All parliamentary appearances

Entries 1 to 7 of 7.

  • 16 Jul 2013 in Senate: Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuunga Hoja hii mkono. Kwanza kabisa, namshukuru Sen. Elachi kwa kuleta Hoja hii hapa. Pili, ningependa kuchangia kwa kusema kwamba kwa kweli tumewakumbuka vijana, haswa walemavu. Kwa upande wa walemavu, unapata ya kwamba sisi hatuna shule ambayo inawafunza vijana. Kwa hivyo, yatakikana vijana wawe waangalifu na wafanye zile kazi wanazopewa. Ningependa pia kuomba kuwa Serikali inapoajiri, iajiri vijana na ikumbuke walemavu kwa sababu vijana walemavu wako na nafasi chache zaidi. Tukiangalia haswa wakati askari wanapoajiriwa, vijana walemavu hawawezi kufanya kazi ya uaskari. Kwa hivyo, tunafaa kuwaangalia kwa upande huo pia. ... view
  • 4 Jul 2013 in Senate: Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir for according me this opportunity. I want to thank Sen. Kagwe for responding to issues regarding the laptops programme. However, I would like him to remember the disabled people. We have blind pupils in our schools. Can a blind pupil in class one use a laptop? When they are sourcing for these laptops, I urge them to consider such pupils. Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 3 Jul 2013 in Senate: Bw. Spika, asante sana kwa kunipa muda. Kwanza nashukuru daktari kwa kuleta Hoja hii kwa sababu ni ya maana sana. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ukiangalia katika familia, utapata watu wanakosana kwa sababu ya kelele ambayo inasababishwa na dawa za kulevya na pombe harama. Maafa katika jamii yamezidi kwa sababu ya madawa ya kulevya. Utapata kwamba mtu akiwa safarini, anapewa tu peremende na kisha anaaga dunia na baadaye inapatikana kwamba alipewa madawa za kulevya. Bw. Spika, ukiangazia juu ya pombe haramu ya kumi kumi, utapata kwamba inafanya watu wengi kupoteza macho ama kuwa vipofu. Kwa upande mwingine, tunaona ... view
  • 18 Jun 2013 in Senate: Asante Bi Spika wa Muda kwa wakati huu ulionipa ili niweze kuchangia Hoja hii. Kwa upande wangu, ninashukuru sana kwa sababu ya Hoja hii. Kwanza ukiangalia kwa upande wa usafiri, unapata kwamba hizi hospitali ziko mbali sana. Kwa mfano wakati mwingine unapata mzazi amebeba mtoto wa miaka kumi na anatembea kwa muda mrefu kwa sababu hakuna usafiri bora. Pia kuna upungufu wa madaktari. Kwa mfano, unapata hakuna daktari ambaye anaweza kusaidia mtoto ambaye ni kiziwi. Hakuna madaktari wanaoweza kutumia signlanguage . Inafaa madaktari washughulikie walemavu. Ninaunga mkono Hoja hii. view
  • 24 Apr 2013 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir, for giving me this time. Mwanzo kabisa, nina furaha kwamba Rais wetu, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto, walichukua usukani na tutafanya kazi pamoja nao. Kwanza, ninawashukuru kwa sababu walitukumbuka sisi kama walemavu na nimefurahi. Pili, nashukuru chama ambacho kilinichagua kama mama kuwakilisha walemavu kwa sababu ni wengi ambao wangeweza kufika hapa lakini chama cha TNA kiliona ni vyema nije Bunge kuwakilisha wale walio walemavu. view
  • 24 Apr 2013 in Senate: Bw. Naibu Spika, nashukuru Katiba ya sasa ya Kenya kwa kuwakumbuka walemavu. Ni mara nyingi ambapo tumefikiria sisi tutakumbukwa lini lakini sasa tunashukuru sana kwa sababu tumekumbukwa. Nikirudi katika Hotuba ya Rais, hii ilinifurahisha sana. Tulipoona kwamba tulikumbukwa kama walemavu, hakika tulifurahi. Nikianzia na swala la elimu, jambo la elimu kwa mtoto mlemavu limekuwa ngumu sana. Lakini kwa wakati huu, tumefurahi kwa sababu tumeona kwamba tunakumbukwa. Tunahitaji vifaa kama vile brailers,scratches na vingine vingi. Tunaomba kwa sababu Serikali imetukumbuka, wakati inapopeana tarakilishi, nasi pia tukumbukwe wakati huo. Pili, katika mambo ya tarakilishi, naona ninaweza kuwasaliti lakini sio sana kwa sababu ... view
  • 24 Apr 2013 in Senate: Katika upande wa michezo na kazi zingine tofauti, kuna michezo tofauti ambayo walemavu wanaweza kuhusishwa kama vile michezo ya mipira. Vipofu hucheza michezo ya mipira. Ninajua kwamba hakuna kitu ambacho mtu mlemavu hawezi kufanya. Tupatie The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus