Isaac Maigua Mwaura

Parties & Coalitions

Born

1982

Email

mwaura.isa@gmail.com

Web

www.isaacmwaura.com/

Telephone

0721864949

Telephone

0733864949

Link

@MwauraIsaac1 on Twitter

All parliamentary appearances

Entries 301 to 310 of 1711.

  • 29 Sep 2020 in Senate: Hizi fedha ziliongezeka kutoka Kshs4.7 bilioni hadi Kshs6.1 bilioni. Ni jambo la kushangaza, tulipomuuliza Waziri husika aliyekuwepo, mheshimiwa Henry Rotich, akasema ni hitilafu ya tarakirishi. view
  • 29 Sep 2020 in Senate: Swala ambalo tulijiuliza ni, je, kunawezaje kuwa na hitilafu ya karibu Kshs2 bilioni. Ripoti hii imeonyesha wazi. Mimi nachukulia huu kama wizi mkubwa wa mali ya umma. Ni pesa ambazo zimetengwa kwa huduma ama majukumu ambayo yamegatuliwa, lakini kupitia mikataba ya serikali ugatuzi tunaona vile ambavyo hivi vifaa vilvyokodiwa ni jambo kla kutamausha. Ukiangazia zaidi ya Kshs63 billioni zimetumika katika mradi huu ilhali mahospitali yetu hayana vifaa vya kutosha. Vingi vya vifaa hivi havijatumika kwa sababu hatuna wataalam wa kutosha fauka ya kwamba tumeleta madaktari kutoka nchi ya Cuba. view
  • 29 Sep 2020 in Senate: Bw. Spika, jambo hili ni la kufedhehesha ambalo tunafaa kuchukua msimamo. Kamati imeeleza kinagaubaga, shida, matatizo, madhila na majanga ya mradi huu. Lakini ukiangazia mapendekezo yao, hayana mashiko. Mapendekezo haya ni ya kijuu juu. Haya mwangazii mtu yeyote kibinafsi iwe kwamba hakuna mtu yeyote aliyefanya hatia, wawe watu wataweza kusitiliwa na sheria zinazotokana na kukinga afisi walioko. Ni vizuri tuwe tunajua kampuni zilizohusika na mradi huu. view
  • 29 Sep 2020 in Senate: Kwa mfano, kampuni hii iliweza kuweka bei ya juu kwa vifaa ambazo zinepatikana hapa nchini na kwa kiasi hiki kampuni hii ikapata pesa ambazo haingeweza kupata. Wale The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 29 Sep 2020 in Senate: wote waliotia sahihi nyaraka hizi wachukuliwe hatua. Haiwezekani tuje hapa, tuongee kama chiriku aliyekunywa maji ya chooni ilhali hakuna choshote kitachukuliwa na hotuba na marubano ambayo hayaishi. Ni lazima Bunge la Seneti liimarishe staha yake kwa kuhakikisha hii ripoti itupiliwe mbali kwa sababu ya yale mapendekezo ambayo nimetoa. view
  • 29 Sep 2020 in Senate: Baada ya hapa, tuna njia mbili. Aidha tubadilishe mapendekezo haya na kutoa masharti na msimamo ambao utahakikisha ya kwamba wafisadi hawa wamechukuliwa hatua za kisheria--- view
  • 17 Sep 2020 in Senate: Bw. Spika, naunga mkono Taarifa ambayo imetolewa na Sen. Iman kuhusu TikTok Application . Mambo hayo pia yanahusisha zingine kama vile view
  • 17 Sep 2020 in Senate: na kadhalika. view
  • 17 Sep 2020 in Senate: Tunafahamu fikra inayoendelea katika anga za kimataifa. Uchina ni nchi ambayo imeendelea sana kutokana na utengenezaji wa bidhaa nyingi. Ukiangalia bidhaa tulizonazo hapa, utapata kuwa nyingi zimetoka Uchina. Sasa wameanza kuingia katika mambo ya mtandao; kutumia technolojia katika mawasiliano. Kampuni nyingi zilizoanzishwa Silicon Valley kule Marekani zilishtakiwa katika anga za kimataifa kwa sababu ya kutokuwa na usiri wa data ambayo wanapata kutoka kwa watu wote ulimwenguni. view
  • 17 Sep 2020 in Senate: Nakubaliana na Sen. Iman kwamba ni vizuri kuangalia jinsi ambavyo data inatumiwa hususan kwa mambo ya ununuzi katika soko huria zilizoko ulimwenguni. Hata hivyo isiwe kama vita kati ya iPhone na Huawei. Hii ni kwa sababu Uchina inaingiliwa kwa sababu wameanza kuchukua soko ambazo zilikuwa zimedhaminiwa na nchi za kimagharibi. Isiwe ni kisingizio cha kuwaharibia jina kwa sababu nchi kama Marekani ina bejeti maalum ya kupinga utumiaji wa bidhaa kutoka Uchina. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus