All parliamentary appearances
Entries 21 to 28 of 28.
-
27 Mar 2007 in National Assembly:
Tukiendelea hivyo, hata mimi nitafikiria kama nitajiunga na ODM(K) nione kama nitapewa Hummer kwa sababu siwezi kuinunua. Ni lazima viongozi wetu waseme wanavyotaka kufanya. Nikizungumzia jambo lingine, watu wamewatumia vijana vibaya. Kama ningetumiwa vibaya, singekuja Bungeni. Niliomba kura kwa watu wangu nikitumia baiskeli. Hakuna mtu aliyesema kuwa nilikuwa naomba kura na kwa vile ninampinga mtu fulani yafaa nichomwe. Hata juzi nilijaribu kusema kuwa vile rafiki yangu mhe. Wamwere alifanyiwa si vizuri. Lakini nilisema kuwa si chama kinachofanya hivyo; ni watu. Watu wasifanye kitu na wasingizie chama. Kwa yale mambo nilifanyiwa huko Mwingi, sikuona chama cha ODM(K) pale. Ni watu walipanga! ...
view
-
27 Mar 2007 in National Assembly:
Asante, Bw. Spika. Wakati mwingine ukiona jambo, unaponyokwa na maneno. Sikuwa nikizungumza hivyo kwa ubaya. Walisikika wakisema: "Mhe. Ndile ameshikwa sikio! Mhe. Ndile ni chawa; ameondolewa!" Walionekana!
view
-
27 Mar 2007 in National Assembly:
Bw. Spika, siyataji majina yao sasa, lakini kuna watu ambao walionekana. 116 PARLIAMENTARY DEBATES March 27, 2007
view
-
27 Mar 2007 in National Assembly:
Nasema hivyo kwa sababu hao watu walisikika wakisema: "Vile mwingine amesema, nimeweka sahihi, eti mhe. Ndile ameondolewa." Ni hao watu! Ni lazima siasa zetu ziwe za kukubaliana kimawazo. Niliwasamehe na sitaki kurudia hayo maneno lakini sitaki kuona vijana wakitumiwa vibaya. Vijana ni lazima waanze kufunzwa. Mimi nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa ukoo wetu nikiwa na miaka 28. Nilimuuliza baba yangu ni kwa nini wazee walinichagua na kama ningeweza kutatua matatizo kama vile baba yangu angekosana na mkewe. Waliniambia nisijali kwa maana siku kama hiyo ikifika, watatafuta wazee wa kusuluhisha hayo mambo, maana ni makubwa kuliko mimi, ijapokuwa walikuwa nyuma yangu. Ni ...
view
-
27 Mar 2007 in National Assembly:
Profesa mzima!
view
-
22 Mar 2007 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Spika. Umemsikia Waziri Msaidizi wa Habari na Mawasiliano akisema kwamba wafuasi wa chama cha NARC(K) walijaribu kumchoma na hali tunaelewa kwamba ni mpinzani wake, Bw. Ngunjiri, ndiye alitenda jambo hilo. Je, ni haki kwake kusema hivyo?
view
-
29 Mar 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, naomba kujibu Swali hili wiki ijayo kwa sababu nililipokea ofisini jana, lakini kazi ya kulijibu haikukamilika.
view
-
29 Mar 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, nitajaribu kulijibu kesho.
view