29 May 2025 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir, for this opportunity to comment on the Statement by the Senator for Wajir on implementation of ECDE centres in Wajir County. Problems that are being faced by Wajir are not unique to that county alone, but are replicated across the whole country. Right now, we are doing an inquiry on the level of implementation of ECDE centres, Vocational Training Centres (VTCs) and libraries, which are devolved. Preliminary findings are that our ECDE centres and VTCs, which are devolved, are suffering. They are in deplorable conditions because governors have elected to leave out functions that are ...
view
14 May 2025 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa fursa hii ili kuchangia na kuunga mkono moja kwa moja ripoti hii ya kamati kuhusu Kaunti ya Nyamira. Swala hili liliibuka wakati Gavana wa Nyamira alipokuja katika Kamati ya Bajeti na Fedha ambapo tunaketi na Seneta wa Nyamira, Sen. Omogeni. Tuligundua kwamba kuna vikao viwili tofauti. Kikundi cha kwanza kinaketi katika Bunge la Kaunti ya Nyamira lililo mkabala na Jengo la KIE na bunge lingine linaketi mahali tofauti tofauti. Linaitwa Bunge Mashanani.
view
14 May 2025 in Senate:
Ningependa kushukuru Sen. Omogeni kwa kuleta Taarifa hii ambapo aliuliza maswali matatu. Kwanza, alitaka kujua ni kikao gani kinachofaa kuketi katika Bunge la Kaunti ya Nyamira ambalo liko katika Taarifa ya Gazeti la Serikali. Pili, alitaka kujua uhalali wa sheria ambazo zinapitishwa na mabunge yote mawili, ikiwemo bajeti ya ziada. Tatu, aliuliza Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali njia ambazo zilitumika kuchagua Spika na Katibu wapya.
view
14 May 2025 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, kamati hii imefanya kazi nzuri ingawaje imepata mapigo. Najua wewe ni Memba wa kamati hiyo. Kwa kujibu swali la kwanza, wamesema kuwa bunge ambalo ni halali ni lile ambalo linaketi mkabala na Jengo la KIE huko Nyamira. Kwa kikundi kinachofanya vikao vyake mashinani, hakukuwa na resolution yoyote ya Bunge la Kaunti ya Nyamira.
view
14 May 2025 in Senate:
Swali la pili kuhusu uhalali wa sheria zinazopitishwa na kikundi kinachoenda mashinani limejibiwa---
view
14 May 2025 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate
view
14 May 2025 in Senate:
Swali hilo limejibiwa na mabadiliko katika Hoja ya kwamba sheria zote zilizopitishwa na bunge hilo ambalo siyo halali basi pia siyo halali. Nakubaliana mia kwa mia na pendekezo hilo. Je, sheria hizo ambazo tunasema siyo halali zitachukuliwa namna gani? Kwa mfano, kuna bajeti ya ziada, ama supplementary budget, ambayo ilipita na tayari inatumika. Je, wale ambao wanatumia pesa watachukuliwa hatua aina gani?
view
14 May 2025 in Senate:
Sen. Omogeni alitaja mambo ya Taita-Taveta. Ni kweli kuwa kuna shida katika bunge hilo ingawaje siyo kama Bunge la Kaunti ya Nyamira kwa sababu kule Taita- Taveta, Spika alibanduliwa kupitia kwa impeachment kisha akaenda kortini. Alipoenda kortini, saa hii aliyekuwa Naibu wa Spika ni Acting Spika. Tunafaa tuangalie sheria ili kukiwa na kesi katika korti itachukua muda gani ili yule ambaye ni Naibu wa Spika awache kuwa Acting Speaker? Ikiwa kesi itachukua muda sana kama hii ya Nyamira County, huo mkanganyiko unachukua muda mrefu na katika sheria hakuna Acting Speaker . Kuna Spika na wakati Spika ametolewa lazima kuchaguliwe Spika. ...
view
14 May 2025 in Senate:
Asante, Bi. Suka wa Muda.
view
14 May 2025 in Senate:
The Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) inafaa iingilie kati na kuangalia uhalisia na maadili yanayotokana na hilo jambo. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono hii ripoti. Ni kweli kwamba, lazima iwe ni interim kwa sababu bado wanataka kwenda kule ili kuangalia kama wanaweza suluhisha yale mambo yaliyoko huko kisiasa. Nashukuru.
view