Kibwana Kivutha

Born

13th June 1954

Post

30521, Kenya

Link

Facebook

Telephone

0721353057

Telephone

+254-20-221291

All parliamentary appearances

Entries 311 to 320 of 465.

  • 24 Nov 2022 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. Veronica Maina. Kusema kweli, huu mjadala unatatanisha sana. Tumeona kweli waschana wetu wameumia, wamenajisiwa, wananyimwa pesa na waajiri wao na kunyimwa chakula, wanapokonywa pasipoti na simu zao ili wasiweze kuwasiliana na Familia zao. Hii ni kisa tu cha waschana wale tunaona. Nashuku pia kuna vijana wetu ambao wanalawitiwa na hawawezi kuzungumziwa kwa sababu wanaona haya, ambao. Vijana pia hueenda kutafuta kazi hizo za nyumbani. Bi. Spika wa Muda, haya ni mateso tumeyaona kwa hawa watoto wetu, dada zetu na ndugu zetu. Kusema ukweli, Serikali ingechukuwa sheria kali ... view
  • 24 Nov 2022 in Senate: na kupata ugonjwa wa kiharusi na kutojiweza kabisa. Kusema kweli, inasikitisha sana. Bi. Spika wa Muda, juzi tulitembelewa na balozi wa Qatar. Alisema ni kweli ameona Wakenya nchi yao na wanazungumza vizuri sana. Ukifika Doha vile Seneta Orwoba amesema, Wakenya ndio wanakukaribisha kwa furaha. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Mimi pia nimekuwa hapo na kusema ukweli, wale Wakenya niliowapata -kwa sababu kusema kweli Airport ya Doha ni ya Wakenya- kila mtu anakuonyesha furaha. Ilibidi niulize kama ni airport ya Wakenya au wameajiriwa. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Nilipozungumza na hao Waarabu, walisema wanapenda Wakenya. Wao huajiriwan zaidi kwa sababu ya bidii yao ya kufanya kazi na pia kuwa watu wazuri sana. Balozi wa Qatar, Jabor Bin Ali, alipotembelea Bw. Spika aliuliza kwa nini hatujasikia mambo ya Qatar. Pia alisema kama kuna shida kama hiyo, twende kwa Balozi, tukae chini tuweze kuiangalia kwa kinaga ubaga. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Kila Mara, mimi huuliza kwa nini ni Saudi Arabia peke yake? Kwingine kwaonekana lakini sana ni kwa Saudia na mpaka sasa sijaelewa. Nataka kueleza Seneta Veronica Maina ya kwamba juzi nilikuwa na Balozi wa Saudia aliyerudi tu juzijuzi. Alinipa kadi yake na akanialika kwake kuzungumzia jambo hili. Kitu cha kwanza nilizungumza naye ni hayo mambo ya vijana wetu kwenda kule na kusumbuliwa, kuadhibiwa na kuuliwa. Alisema labda tukae chini kuzungumzia haya mambo. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Ningetaka kumwalika Seneta Veronica Maina ile siku tutakuwa na nafasi twende naye kwa sababu Balozi wa Saudia amenialika kwake ili tuzungumzie mambo haya. Pia, ningeomba “hustler Nation” kwa hii Serikali ya Mhe. Rais William Ruto itafute nafasi na kupea watoto wetu kazi hapa. Tusiwasumbue sana. Watoto wetu wanaenda kutafuta riziki yao kwa sababu imekosekana hapa. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Tuliambiwa mama mboga na vijana wote watasaidiwa na pia kuna mambo ya “bottom-up.” Serikali hii imepewa nafasi ionyeshe ubingwa wa kupea vijana wetu kazi. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: La mwisho, nawapa pole wazazi na familia za wale wote wamepoteza watoto wao na ndugu zao huko Saudi Arabia. Inasikitisha sana kuona maiti ikiletwa kila siku. Kwa nini Saudia Arabia? Saudia Arabia iko karibu na kule sisi Waislamu tunaita Mecca. Tunashangaa ni kwa nini unyama huu unatendewa watu wetu wetu. Sisi tunajua Wakenya wana bidii katika kazi na wengi wao ni waaminifu. Labda nchi zingine zinalia vile sisi tunalia kwa hawa watu wetu. view
  • 24 Nov 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, hili ni jambo la unyama na kusikitisha. Tunaomba Serikali ya Kenya na ya Saudi Arabia zitatue haya mambo. Pia, tuone wale waliotendewa unyama wakirudishwa au kulipwa fidia. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus