27 May 2025 in Senate:
Kwa hayo mengi, Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii.
view
14 May 2025 in Senate:
Mhe. Spika, pia mimi najiunga na Maseneta waliotangulia kuchangia Hoja hii kwamba yanayoendelea katika Kaunti ya Nyamira ni makosa. Hoja hii ilipokuja kwa mara ya kwanza, kabla ya Kamati kuambiwa ichunguze, suala hili lilikuja katika hali isiyokupendeza. Kuna bunge mbili katika Kaunti ya Nyamira yanayotoa mwongozo tofauti kwa serikali ya Kaunti ya Nyamira. Ni lazima Gavana wa Kaunti ya Nyamira alaumiwe kwa sababu yeye ndiye msimamizi mkuu wa mambo yote. Ijapokuwa Bunge la Kaunti lina nafasi ya kufanya maamuzi yake kibinafsi, masuala yote yanapitia katika meza yake. Ni aibu kwamba hata baada ya Kamati kwenda, mabunge yale mawili hayakuweza kuamua ...
view
14 May 2025 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Asante, Waziri, kwa kuja asubuhi hii ya leo. Swala langu ni kuhusu malipo ya SHA. Je, inakuwaje wakati mgonjwa, kwa mfano, anapofanya operation, SHA inasisitiza kwamba lazima alipe malipo ya zaidi ya miaka miwili ili aweze kupata huduma anayohitaji, aidha ya operation ama ya kulazwa kwa matibabu fulani ambayo ni ya kitaalamu? Nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kwamba wanalazimishwa kulipa subscriptions za miaka miwili au miaka miwili na nusu ili waweze kupata huduma hiyo kutoka kwa hospitali zao. Asante. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version ...
view
13 May 2025 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I rise pursuant to Standing Order No.56(1)(b) of the Senate Standing Orders to make a statement regarding the activities of the Standing Committee on Land, Environment and Natural Resources during the period February to April 2025. The Standing Committee on Land, Environment, and Natural Resources is established under Standing Order No.228(3) of the Senate Standing Orders. It is mandated to consider all matters related to lands and settlement, environment, forestry, wildlife, mining, water resource management and development as well as aspects of climate change During the period under review, the Committee held 23 meetings. It ...
view
13 May 2025 in Senate:
invitations to appear before the Committee. These invitations were to address pending legislative business, including 27 statements and seven petitions. This has slowed the Committee's output. Consequently, the Committee has resolved to summon the Cabinet Secretary to appear before it, initially on 8th May, 2025 and now on 14th May, 2025, to address the aforementioned matters. In addition, written responses have been sought, with some still pending before the National Land Commission (NLC). The Committee is scheduled to meet the Commission on 15th May, 2025, which is on Thursday this week. During the period under review, the Committee considered the ...
view
13 May 2025 in Senate:
During the period under review, 13 Statements were considered and dispatched to the relevant Senators. A detailed analysis is annexed. Given the large number of statements before the Committee, a more comprehensive updated tracker is available, providing their status. In conclusion, I wish to thank the Office of the Speaker and the Office of the Clerk of the Senate for their continuous support accorded to the Committee while undertaking its work. I also extend my gratitude to the Members of the Committee for their commitment, diligence and contributions during the Committee’s activities. I thank you.
view
13 May 2025 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninachukua fursa hii kuongeza kauli yangu kwa hii taarifa iliyoletwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu kuhusu uteuzi wa makamishna wa IEBC. IEBC ni kiungo muhimu cha uchaguzi katika nchi yetu ya Kenya na makamishna hawa pamoja na mwenyekiti wao watakapofanya kazi, itakuwa ya kuangalia uchaguzi wa Rais, magavana, maseneta, wabunge wa Bunge la Taifa na vile vile wabunge wa kaunti. Uteuzi wao lazima upitie katika Bunge la Seneti kwa sababu Seneti ina linda masilahi ya ugatuzi; bunge za kaunti na masilahi ya magavana. Haiwezekani kwamba sheria inayotumika kuwachagua ni ile ambayo iliyofanywa ...
view
13 May 2025 in Senate:
Bw. Spika, natoa kauli yangu kushinikiza kwamba ni lazima uteuzi wa makamishna wale ufike katika Bunge la Seneti ili kuona kwamba haki inatendeka katika uteuzi huo. Asante, Bw. Spika.
view
8 May 2025 in Senate:
Asante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia maombi ya Taarifa yaliyoletwa Bungeni na Sen. Hamida. Ni kweli kwamba baadhi ya mashirika ya ndege yanayohudumu katika nchi yetu, hususan Turkish Airlines na mengineyo, huduma za viwango vya juu wanazotoa yanaacha maswali mengi kuulizwa kuliko majibu. Nilibahatika kusafiri kwa ndege ya Turkish Airlines kuenda Istanbul hivi majuzi. Huduma za Business Class kwa ndege ile ni tofauti za zile zinazotolewa kwa kiwango hicho hicho kwa ndege zinazosafiri kutoka Istanbul kuenda maeneo mengine kama Europe, America na Asia. Haiwezekani ndege ile ile itoe huduma tofauti kwa watu wanaokuja Africa na wale wanaoenda sehemu ...
view
6 May 2025 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kujiunga na Maseneta wenzangu pamoja na wewe kutoa rambirambi zetu kwa mwendazake Mhe. Charles Ong’ondo Were. Mwaka juzi tulitembelea nyumbani kwake tukiwa tumekwenda mkutano kule Homa Bay na akatufariji kwa chakula cha mchana siku hiyo. Tulijua kweli alipendwa na watu wake na hakuwa mtu wa kutaka makubwa. Mara nyingi utampata hapa Bunge akifanya kazi yake bila kufanya mambo isiyo ya kawaida. Kwa hivyo, kifo chake ni pigo kwa chama chetu cha ODM, Bunge na taifa. Ninasema hivi kwa sababu ameuliwa katika hali ambayo inatatanisha. Bw. Spika, usalama umezorota nchini. Kuna haja ya taasisi ...
view