27 May 2025 in Senate:
Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, naunga mkono Taarifa iliyoletwa na Kiranja wa Walio Wengi Bungeni kuhusu mfumo mpya wa afya wa SHA. Ni vizuri ijulikane ya kwamba, wakati tulipopata Katiba mpya, watu ambao walikuwa wakifanya kazi katika manispaa na gatuzi zingine, walijumuishwa katika gatuzi mpya. Vile vile, itakuwa bora zaidi wafanyakazi ambao walikuwa wa NHIF wajumuishwe katika mfumo mpya wa SHA, ndiposa hawa wafanyakazi wawe na uzoefu na walete utaratibu mpya katika sehemu ambazo hazifanyi vizuri. Kikatiba, itakuwa vibaya kuwadhulumu hawa wafanyakazi ambao wamefanya kazi na mfumo wa NHIF. Kisheria, wanapaswa kujumuishwa na kuendelea na kazi ...
view
14 May 2025 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nitaanza kwa kuvulia njuga Hoja hii ikiwa na marekebisho. Ni jambo la kuvunja moyo sana ukitembelea gatuzi unapata ina na maspika wawili, karani wawili na vikao viwili, ilhali ni gatuzi moja.
view
14 May 2025 in Senate:
Bw. Spika, ikiwa Spika ametimuliwa kutoka kwa kiti chake, hana haja yoyote kuwa na kikao chochote mahali popote. Lakini hata tukiwa tunasema hivyo, nimeangalia nikaona ya kwamba kuna hizi sehemu ambazo kwa lugha ya kiingereza wanasema zimegazetiwa na ambazo zinapaswa kutumika kama vikao maalum vya Bunge la Kaunti ya Nyamira.
view
14 May 2025 in Senate:
Idara za Serikali zinachangia kuchanganya wananchi wa Kenya. Unapata ya kwamba mahali ambapo hiki kikao cha Wawakilishi Wadi wa Nyamira wamekutana, wanatumia sheria. Nimemsikiza Mwenyekiti akituambia ya kwamba tayari hiki kikao chenyewe ni gazetted na kuna namba ya Gazeti Rasmi ambayo imepewa.
view
14 May 2025 in Senate:
Bw. Spika, ni kama tuna idara tofauti za Serikali. Kuna idara ambayo inasema ya kwamba ndiyo, kuna wale ambao wanapaswa kuwa mashinani na kuna wale ambao wako katika ile sehemu ambayo imetengwa maalum ya hawa wawakilishi wadi kukutana na kufanya vikao vyao. Idara za Serikali zinapaswa kuwa zinawasiliana, si kupeana mambo kiholela. Kwangu inakaa ni kama ni miujiza kama si maajabu.
view
14 May 2025 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nimemsikiza Seneta kutoka Nyamira akielezea yale mambo ambayo yanatendeka huko. Unapata ya kwamba kama ni hela, zinatoka na zinapeanwa kwa gatuzi hizi mbili. Ikiwa pesa zinatumika na kaunti hiyo kwa njia ambayo haifai, basi wanapaswa kurejesha.
view
14 May 2025 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate
view
14 May 2025 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nashindwa ni kwa nini tunaandika kwa mate ilhali kuna wino. Tusiwe tunatoa mapendekezo ya kupoteza muda. Wakati mwingi tunatoa mapendekezo ambayo hayafuatiliwi. Kamati husika imekuwa ikishughulikia jambo hilo kwa zaidi ya siku 45 lakini watu hawajapata majibu. Isiwe sisi kama Seneti tunatoa mapendekezo ambayo hayatiliwi maanani.
view
14 May 2025 in Senate:
Kiingereza hunichanga. Nitafurahi akinijuza kwa Kiswahili.
view
14 May 2025 in Senate:
Mr. Temporary Speaker, Sir, I have no problem being informed by Sen. Wakili Sigei.
view