3 Oct 2019 in Senate:
Asante Sana, Bw. Spika; na pia asante sana, Sen. Mutula Kilonzo Jnr., kwa kupiga makofi vile nimekuja kuzungumza.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili kuunga mkono Mswada huu ulioletwa na Seneta wa Kirinyaga, ambao ni Mswada muhimu sana. Nimefurahi kwamba huu ni mojawapo ya Miswada ambayo magavana wetu wameweza kuifikiria na, kupitia wenzetu, kuuleta Mswada huu. Gavana Mwangi wa Iria ndiye aliyeuleta Mswada huu katika Bunge la Seneti kupitia Seneta mwenzetu. Ingawa kuna vipengee kadhaa ambavyo lazima tutaangalia, kukagua na labda kuleta mabadiliko kwayo, huu ni Mswada mzuri sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, ni kweli kwamba wachuuzi wetu wa biashara za reja reja ni wengi sana katika miji mikuu au miji mbali mbali kama Nairobi, Kisumu, Mombasa, Nakuru na kwengineko. Hata hivyo, hawa wachuuzi wamedharauliwa kwa muda mrefu. Pia ni kweli kwamba serikali za kaunti na pia Serikali Kuu hapo awali kabla tuwe na mfumo wa ugatuzi, badala ya kusaidia wafanyibiashara kustawisha biashara zao, imekuwa ikiwadhulumu na kuwafinyilia chini. Hilo ni jambo ambalo halifai. Bw. Spika, ukitembea kila mahali katika Mji wa Nairobi, utapata vijana wetu na kina mama wakijaribu kutafuta riziki yao; wakitafuta njia ya kupeleka chakula nyumbani. Lakini kila ...
view
3 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, nakubali kuarifiwa na Seneta wa Bungoma.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Asante sana, Sen. Wetangula. Hiyo ni taarifa ambayo nilikuwa nayo hapo awali. Ningependa kumweleza kuwa shida ya wachuuzi wetu Nairobi haswa sio tu kiwango cha ada lakini wanalipa hizo hela na hawapati huduma.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, shida yao kubwa ni kwamba ukienda soko za Marigiti, Gikomba ama popote pale, hawana shida na kulipa ada, bora soko zisafishwe, wapate usalama na wasi dhulimiwe na serikali. Zaidi ya hayo, sio vizuri kwamba mtu analipa ada na hizo hela hazitumiwi kwa njia ambayo inafaa.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Shida ya pili ni kwamba labda itakuwa ni vizuri wakipunguza hiyo ada. Hii ndio sababu ninaunga mkono Mswada huu. Baada ya huu Mswada kupitishwa hapa katika Bunge la Seneti, tunataka Mswada kama huu upitishwe katika County Assembly ya Kaunti ya Nairobi. Mimi mwenyewe nitawapatia hao wawakilishi wa Ward waweze kupitisha Mswada kama huu.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Juzi nilisema siyo sheria tu ambayo ina tufunga mikono tusiweze kuhudumia watu vizuri. Wakati mwingine ni ukosefu wa utu na kwa kiingereza tunasema “commonsense”. Hakuna sheria ambayo ita kufunza kufikiria maslahi ya mtu wa kawaida au ubadilishe roho yako. Juzi nilikuwa na wachuuzi wangu wa Westlands ambao hapo awali walikuwa katika soko la Westlands. Wali tolewa na kuambiwa, “Sasa tunajenga, kaeni hapa karibu na barabara”. Walitolewa na kuwekwa kwa barabara. Jengo hilo limechukuwa zaidi ya miaka kumi likijengwa.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Juzi tulisukuma maneno na wakaendelea. Lakini baadaye wakafurushwa na serikali hiyo wakiambiwa kwamba inataka kujenga barabara. Hadi wa leo hiyo barabara haijaanza kujengwa na wako nje. Si ingekuwa bora wamalize kujenga soko, wawa hamishe hapo halafu ndio wajenge barabara? Haiwezi kuwa kwamba hatuwafikirii hawa watu wa kawaida. Mama akinyang’anywa bidhaa zake anaambiwa alipe Shilingi 20,000 ndiyo apate bidhaa zake aweze kuendelea na biashara. Ni ukosefu wa utu hata si ukosefu wa sheria. Hawa watu tunasesema washindwe! Ama vile tunavyosema nyumbani riswa!
view
3 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, shida ambayo tuko nayo ni ukosefu wa mpangilio thabiti kwa sababu kuna wale wachuuzi rejareja na pia wale ambao wana duka. Ukiangalia hao ambao tunaita hawkers ama wachuuzi wa bidhaa rejareja, sana sana wanapatikana karibu na stesheni za matatu ama pahali pa uchukuzi. Hii ni kwa sababu watu wengi wakitoka kazini jioni, wakitembea kwenda kupanda matatu, wakiona nyanya mbili hapa na vituguu wananunua. Ama mtu ataona sketi au viatu vya pumps amnunulie mke wake. Ni lazima wawe hapo karibu na sehemu za usafiri.
view