Her constituents in Laikipia County fondly call her "Mama Amani", long before she joined politics, she was already a peace crusader in a county where cattle rustling is the order of the day.
9 May 2017 in National Assembly:
Ukiangalia huko Turkana, watu wanalia njaa. Hii ni kwa sababu hatujaweka mikakati yoyote. Inafaa tuweke mikakati kwa sehemu kame za Kenya na tuangalie kama tunaweza kupata maji. Tumeambiwa sehemu kama Turkana ziko na maji ya kutosha lakini nani anafikiria vile tunaweza kupata hiyo maji ili watu wapate kukuza chakula? Inaonekana kama hakuna jambo linalotendeka. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
9 May 2017 in National Assembly:
Pia afisi ambazo zinashugulikia mambo yakulipisha kodi zinafaa kuangalia ni bei ya nini ambayo watapunguza hata kama ni mwaka huu peke tu. Hili si jambo ambalo litakuwepo kwa muda mrefu lakini ni lazima tuangalia mikakati ya kupunguza bei kwa muda mrefu. Pia tunapaswa kuwaangalia wakongwe huku nchini ili kutoka miaka 65 waweze kupata fedha za matumizi na kulipiwa malipo yaNHIF ili wapate matibabu kwa urahisi. Hawa ni watu ambao hawajiwezi na tungetaka wawe wakienda hospitali bila kulipa hela yoyote. Umri umewakabili na hawawezi kuajiriwa tena na hawana nguvu ya kufanya kazi. Sisi ambao tuko kwa Bunge hili ambako sheria zinatengenezwa, ...
view
9 May 2017 in National Assembly:
Huu si wakati wakulaumiana lakini ni wakati wa kuangalia kama Wakenya wako na chakula cha kutosha. Tukiangalia wakati uliopita, ufisadi umechukua sehemu kubwa zaidi. Wengine wameweka pesa kwa magunia na kuzificha katika godoro wanazolalia ndani ya nyumba. Hakuna pesa ambazo zinazunguka nchini. Hakuna hata uajiri. Kwa hivyo, lazima tuuangalie upande wa ufisadi. Lazima jukumu la sheria liwepo. Tumewaweka pale watu wa sheria ili wachukue lile jukumu sawasawa na kwa ukamilifu. Nikimalizia, ningependa kusema ya kwamba Kenya inaweza kujipatia chakula ikiwa kuna mikakati ambayo itatengenezwa na zile ofisi zote zinazohusika na ukulima na ushuru. Hizo zote zikihusika, tunajua chakula chaweza kupatikana ...
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Hon. Spika, nashukuru kwa kunipatia fursa hii kuchangia mjadala wa lala salama tukielekea kwa likizo. Leo ni siku kubwa zaidi kwani tumepitisha Miswada mitatu muhimu zaidi katika Kenya yetu. Miswada hii ni muhimu zaidi kwa sababu tumekuwa na Miswada mingine mizuri lakini hatujapitisha Miswada kama hii inayohusu uchaguzi na kuhamahama vyama. Tungepoteza mwelekeo wakati sisi sote tulikuwa tumekataa, lakini kwa kuwa na uongozi mwema ambao uko katika Kenya, tukihusisha Rais wetu, naibu wake na kinara wa upande ule wa wasio wengi, tumefanya vyema. Pengine hatutajua matunda ambayo tumevuna leo lakini tunajua ya kwamba tuna matunda ambayo tutaona yakivunwa. Huu ni ...
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ambayo nimefurahia. Tutapata likizo leo ya kwenda nyumbani kwetu. Ninashukuru kwa kazi ambayo Bunge limefanya kwa sababu tumepata Kamati ambayo itaangalia mambo ya IEBC ambayo imekuwa ni shida zaidi katika nchi yetu.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Ninasema imeleta shida kwa sababu tumepoteza mali kwenye vurugu ambazo zimekuwepo. Pia, tumepoteza maisha. Ile Kamati itawajibika kumaliza vurugu na tuko na imani kwamba tutapata suluhisho la kudumu na hakutakuwa vurugu na maandamano ambayo hata wazee wanashiriki na kutembea mitaani. Hili litakuwa jambo la maana katika Kenya yetu na tunashukuru zaidi. Tunajua kwamba ripoti hii itakapoletwa hapa Bungeni, itajadiliwa vilivyo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
6 Jul 2016 in National Assembly:
Wabunge wengine walikuwa na shauku kuwa jambo hilo haliko sawa katika sheria za Bunge. Lakini litakaporudi hapa wakati wa pili, tunajua litajadiliwa. Ikiwa ni jambo ambalo litahitaji kupitishwa, itakuwa ni wakati wao wa kuzungumza yaliyo ndani yao. Kwa hayo yote, nashukuru.
view
24 Mar 2016 in National Assembly:
Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mswada uliopo mbele yetu wakati huu wa kusawisha idadi ya akina mama katika Bunge hili ni muhimu sana. Tunafurahi tunapofikiria jinsi tutakavyoweza kuwaongeza wanawake katika Bunge. Sio katika Bunge peke yake bali pia katika ajira na hata huko mashinani wanaweza kusimamia mahali popote. Tunafaa kuwahusisha akina mama. Tunapaswa kujua kuwa akina mama ndio wenye idadi kubwa zaidi. Sisi Wabunge tunapigiwa kura na akina mama. Pili, sisi sote tumetoka kwa akina mama. Ni wazazi wetu, dada zetu na watoto wetu. Kwa hivyo, tunapowafikiria akina mama, tuangalie kama sisi Wabunge tuna watoto wasichana. Je, tungetaka watoto ...
view
24 Mar 2016 in National Assembly:
kulingana na Malengo ya Milenia. Muda wa malengo haya utakapotimia, lazima idadi hii iwepo kwa sababu sio Kenya peke yake bali dunia nzima. Sisi tutaweza kuachwa vipi nyuma? Sisi akina mama hatuombi. Ni jambo ambalo linaendelea. Ni haki yetu pia sisi kupatiwa nafasi. Katika hili Bunge, tunafurahi sana kwani tunaungwa mkono na wenzetu wanaume ambao wana watoto wasichana ambao wangetaka waingie katika Bunge hili na pia katika Bunge za Kaunti. Tunaomba tupatiwe nafasi na tutawaonyesha kuwa akina mama wanaweza. Akina mama wanaweza kushikilia nyadhifa zozote. Tunataka akina mama huko mashinani tunakotoka wasijihisi kama wameachwa nyuma. Wakijihisi kama wameachwa nyuma ilhali ...
view
24 Mar 2016 in National Assembly:
Naunga mkono. Kwa hivyo, sisi tunangoja wakati ambao Mswada huu utakapopitishwa tuwe tumepata ile sehemu yetu. Asante.
view