Jane Agnes Wanjira Machira

Her constituents in Laikipia County fondly call her "Mama Amani", long before she joined politics, she was already a peace crusader in a county where cattle rustling is the order of the day.

All parliamentary appearances

Entries 71 to 75 of 75.

  • 18 Nov 2014 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mhe. Shebesh katika hili jambo. Jambo hili lilituweka katika picha mbaya sana kama kina mama. Pia limeweka picha mbaya zaidi kwa wazee; hata Wabunge walio katika Bunge hili, picha yao itachukuliwa kama wazee ambao wana picha kama ile ikiwa hawataunga mkono huu mjadala. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kiazi gani cha nguo ama ni urefu gani wa nguo ambao kina mama wanahitajika kuvaa? Ikiwa kuna urefu wowote, basi hatuwezi kuelezwa na makanga . Ni sisi Wabunge ambao tunapaswa kupitisha sheria hiyo. Ni wanaume wangapi leo wanavaa suruali ambazo ni nusu ... view
  • 18 Nov 2014 in National Assembly: Wanaume, mwataka kujifurahisha na watoto wetu? Mwataka kuona nini ambacho hamjawahi kuona? Ikiwa kina mama wazee walioishi miaka ya 60, mama yangu alikuwa akivaa nguo fupi na sikuona hata yule mtoto wa kijiji akienda kumwangalia chini na walikuwa wakivaa nguo fupi, mbona nyinyi na mmesoma mnafanya hivyo? Mwataka kuwa na tamaa ambayo haijulikani ni ya aina gani. Naomba--- view
  • 3 Apr 2014 in National Assembly: Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa ruhusa ili nami niongee kidogo kuhusu Hotuba ya Rais. Rais Uhuru ametueleza kuhusu mpangilio wake wa kazi ili kutujulisha mambo anayofikiria kuhusu nchi yetu. Rais Uhuru ameshateua watu ambao tunaweza kusema ni watu ambao kazi yao ni ya mkono katika nchi nzima, nao ni Mawaziri. Tunaposema kwamba Rais hafanyi kazi labda kuna watu ambao wamesinzia katika nyadhifa zao. Tusitupe mawe kwa Rais tukisema kuwa hajafanya kazi yoyote. Rais alitujulisha mpangilio wake katika usalama. Aliteua nyumba kumi. Hii itatusaidia katika kuimarisha usalama. Huenda katika miji nyumba kumi isifaulu sana lakini mashinani najua zinaweza. ... view
  • 23 Apr 2013 in National Assembly: (Hon. (Ms.) Machira): Shukrani, Mhe. Spikar. Ni pongezi kwako kwa kuchaguliwa kama Spika wetu. Nikiongezea, ningependa kusema kwamba nilikuwa afisa wa uhusiano mwema na ndio sababu hakukuwa na fujo yoyote wakati ulichaguliwa. Nasema ahsante pia kwa wabunge wenzangu. view
  • 23 Apr 2013 in National Assembly: Kulingana na ile Hotuba ya Rais, nasema hongera. Ilikuwa Hotuba nzuri sana lakini nataka tupige hatua katika mambo ya ulinzi na usalama katika sehemu ambayo nimetoka. Kabla zijasema hivyo, ningependa kutoa hongera kwa watu wa Laikipia kwa kuchagua huyu mama ambaye anaitwa Jane Machira. Niliapa mbele ya Bunge hili kwamba nitawatumikia wote. Tukiangazia ulinzi na usalama, Kenya ilifanya vizuri sana wakati ilielekea Somalia na kuhakikisha amani katika nchi hiyo. Lakini sisi wenyewe tunaweza kuwa tunakunywa maji, ili hali majirani wetu wanakunywa pombe za kifahari. Katika sehemu ya Laikipia, majirani wetu wamekuwa wakipigwa na kukipigana wenyewe kwa wenyewe na hata kuuana ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus