23 Mar 2016 in National Assembly:
Kama inawezekana, tuwe na madaktari kule mashinani wa kuwashughulikia watu hao. Nikimalizia, nawaeleza Wakenya ambao wanatusikiliza tukiongea kwamba pesa ambazo zinapelekwa kwa serikari za kaunti zinapitia katika Bunge hili kama Bajeti. Kwa mfano, tunajua pesa za Kajiado, Kilifi, Mombasa, Nairobi, Kericho na Meru ni ngapi. Hizo pesa ni nyingi na zimepewa kaunti ili washughulikie hospitali lakini zikifika huko, hazishughulikii mwananchi wa kawaida aliye na taabu nyingi sana. Ukienda Hospitali ya Meru, haiko vile ilivyokuwa wakati wa Rais mstaafu Kibaki au “Nyayo”. Ilikuwa safi sana na haikuwa na harufu yoyote. Hivi sasa, watu wanaoishi karibu na chumba cha kuhifadhia maiti cha ...
view
17 Dec 2015 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Yangu ni machache na ningependa kumuunga Rais mkono kwa kazi nzuri aliyoifanya. Ningependa kusema kwamba uchaguzi unapofanywa nchini Kenya, nchi nzima inafaa kuangaliwa kwa sababu watu wote ni wa Mungu. Kutoka wakati wa enzi ya Rais Moi, Tigania Mashariki na Magharibi hawajawahi kupata Katibu Mkuu au Waziri. Lakini naunga Hoja hii mkono kwa sababu imetoka kwa Rais.
view
17 Dec 2015 in National Assembly:
Kama viongozi Bungeni, pia sisi tunafaa kuitwa na kumshauri Rais maeneo ambayo yanafaa kupewa nafasi kusimamia ofisi mbalimbali katika Serikali. Rais amefanya kazi nzuri.
view
17 Dec 2015 in National Assembly:
Katika Bunge hili, mtu anapokosoa Serikali inasemekana kuwa anapinga Serikali. Sijapinga Serikali lakini watu wote lazima wachukuliwe sawa. Wanatigania tuko wengi. Wakati wa kupiga kura, Mlima Kenya huwa na nyasi na mtu wa Mlima Kenya huambia Wanatigania anawapenda wampe kura. Lakini ikifika wakati wa kula na kugawa, Mlima Kenya humea nyasi na Mtigania haonekani tena. Wakati umefika bendera ya Mtigania ipande juu ili aweze kuonekana nchini Kenya.
view
17 Dec 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
10 Jun 2015 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii.
view
10 Jun 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kuniokoa hapo. Ninaunga mkono Hoja hii. Kule ninakotoka ni shida kubwa sana mtu kuoa. Hii ni kwa sababu watu wengi hawawezi kupata vyeti vya ndoa. Zamani vyeti hivyo viligharimu Ksh100. Hivi leo nafikiri vinagharimu Ksh500. Kuna mahali kwingine vinagharimu Ksh1,200. Kwa hivyo, imekuwa shida kubwa sana. Kama inawezekana, vile mheshimiwa mwenzangu amesema ni muhimu watu wapelekewe hivi vyeti kule mashinani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
10 Jun 2015 in National Assembly:
Jambo lingine ni kwamba siku hizi sisi wanaume tuna taabu sana ya kuoa akina mama. Ukisoma magazeti kila siku utaona kwamba akina mama wamekuwa wakiwapiga na hata kuwaua wanaume. Kuna wanaume ambao wanatafuta pesa kwa taabu sana. Wakati umepata pesa, mwanamke atasema eti lazima ufe ndio abaki na mali. Kwa mfano, angalia mambo yanayotendeka huko Nyeri, ambayo yamesimuliwa katika magazeti. Sisi wanaume tuna taabu. Ni lazima tutafute kufuli na mabati ili tujikinge kwenye nguo zetu ndiposa vitu vyetu visiende - imekuwa shida. Ona sasa huko Nyeri mtu aling’olewa “mizigo” yake na hali hiyo “mizigo” ndiyo inasaidia mama. Hiyo “mizigo” imesaidia ...
view
10 Jun 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia gazeti la leo la The
view
10 Jun 2015 in National Assembly:
, katika ukurasa wa tatu, utapata “mizigo” ya mwanaume. Unaelewa “mizigo” ya mwanaume. Hatuwezi kuitaja lakini kila mtu anaielewa. Wanawake wa Nyeri wakifanya harusi, baada ya kupewa vyeti, wanangoja wakati wanaume wamelewa pombe ama wamelala kisha wanakuja na kisu na kung’oa kila kitu. Sisi wanaume tumechokeshwa na hawa akina mama. Ndio maana nasema hata ni shida kuunganishwa katika ndoa. Mimi natetea wanaume kwa sababu wanawake wamekuwa shida kwetu. Lazima tuende polepole na tuelewane na akina mama kwamba, “Mimi nimekuoa uwe bibi yangu. Nimeunganishwa na wewe na kuwekwa pete na nitakaa pamoja na wewe.” Hakuna maana ya mama kutoheshimu bwana yake. ...
view