All parliamentary appearances
Entries 5371 to 5380 of 6328.
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Waheshimiwa Wabunge, ninaomba kutoa Hoja ijadiliwe.
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Kabla tuanze huu mjadala, ningependa kutumia huu wakati kuwatambua wanafunzi kutoka Shule ya Upili ya Wasichana ya Mwasere, Eneo Bunge la Mwatate, Kaunti ya Taita Taveta. Wameketi kwenye Ukumbi wa Umma. Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Jumba hili lote, ninawakaribisha. Nafasi hii itamwendea Mbunge wa Laikipia Kaskazini, Mhe. Sarah Korere.
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Asante, Mhe. Sarah Korere kutoka Laikipia Kaskazini. Tunapoendelea, ningependa kuwakumbusha kwamba tunatawaliwa na sheria zetu – Kanuni za Kudumu. Hata ingawa haukubaliani na maneno yaliyosemwa na mtu mwingine: “87 (1) Hairuhusiwi kudhalilisha mwenendo binafsi wa Rais, Spika, Jaji ama mtu yeyote anayetekeleza majukumu ya kimahakama…” Ni vyema pia tutilie hayo maanani katika michango yetu na tuweze kufuata sheria vilivyo. Nataka nimpe sasa wakati huu, Mbunge wa Kinango, Mhe. Gonzi Rai.
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante Mbunge wa Kinango. Ninampatia nafasi hii Daktari James Nyikal, Mbunge wa Seme.
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante Daktari. Muda wako umeyoyoma. Tutampa nafasi hii Naibu Kiongozi wa Chama cha Walio Wengi Bungeni, Mhe. Owen.
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Wabunge, tafadhali tutilie maanani Kanuni ya Kudumu 77: “77. (1) Shughuli zote za Bunge la Taifa zitaendeshwa kwa Kiswahili, Kiingereza au Lugha Ishara ya Kenya. (2) Mbunge anapoanza kutoa mchango wake katika lugha yoyote kati ya zile zilizotajwa katika aya ya (1), ataendelea kwa lugha hiyo hadi mwisho wa mchango wake.” Tusichanganye lugha. Tufuate sheria zetu.
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Hoja yako ya nidhamu ni gani, Mhe. Tandaza?
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Mhe. Gikaria wa Nakuru Mashariki, hoja yako ya nidhamu ni ipi?
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Ahsante, Mheshimiwa Gikaria.
view
-
15 Mar 2023 in National Assembly:
Kabla Hoja yoyote ifike mahali hii imefika, kuwa mjadala katika Ukumbi huu, lazima imepitia mikono ya wanasheria wetu, ikahakikishwa kwamba haijaenda kinyume na Katiba, na ikawasilishwa hapa kwa haki. Kwa hivyo, tutilie hilo maanani. Mheshimwa Owen Baya, tafadhali. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view