29 Jun 2016 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Temporary Deputy Speaker.
view
29 Jun 2016 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. Because this Motion has been discussed for long, can I ask that the Mover be called upon to reply?
view
13 Apr 2016 in National Assembly:
On a point of order.
view
13 Apr 2016 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. Mr. Mithika Linturi must apologise to this House for saying that this is the first time for Mr. Karithi to speak in this House. This is very bad. He has to apologise. It is untrue.
view
29 Mar 2016 in National Assembly:
Asante, Naibu Mwenyekiti wa Muda. Yangu ni machache sana ambayo ni kusema ya kwamba afya ya binadamu ni ya maana sana duniani. Serikali yetu ambayo inaongozwa na Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta na Mhe. Ruto imefanya kazi nzuri kwa Wakenya. Wamefanya kazi ya kutoa pesa katika Serikali Kuu na kupeleka mashinani. Ikipelekwa pale mashinani unakuta wengine hawana heshima na hawana mipango yoyote kwa hizo pesa. Zikifika kwao, zinaingia mifukoni ya mabibi.
view
29 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda, wakati tunaongea mambo haya, ni lazima tukumbuke nyumbani kwa sababu ndio imetuleta hapa. Kama sio wale watu wa Meru ama watu wa Tigania Mashariki ambao walinipigia kura, singeweza kuja katika Bunge hili. Wakati ninaongea, akili yangu hainionyeshi Kenya nzima, bali inanionyesha Watigania na jamii ya Wameru. Ndivyo ninasema Wakenya wajue ya kwamba pesa zote ambazo zinaenda kwa afya, zinapitia katika Bunge letu ambapo Mhe. Kajuju yuko na wewe ukiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda. Sikumaanisha ya kwamba ni gavana analeta pesa. Tunazipitisha zinapelekwa Kericho, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. ...
view
29 Mar 2016 in National Assembly:
Kilifi, Mombasa na Meru. Zikifika kule Meru, zinakuwa za mtu mmoja. Naiunga mkono Serikali lakini imekuwa na ukora mwingi ambao haufai. Naunga mkono.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ugonjwa wa saratani ni shetani kwa sababu uliuwa mama yangu. Mimi niliweza kuzunguka na yeye Kenya nzima. Hakuna mahali sikuenda na yeye. Tulikuwa na uwezo wa kumnunulia dawa lakini baadaye, pesa ziliisha kwa sababu ya huo ugonjwa. Kule mashinani, watu wengi hawana uwezo wa kuja huku Nairobi kutibiwa. Saa hizi, mtu akipatikana na huo ugonjwa, anajua ya kwamba yeye anaenda kufariki.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Kama ingewezekana, tungekuwa na madaktari kule kwenye kaunti ambao watawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kuja Nairobi. Ukiangalia mwaka huu kuanzia Januari, wake wa magavana wa serikali za kaunti wamekuwa wakitembea kule mashinani na magari wakiwashughulikia wagonjwa wa saratani. Zile pesa ambazo serikali za kaunti zimepewa za kuwashugulikia watu hao hawangepatiwa. Pesa hizo zingebaki kwa Serikali Kuu. Serikali Kuu ingeweza kuwachagua madaktari ambao wangewashugulikia watu hao. Tungefanya hivyo kuliko kutuma hizo pesa za ugonjwa wa saratani kwa serikali za kaunti. Serikali za kaunti siku hizi zimekuwa za “wanyama” ambao hata hawajali mambo ya watu. Wanajali mifuko yao.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Namuunga mkono Bi. Wanga kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Watu wengi sana wanahangaika kule mashinani. Nikimalizia, ningependa kusema ya kwamba ugonjwa huo ni mbaya sana na kila mtu anauogopa. Nimemsikia Mheshimiwa akisema watu wengi wanaogopa kwenda kupimwa. Ndani ya Bunge hili, tuko Wabunge wengi. Hatuwezi kukosa wawili ama watatu ambao wako na ugonjwa huo. Hata mimi naweza kuwa nao. Lakini naogopa kwenda kupimwa na nipatikane na saratani kama ile ya mama yangu halafu nife.
view