27 Mar 2019 in National Assembly:
Kwa mfano, ukitoka kwa nyumba kwenda kujenga nchi na unaporudi nyumbani uwe huna hata mkate uliobebea wanao, hilo ni jambo baya. Ni vema sisi kama Bunge tulichukulie hili jambo kuwa la dharura na kuhakikisha kuwa hawa wazee tunawasaidia ili waweze kupata mshahara kama wafanyikazi wengine nchini. Kwa hayo machache, naunga mkono hoja hii.
view
24 Oct 2018 in National Assembly:
Shukrani, Mhe. Spika kwa kunipa hii nafasi. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Imekuja kwa wakati ufaao. Shule nyingi haswa za upili wakati huu zilianzishwa kama shule za msingi. Kwa mfano, kuna shule moja kutoka kwangu ambayo imeanzishwa kwa ekari moja ya shamba. Ukiangalia mahitaji na majengo ya shule hiyo, watoto wanahitaji mahali pa kuchezea. Mahali pa kuchezea kama uwanja wa mpira utachukua kiasi cha ekari moja ya shamba. Kwa hivyo, hii ni Hoja iliyokuja kwa wakati unaofaa. Serikali yetu inafaa kuweka sheria kwa sababu ya upanuzi wa shule zetu. Naunga mkono Hoja hii. Ahsante.
view
8 Aug 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Naunga mkono Ombi hili kuhusu mateso ambayo wakulima wetu wanapitia. Ni kweli mkulima wetu anapitia mateso mengi kwa sababu unapolima shamba lako, unatarajia kupata mavuno kama vile sisi tunavyokuja Bunge tunatarajia tupate mshahara wetu. Wakulima wa Kenya wanaendelea kupata mateso awe ni mkulima wa miwa au wa mahindi kwa sababu hapati mavuno ambayo anatarajia. Hili ni jambo ambalo tunafaa kulichukulia maanani kwa sababu mkulima akilima shamba lake anategemea mazao hayo kufanya kazi, kwa mfano, kulipia watoto wake karo ya shule na kulima shamba tena arudishe mazao ndani. Si vyema Serikali tukufu iwache wakulima kama hao wateseke. ...
view
8 Aug 2018 in National Assembly:
Lakini, Mhe. Spika, wote ni wakulima.
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Spika. Lazima sisi kama Bunge tuchukulie hili jambo kwa njia inayotakikana. Ukiona jambo linaguza maisha ya mwanadamu, ni lazima sisi kama Wabunge tulichukulie hatua ambayo inatakikana. Maneno ya sukari yameongewa kwa muda mrefu katika nchi hii. Mimi kama Mbunge ambaye anatoka eneo ambalo linakuza miwa, wakulima wa miwa wanateseka. Kwa sasa, kiwanda cha Mumias kimekufa kwa sababu watu katika nchi hii wanatoa sukari nje kwa kiwango kikubwa hadi ile ambayo inatengenezwa katika viwanda vyetu haitumiki. Ya pili, unaona ya kwamba ripoti imetolewa jana na mahabara ya Serikali ya kuonyesha ya kwamba hiyo sukari iko na sumu. Ikiwa ...
view
20 Jun 2018 in National Assembly:
kuleta sukari katika nchi hii kwa njia ambayo haitakikani. Hatutaki tusaidie majangili wa kuleta sukari na kuharibu uchumi wa nchi hii.
view
29 Nov 2017 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kuongea katika Jumba hili la Bunge, ningependa, kwanza, kushukuru watu wangu wa Matungu kwa kunichagua kuwa mwakilishi ama mjakazi wao katika hili Nyumba Kuu. Nikiunga mkono mapendekezo ambayo tunajadili kuhusu barabara zetu, naunga mkono Mheshimiwa mwenzangu ambaye ameongea hivi karibuni kwamba tusiongee juu ya barabara za mijini peke yake. Barabara za mashambani pia ziongezwe kwa mpangilio huu kwa sababu Kenya inakua kila siku. Barabara zetu kuu zimekuwa na shida, si ya Mombasa peke yake. Wale tunakaa sehemu hii ya upande wa Mombasa Road tuko na shida tunapokuja ...
view
29 Nov 2017 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
29 Nov 2017 in National Assembly:
Nikiongezea nguvu kwa mwenzangu Mheshimiwa aliyesema ya kwamba wale wanaohusika na maneno ya sheria hawafanyi kazi yao; wamelala kwa kazi yao. Barabara mbili ambazo zilitengenezwa hivi juzi, barabara ya Eastern Bypass na Southern Bypass, zilitengenezwa kwa sababu ya kuondoa malori makubwa makubwa kupitia sehemu ya mijini. Lakini hata sasa unapotoka nje ya Bunge hili usimame utazame barabara kuu ya Uhuru Highway, utaona ya kwamba malori makubwa yangali yanatumia hii barabara. Badala ya kutumia ile barabara mpya inayopitia sehemu ya Southern Bypass, zingali zinakuja hadi mjini. Ingekuwa wale ambao wanatilia mkazo wanaona ya kwamba sheria inatumika, hatungekuwa na jambo kama hili. ...
view