Johnson Arthur Sakaja

Parties & Coalitions

Born

1985

Email

jsakaja@gmail.com

Link

@SakajaJohnson on Twitter

Johnson Arthur Sakaja

Nairobi Senator; Chairman of the Kenya Young Parliamentarians Association; National Chairman - TNA (2012-2016).

All parliamentary appearances

Entries 2621 to 2630 of 5036.

  • 3 Oct 2019 in Senate: Kuna nafasi ambayo ina tosha katika jiji la Nairobi na kaunti zingine kuweza kusema hapa kutakuwa na wachuuzi rejareja na pale pengine duka. Haifai kuwa tusadie hawa halafu tuwadhulumu hao wengine ambao pia wanalipa ushuru kwa serikali. Hii inatokana na ukosefu tu wa mpangilio. Ni rahisi kufanyika na imefanyika katika mataifa mengi ambayo tumetembelea; ambayo yako katika kiwango kimoja na Jamhuri ya Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Bw. Spika tunasema ya kwamba tuwe na mangilio na orodha ya hawa wachuuzi. Wanafaa wapewe nambari ili tujue wachuuzi wagani ni wa Moi Avenue na watakuwa wanakuja kufanya biashara siku gani. Barabara hii labda itakuwa inafungwa siku zingine ili waweze kuja kuuza hapo. Tunafaa kuwasaidia kukuza biashara zao. view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Bw. Spika, jana nilikuwa upande wa Waiyaki Way nikaenda kula kwa kibanda pale karibu na Njuguna’s, kando ya barabara. Hao wachuuzi waliniambia ya kwamba wanadhulumiwa na kila siku wanafukuzwa. Wako mahali ambapo ni kiwanja ambacho kiko bure, hakitumiki kwa kazi yoyote. Hakuna nyumba inajengwa hapo au barabara inayopita hapo. Kuna wafanyi biashara watano au sita hivi ambao wameajiri zaidi ya akina mama na vijana 90. Lakini hivi karibuni utasikia wamefukuzwa kwa sababu ni wachuuzi wa bidhaa rejareja na hapo pahali patakaa tu wazi bila kuleta faida kwa uchumi. Hao akina mama na vijana wataenda wapi? view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Kama kungekuwa na serikali ya Kitaifa ama ya Kaunti ambayo inafikiria maslahi ya watu wake, ingechukua watu hao iseme: “tutawajengea hapa vibanda, tupige rangi, tuwasaidie na mahali pa kuweka bidhaa zenu.” Ni nini mihimu, ni kuona tu nafasi ziko wazi ama watu wetu kupata ajira? Haya mambo ya kupamba mazingira tutafanya baada ya vijana wetu kupata ajira. view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Kuna wachuuzi ambao walikuwa Outer Ring Road na wale wa Mutindwa. Walifukuzwa kwa sababu walikuwa kwa ukuta karibu na shule. Wale wa Kibera hapo kwa DC, walifukuzwa na vibanda vyao kubomolewa. Walifurushwa bila kupewa fidia au pahali pengine pa kufanya biashara yao. Wamebaki hapo nje kwa sababu ilisemekana kwamba walikuwa wanafanya kuwe na ukosefu wa usalama katika shule. Lakini kwa sasa vile wamekosa ajira, si ukosefu wa usalama utazidi? Ni lazima tubadilishe vile tunavyofikiria kuhusu hawa watu wa kawaida. view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Nimefurahi ya kwamba tumeweza kujenga, pamoja na Banki ya Kitaifa - World Bank - sio kila neno unaweza kubadilisha kwa Kiswahili - tumeweza kujenga soko upande wa Kangundo Road ambapo tunataka waweze kuingia wote. view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Asante sana. Ni vile tu katika hii Bunge hatujakubali sheng . Tungeweza kukubali sheng, ningepeleka watu wa Nairobi na “ radaa” ama na “ rieng”. Lakini sasa kwa sababu sheng haikubaliki ni lazima nijaribu kuzungumza kama Mhe. Faki. Lakini kweli, Benki ya Dunia pamoja na Serikali kuu tumeweza kujenga soko kubwa hapo Kangundo Road. Tayari tumeanza kuona ufisadi ukiingia kwa sababu wale ambao walikuwa wametolewa Outer Ring Road, Mutindwa na mahali pengine--- Kulikuwa na orodha ya wale ambao walikuwa wanapaswa kuwekwa katika soko hiyo lakini inaonekana hizo orodha zimebadilishwa. Ningependa kueleza watu wa Nairobi kuwa hatutakubali hii ifanyike. Wale ambao ... view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Bw. Spika kuna vipengee kadhaa katika Mswada huu ambazo lazima tuta badilisha. Sioni sababu ya Serikali kuu - naomba Sen. Faki anisikize kwa sababu yeye ndiye anakosoa Kiswahili- iwe ndiyo inayochukua orodha ya wachuuzi. Mbona mnataka orodha ya wachuuzi? Kwani kuna orodha ya wafanyibiashara aina tofauti? Hakuna haja hiyo ya orodha iwe katika Serikali kuu. Lakini itakuwa ni vizuri serikali za kaunti ziweze kujua kwa minajili ya kupanga na kuwezesha usalama. view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Ya pili, lengo letu kuu la kuleta sheria hii ni kuwapa wale ambao wako katika bunge za kaunti nafasi ya kuiga Mswada kama huu. Tusitoe hii kazi ya kuangalia mambo ya uchuuzi kutoka serikali za kaunti na kuzileta katika Serikali kuu kwa sababu mkiweka vizuizi vingi na mpangilio mkubwa sana wa kuweza kuwasajili hamtakuwa mnasaidia. Mnataka yule mama ambaye ako Kamulu ama Kawangware, aanze kuja hapa katikati mwa jiji la Nairobi kutafuta Mkurugenzi wa idara fulani ili kusajiliwa? Hapana! Mnawasumbua. Wacha watu wafanye kazi walipo. Serikali za magatuzi zinafaa kuenda pahali walipo. Kwa mfano, Serikali ya Jiji la Nairobi inafaa ... view
  • 3 Oct 2019 in Senate: Hiyo sio haki. Lazima tuangalie jambo hilo ili kumwezesha mwananchi wa kawaida kupata mikopo ambayo anaweza kulipia kwa kiwango cha chini cha riba. Namsihi Sen. Kibiru na Kamati yake wabadilishe annual licence ili leseni zilipiwe kila mwezi au kila wiki. Ni vyema kuwe na Kipengele ili kutengwe pesa ambayo itatumiwa kuhakikisha kwamba pahali wachuuzi wanafanyia kazi pana safishwa na kuna usalama. Nikimalizia kwa sababu nimezungumza kwa muda mrefu kwa lugha ya Kiswahili, kuna Miswada mingi ambayo tumepitisha katika Seneti ambayo imelala katika Bunge la Taifa. Hili ni jambo la kusikitisha sana. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus