view
-
22 Apr 2014 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, ningependa kusimama kuunga mkono Mswada huu. Kwanza, ningependa kusema kwamba ukitathmini na kuangalia hii sheria na ulinganishe na ile tuliokuwa nayo mwaka jana, ni ishara kwamba kumekuwa na mabadiliko. Kumekuwa na uwiano wa mambo ambayo tunafaa kuyaafikia kama Taifa la Kenya. Inasemekana kwamba hii sheria itazungumziwa na Bunge zote mbili - Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Ukikumbuka, kulikuwa na tashwishi na watu wakakimbia kwa Mahakama Kuu ili ieleweke ni vipi ambavyo tutaweza kuangazia swala hili. Pia, tumeona wakati uliopita kwamba kumekuwa na malumbano kati ya yale maamuzi ambayo yanafanyika kutoka katika korti zetu na kuendelea ...
view
-
22 Apr 2014 in National Assembly:
ambazo zimewekwa kufikia mashinani kupitia serikali za ugatuzi, ni kweli kwamba zimeongezeka kwa kiasa cha asilimia 43. Lakini pia tumekuwa na mazungumzo kama Kamati ya Bajeti na Makadirio kwamba kulikuwa na kiwango ambacho kilikuwa kimependekezwa na ile Tume ya Ugavi wa Rasilmali cha Kshs279 bilioni. Tulitoka pale hadi Kshs238 bilioni. Kwa hivyo, huu mchakato lazima uendelee kwa sababu sijui kana kwamba kupunguza kule ni kutokana na majukumu ambayo yamezidi katika Serikali ya Kitaifa. Pia ukiangalia zaidi, nafikiri Wakenya wamekuwa na mwito wa kuhakikisha kwamba hakuna rushwa ambayo inajikidhiri katika maeneo ya mashinani kupitia mifumo ya serikali za ugatuzi. Lakini pia ...
view
-
22 Apr 2014 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, mwaka jana kulikuwa na tetezi kwamba Kshs16.6 bilioni zilikuwa zimewekwa ili ziweze kutumiwa na serikali za ugatuzi kama masharti fulani yangeweza kufuatwa. Kwa lugha ya Kimombo ukipenda “Conditional Allocations”.
view
-
22 Apr 2014 in National Assembly:
Kwa hivyo, katika masuala ya elimu, kuhakikisha kwamba wale ambao hawajahitimu kujiunga na shule za upili wanapata nafasi ya kupata taaluma ili waweze kujikimu katika maisha na kusaidia jamii ndiposa tuweze kuafikia Ruwaza Ya 2030, ninafikiri ni jambo la kutajiwa.
view
-
22 Apr 2014 in National Assembly:
Pia, kumekuwa na tetesi kuhusu masuala ya usalama na nafikiri jambo hili linaweza kuangaziwa ili vijana wetu waweze kupata ajira na riziki ya kila siku.
view
-
22 Apr 2014 in National Assembly:
Mhe.Naibu Spika, pia,ni jambo la kutajika kuona kwamba kuna hela ambazo zimetengwa za kuinua miradi ambayo inafaa kusaidia uchumi wetu uweze kukua kwa kiwango ambacho kinafaa. Jambo la kusikitisha ni kwamba Kenya inaorodheshwa kufikia mwezi wa Septemba kuwa na uchumi ambao ni wa nne bora zaidi katika ukanda wa Afrika. Lakini jambo ambalo tunafaa kuangazia ni, ni vipi tutaweza kuweka pesa mashinani ambazo zitawasaidia wananchi kupata ajira? Hii ni kwa sababu ukuaji wa uchumi pasipo na ajira si jambo ambalo linasaidia kwa sababu linafanya maskini wawe maskini zaidi na mabwenyenye waendelee kuwa mabwenyenye na matajiri zaidi. Kwa hivyo, ni jambo ...
view
-
22 Apr 2014 in National Assembly:
Pia, katika kiwango cha kitaifa, tumekuwa na mwito mpya kama Kamati ya Bajeti na Makadirio kwamba tunaangalia takwimu ama unapatiwa hela ambazo unahitaji lakini lazima uwe ni miradi ambayo unaonyesha kweli kwamba Wakenya wataweza kufaidika. Tungependa Bunge la Seneti liweze kuangalia jambo hili baada ya Mswada huu na ule The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view