Kalembe Ndile

Full name

Kalembe Richard Ndile

Born

16th April 1964

Post

P.O. Box 255 Kibwezi, Kenya

Telephone

0722 352009

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 28.

  • 13 Sep 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, pia nami ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale ambao wameuchangia Mswada huu. Ningependa kusema kwamba sisi upande wa Serikali ni lazima tujifunze kusikizana na kuelewana. Hilo ni jambo muhimu sana. view
  • 13 Sep 2007 in National Assembly: Mama akitaka wazee na watoto wasile, yeye hutia chumvi nyingi katika chakula. Yeye hukitia chakula chumvi nyingi kikiwa jikoni na kukichemsha, ndipo hata ukiiosha hiyo nyama, haiwezi kulika. view
  • 13 Sep 2007 in National Assembly: 3960 PARLIAMENTARY DEBATES September 13, 2007 Kwa hivyo ni vizuri wakati mwingine tuwe tunaelewana kabla ya kuleta Miswada hapa. Inafaa tujue vile tunavyofanya kazi, na hilo litaisaidia nchi hii, kwa sababu sitaki kuwa katika upande ambao unashindwa kila wakati katika mambo ambayo tungeshinda. Ahsante sana! view
  • 1 Aug 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, nasimama hapa kupinga hii Hoja. Nataka kumkumbusha rafiki yangu, Bw. Wamwere, kwamba Yesu asingalikufa, asingalisamehewa dhambi. Kwa hivyo, ulikuwa ni mpango wa Mungu kumleta mwanawe hapa afe ili tusamehewe dhambi. Nashukuru kwa sababu juzi nilimwona Agwambo akiombewa na wachungaji. Mtu akiamua kutenda maovu--- Najua kuna korti ambalo huchunguza kama aliua au la. Ikiwa aliua kwa bahati mbaya, korti lina uwezo wa kumsamehe, lakini inaweza kuwa alipanga, kama waliotaka kupindua Serikali na tukawapoteza watu wengi. Watoto wa vyuo vikuu walikufa, na hata watu wengine, ambao hawakuwa na hatia. Ni nani aliowaongoza? Hata juzi nilifikiri Agwambo angeombewa na hao ... view
  • 19 Jul 2007 in National Assembly: Wewe! Wewe! view
  • 19 Jul 2007 in National Assembly: Wewe wacha--- view
  • 11 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, tunapata majibu yote kutoka kwa maofisa wetu. Kama hatujapata majibu yanayofaa, kuna uwezekano wa kuahirisha kujibu hili Swali mpaka wakati tutakapokubaliana na wao. Kwa hivyo, hii haimaanishi kwamba hatuna majibu, lakini ni lazima tutoe majibu sahihi. view
  • 4 Jul 2007 in National Assembly: Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. view
  • 4 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ukinipa hiyo nafasi, naweza hiyo kazi ya kumwondoa kama huwezi! view
  • 20 Jun 2007 in National Assembly: Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii fursa ili nami nitoe maoni yangu. Ningependa kusema kwamba Bajeti ya mwaka huu ilikuwa nzuri zaidi ikilinganishwa na ile ya miaka iliyopita. Kwanza, Bajeti hiyo imewapa akina mama pesa. Ukimpa mama pesa, kwa mfano, yule anayeuza tomato, itamsaidia. Si rahisi kwa akina mama kufanya biashara zao zianguke. Wao ndio wametusomesha kwa kutumia pesa zile kidogo ambazo wamepata. Pia, wamesomesha hata mabwana na watoto wao. Sijasema kuwa vijana wasipewe pesa lakini ninashukuru kwa kuwa wanawake wamepewa pesa ili wajue kufanya biashara. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lilonifurahisha zaidi ni kuwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus