Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 2123.

  • 29 May 2025 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Sen. (Dr.) Khalwale kuhusu kucheleshwa kwa kumalizika kwa miradi kadhaa katika Kaunti ya Kakamega. Hili limekuwa donda sugu katika kaunti nyingi. Utapata Magavana wanaingia ofisini na kupuuza miradi iliyoanzishwa na magavana waliotangulia. Kwa mfano, kule kwetu Mombasa kuna miradi ya ECDE ambayo hivi majuzi tuliizuru tukiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu katika Seneti. Tulizuru ECDE ya Kengeleni ambayo ilianzishwa 2016, Chaani pia, 2016 na nyingine nyingi ambazo zimekwama. Hivi sasa wananchi wanalalamika kwamba hakuna huduma zinazotolewa katika majengo hayo. Wanakandarasi wanaendelea kupata shida kulipwa pesa ... view
  • 29 May 2025 in Senate: Bw. Naibu Spika, tuliona pia katika maeneo ya Likoni, Shonda kuna hospitali iliyoanzishwa na ikakamilika, lakini mpaka sasa haijatumika. Wananchi pale wanapata shida kwa sababu zahanati zilizopo pale hazitoshi. Hospitali hiyo ingetoa huduma muhimu kwa wananchi wa sehemu zile. view
  • 29 May 2025 in Senate: Hii Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kanda isikomee Kakamega. Ivalie suala hili njuga na kutembelea kaunti zote, ili kubaini miradi iliyokwama ambapo fedha nyingi zimeingizwa wakati hakuna chochote kimepatikana kwa muda wote huu. view
  • 27 May 2025 in Senate: On a point of order, Mr. Temporary Speaker, Sir. view
  • 27 May 2025 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, I usually do not like interrupting a colleague’s thoughts during his presentation in this House, but I heard Sen. (Dr.) Khalwale talk of the theft at Ketraco. He is casting aspersions on the person of the Governor of Kakamega County. I do not think that is right because there are no accusations levelled against that Governor in this House to warrant such blatant attack and violation of our Standing Orders. Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. view
  • 27 May 2025 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii pia kuchangia kuhusu Hoja ya kupeleka fedha katika kaunti zetu. Yangu yatakuwa mafupi kwa sababu wengi wamechangia. Kwa hivyo, singependa kurudia. view
  • 27 May 2025 in Senate: Jambo la kwanza ni kwamba ipo haja kuwa na sheria ambayo itasaidia kaunti zetu kupata fedha ambazo zinapelekwa kwa Serikali ya Kitaifa na baadaye zinarudi kwa kaunti. Kwa mfano, faini zinazotozwa katika mahakama zetu kwa makosa kuhusiana na sheria ambazo zinasimamiwa na kaunti. Kuna sheria kuhusu ujenzi, wale wanaouza bidhaa kwa rejareja bila vibali na sheria nyingine kama hizo. Pesa hizo zinalipwa kwa Serikali ya Kitaifa inayokaa nazo kwa zaidi ya mwaka kisha baadaye inaleta Mswada Bungeni ili upitishwe. Kwa mfano, pesa zitakazopelekwa mwaka huu zilikusanywa mwaka 2022. Ipo haja ya kuhakikisha kuwa pesa hizo zinaenda moja kwa moja katika ... view
  • 27 May 2025 in Senate: Jambo la pili ni kuhusu royalties zinazolipwa katika kaunti zetu. Nitatoa mfano wa base titanium . Walienda Kwale wakachimba madini na sasa wamefunga. Hata hivyo, pesa zilizolipwa kwa Serikali ya Kitaifa hazijaenda katika Serikali ya Kaunti ya Kwale ili kufaidi jamii ambapo uchimbaji huo ulikuwa ukifanyika. Kaunti ya Kwale inadai karibu shilingi bilioni moja. Hizi ni pesa ambazo ni view
  • 27 May 2025 in Senate: ambazo zilienda kwa Serikali ya Kitaifa lakini hazijalipwa kwa Serikali ya Kaunti ya Kwale. Vile vile, karibu Shilingi milioni 700 zinastahili kulipwa kwa kamati katika maeneo ambapo uchimbaji ulikuwa unaendelea. Hata hivyo, pesa hizo hazijalipwa na Serikali ya Kitaifa. view
  • 27 May 2025 in Senate: Bw. Spika wa Muda, tutapendekeza katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchimbaji wa Madini kwamba Serikali ya Kitaifa, serikali za kaunti na jamii zinazoathirika zipokee royalties zao kando kando. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus